Wanafunzi wenye IQ kubwa ni wale waliopata division 1 shule za kata hasa vijijini, wana upeo mkubwa wa kusoma bila walimu, tuition, past papers

That is correct.
 
Kumzidi GPA chuo sio kigezo kabisa, kwanza mmesoma course moja? Afu hawa waseminari wengi wakifika chuo wanakuwa kama wamezuzuka na mademu plus pombe maana huko shule kwao huwa wanabanwa sana. My take, tafuta hela mwanao asome shule bora na nzuri asiwe anakariri madesa kama wewe
 
Kimsingi kama kwenu mmezaliwa mna akili ni mnazo tu..

Kwetu tumezaliwa tuko 7 na wote ni A-List.

Tumesoma shule za kata wote, mimi ordinary nilipata div 2 ya 21, advance nikaichapa div 1 ya 6.

Wote wanaofuata ni mwendo wa one one tu, na wako shule za kawaiiiiiida kabisa..
 
Yani 2.21 nawe unajiita kipanga?
Tukianza kuringishiana hapa matokeo ya secondary si utakimbia wewe?
 
📌📌📌ENDELEENI KUBISHANIA UJINGA UJINGA ILA HAKIKISHA HUYO MTOTO WAKO ANAMALIZA SHULE NA AJIRA APATE KWENYE MASHIRIKA YA KIMATAIFA,KITAIFA AU KWENYE TAASISI, SIO HALMASHAURI😁😁😁

TOFAUTI NA HAPO KAMA UNATUMIA GHARAMA NYINGI HALAFU MTOTO ANAMALIZA SHULE. ANAOMBA KAZI HUKO HALMASHAURI FIKIRIA VIZURI HUO UWEKEZAJI WAKO.
 
Wane prove wako vizuri licha ya mazingira magumu, prblem is hayo mazingira magumu yatawakatisha tamaa wasipotoka huko
 
Hao St LIKUD wanafaulu kwa kukariri, hawana IQ yoyote kubwa! wanakariri toka mwanzo wa kitabu hadi mwisho ila hawaelewi vzr walichokikariri.
Mtu aliyeongoza kitaifa Kwenye mtihani wa Physics A-level mwaka 2013 elimu yake ya O-level alisoma Government school nafikiri kitu kama Sengerema au huko Kilimanjaro.

Sasa Kwa hii mantiki yako unamaanisha huyo jamaa aliwapiku hadi wanafunzi waliosoma Feza,St.marians,St.Francis Kwa uwezo wake mkubwa wa kukariri na sio kuelewa SI ndio? Tena kwenye somo linalohitaji kuumiza akili kama Physics???

Una assumptions za kipuuzi sana. Na inaonekana umezoea spoon-feeding kwenye kila jambo
 
Hizo shule kama St. Francis wanapokea the best of the best. Yes, mazingira mazuri yanawasaidia lakini watoto wale ni vichwa kwelikweli kutokea huko primary.
Wengi hawajui kuwa shule za vipaji maalumu ziko aina mbili kuna za serikali na za private .Wote huchukua the best kuingia shule zao

Serikali huchukua the best kwenda shule za vipaji maalumu na shule kama St Francis na yenyewe huchukua the best kujiunga nazo

Na wote wakikutaba mtihani mfano kidato cha nne.huwa na ufaulu mkubwa sana lakini shule kama St.Francis huvunja record huchukua vichwa hasa sio utani
 
Tafuta hela.
 
Wane prove wako vizuri licha ya mazingira magumu, prblem is hayo mazingira magumu yatawakatisha tamaa wasipotoka huko
Kusoma mazingira magumu kunachosha ubongo anafika hatua inayofuata ubongo ukiwa umechoka mno

Kuna wengine ni kweli husoma mazingira magumu mfano shule ya sekondari hadi form four yenye mazingira magumu akasoma akafaulu division one akifika form six wengi hu drop huishia kupata division two au three.Sababu ya uchovu wa akili

Kuna umri mtoto anatakiwa kusaidiwa kusoma mazingira mazuri yasiyomchosa sana kiakili umri ukiwa mdogo
 
100%. Fact
 
100% Fact
 
Upewe maua yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…