Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Habari Tanzania!
Wakati Klabu ya Simba inakwenda kufanya mabadiliko ya Kiwendeshaji wa Klabu kulikuwa na tafarani nyingi sana za kukatisha tamaa kutoka baadhi ya Waandishi wa Habari za Michezo na Watangazaji pamoja na Wachambuzi, kama haitoshi walikwenda mbali zaidi kudai Uwekezaji haifai na MO anataka kumiliki Simba kwa manufaa yake.
Lakini Wanasimba waliamini kile ambacho wanakifanya na wakajikita kwenye ule msemo kuwa Mchonga Njia Siku Zote Huonekana wa Kushangaza Ila Wapitao Hupewa Hongera.
Lakini cha kushangaza wale Waandishi walikuwa wakiponda Uwekezaji upande wa Simba SC ndo hao hao wanapongeza Uwekezaji upande wa Yanga na kusifia kama vile ni jambo jipya Tanzania ilhali mchakato ni ule kama wa Simba SC 49/51.
Wale Waandishi wa Michezo walikuwa wakiongoza kundi la kuwahoji Wapinga mabadiliko Simba na kumpa muda zaidi Mzee Kilomoni na kumsifia kuwa yupo sahihi, tuwaone tena upande wa Yanga wakifuatwa na kuwahoji wapinga mabadiliko hasa wale Wazee walikuwa na Press Conference makao makuu.
Katika picha mstari wa mwisho hapo, Mzee licha ya kuhudhuria Mkutano lakini hakuthubutu kamwe kunyosha mkono wake kuunga mkono mabadiliko, amepewe muda tusikie maoni yao akiwakilisha Wazee wenzake.
Haiwezekani jambo liungwe mkono asilimia [emoji817] hata kama ni lenye kuleta mafanikio. Hongera sana Simba SC kwa kuwa mfano wa kuigwa kuelekea kwenye mafanikio ya soka Tanzania.