Wanafunzi wenye IQ kubwa ni wale waliopata division 1 shule za kata hasa vijijini, wana upeo mkubwa wa kusoma bila walimu, tuition, past papers

Wanafunzi wenye IQ kubwa ni wale waliopata division 1 shule za kata hasa vijijini, wana upeo mkubwa wa kusoma bila walimu, tuition, past papers

Mawazo mengine ya ajabu sana! Hebu tumieni akili zenu vizuri
Unamaanisha mwanafunzi mwenye IQ kubwa akisoma shule ya private ile IQ yake haipo tena???
Hebu fuatilia vizuri uone wanasayansi wenye IQ kubwa Duniani uone kama walisoma shule za aina gani?
Umeenda mbali sana huku shule za serikali zina kila kitu kifupi serikali imewekeza kwenye elimu
 
Ambaye hajapita hizo shule hawezi kukuelewa. Just imagine unaingia form one unaanza kufundishwa na mtu kama Askofu Renatus Nkwande, hivi hiyo bahati ya kufundishwa na genius kama huyo utapata wapi? Hapo mwanafunzi anapigishwa topic anailewa nje ndani na siyo kukariri kama hao mnaowafisia wa shule zenu za kata.
Yani akufaulu wa shule ya kata kakariri sio 😂🤣
 
Inapimwa Kwa uwezo wako WA kuleta positive impacts kwenye jamii yako Kwa namna ya upekee, na sio Kwa kupata A saba zote kwenye mitihani ya necta, Halafu wakati huo hata tukikwambia utuletee mpango kazi wa kutokomeza wizi wa TV uliotamalaki huwezi.
Jibu zuri sana hili ✅
 
Hapana. Hii ya kufundisha namna ya kujibu maswali badala ya topic nzima ipo kwenye shule za serikali hasa advanced level.

Hizo shule za kanisa kama St.Francis na seminary huwa wanafundishwa topics zote za silabasi nzima kwa uelewa mpana. Halafu wanafunzi huwa wanalala mapema tu,hawakeshi wanasoma kama Ilboru au Kibaha .

Baadhi ya walimu wanaomfundisha mwanafunzi wa form one seminary kama mapadri unakuta wana elimu yenye level ya kumfundisha mwanafunzi wa chuo kikuu. Mapadri wanapofundisha wanafunzi unakuta wanaichimba topic mpaka kwenye extra ordinary level . Automatically mwanafunzi anayepata bahati ya kufundishwa na ma-philosopher kama hawa lazima atakuwa na I.Q kubwa.

Halafu seminarini au hizi shule za kanisa huwa hawadekezi wanafunzi. Mbali na kusoma , mwanafunzi ana fundishwa kuheshimu muda na kufanya kazi haswa. Mimi kwa uzoefu wangu seminarini muda kujisomea binafsi ulikuwa ni limited na ni mchache sana lakini tulifaulu vizuri.
We unajua ya seminari hujui ya nje ya hapo, hakuna ukwl wwte
 
Kuteseka sio achievement au sifa.
 
Hao wote ni wanakariri. Upeo mkubwa ni mwanafunzi wa shule ya Kata aliyepata 3 na akaenda a level akapata 3 nyingine kisha mnamkuta chuo
 
Back
Top Bottom