Tabutupu,
Hili bandiko limekosewa.
Oscar Kambona hakuwapo katika kuunda TANU tarehe 7 Julai 1954 wala hakuhusika katika mpango wowote ndani ya TAA wa kuunda chama cha siasa.
Waliohusika na kumtia Nyerere katika TANU wanafahamika na historia hii sasa si ngeni tena.
Nimeieleza hapa Majlis mara nyingi sana.
Hamza Mwapachu na Abdul Sykes ndiyo waliomuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA 1953 katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 Aprili 1953 Nyerere na Abdul Sykes walipogombea nafasi ya urais wa TAA.
Nyerere akashinda akawa rais na Abdul makamu wa rais.
Kuna historia ya kusisimua sana katika uchaguzi huu jinsi Nyerere alivyoweza kumshinda Abdul Sykes lau kama hakuwa anajulikana ila kwa wanachama wachache kama Dennis Phombeah, Mnyasa kutoka Nyasaland na yeye ndiye alikuwa msimamizi (Returnig Officer) wa uchaguzi ule.
Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa Nyerere akiwa rais kama Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walivyopanga nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe mwaka wa 1953.
Kambona alikuja Dar es Salaam TANU imeshaundwa.
Kwa kuwa umemtaja Kambona nitakueleza kitu kuhusu Phombeah.
Phombeah alikuwa rafiki mkubwa sana wa Kambona na yeye kama rafiki yake alikimbilia Uingereza na akafia huko.
Kwa kuhitimisha ningependa kukufahamisha kuwa TAA haikuwa chama cha watumishi wa umma,
Kilichokuwa chama cha wafanyakazi kilikuwa Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) na viongozi wake katika miaka ya 1950 walikuwa Rais Thomas Marealle na Katibu Ally Sykes.