Wanahabari kujikita kusifia viongozi zaidi ni kukosa weledi?

Wanahabari kujikita kusifia viongozi zaidi ni kukosa weledi?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Salaam Wanajukwaa,

Hapo zamani ilikuwa ni nadra sana kusikia chombo cha habari kutwa nzima kinasifia kiongozi fulani lakini kadri siku zinavyozidi kwenda imekuwa kawaida na tabia hii inazidi kuota mizizi sana. Unaweza kuta kila kipindi ndani ya dk kadhaa unasikia zinamwagwa sifa za viongozi zingine hata haziakisi uhalisia ila ili mradi tu wanasifia.

Hii inaondoa weledi wa vyombo vya habari kwani watu hutegemea kupata habari au maarifa na si kusikia fulani anaupiga mwingi wakati mwingine ni majukumu yake. Utasiki KIONGOZI FULANI LEO KAFUNGUA JENGO AU DARAJA kutwa nzima ni hivyo ooo huyo jamaa anafanya kazi sana nk. sasa majukumu yake ni nini? Si kafanya jukumu lake kwa nini ageuke kuwa ndio wimbo unaoimbwa na waendesha vipindi vya Radio au televisheni.

Kuna muda nawaza au hizo teuzi za wanahabari kwenda kwenye nafasi za kisiasa ndio zinasababisha kadhia hizi inabidi watu wasifie ili kuweka mazingira ya kuteuliwa kwenda nafasi za kisiasa? Au ni hofu iliyojengeka baina ya vyombo vya habari kuwa watafungiwa kuendesha shughuli zao hivyo husia viongozi ikiwa kama njia ya kujiwekea kinga ya kufungiwa vyombo vyao? Maswali ni mengi bila majibu.

Hii inafanya wananchi kukosa maana halisi ya chombo cha habari kisichokuwa na mrengo wowote wa kisiasa. huwezi tofautisha vyombo vya Serikali, watu binafsi na vyombo vya habari vya vyama vya siasa, wote wanafanya yaleyale.

Ni vyema viongozi wakasifiwa kwenye sifa za maana na kukosolewa wanapokosewa hii itawafanya wasiwe vipofu kuona makosa yao, maana wakilewa sifa hawawezi kuona wanapokesewa kwani kila muda wao wanasifiwa hivyo huona kila kitu kipo sawa na wanaowakosoa wanakosa wanaonea wivu au chuki.
 
Back
Top Bottom