Wanaharakati ndio walio leta Uhuru wa Tanganyika

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Japo walikuwepo wengi lakini mfano mzuri ni Oscar kambona.

Nadhani wanaharakati ni watu muhimu sana katika taifa hili wanahitaji kupewa nafasi na tuwaunge mkono.

IMG-20191227-WA0032.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo walikuwepo wengi lakini mfano mzuri ni oscar kambona.

Nadhani wanaharakati ni watu muhimu sana katika taifa hili wanahitaji kupewa nafasi na tuwaunge mkono.View attachment 1304709

Sent using Jamii Forums mobile app
Walioleta Uhuru walikuwa wanasiasa hawakuwa wahuni waliojificha kwenye uanaharakati.Hata Nyerere aliacha kazi kwa uwazi huku akisisitiza anakwenda kufanya siasa kwenye chama cha siasa.Hakuna wanaharakati kuna wachumia tumbo

Baada ya harakati za uhuru tulianza kazi ya kuleta maendeleo nchini ! Hawa wahuni wa sasa harakati zao ni za nini ? Kama sio za kuturudisha ukolonini kwa mlango wa nyuma ! JPM PIGA KAZI BABA, WATAKUELEWA TUUU !
 
Ukoloni ungalipo tofauti ni Rangi ndo kilichobadilika angalau hata wakoloni weupe walituletea maendeleo
 
Wakoloni weusi ni wachumia tumbo hataree angalia matumbo yalivyojaa gesi CCM
 
Walioleta Uhuru walikuwa wanasiasa hawakuwa wahuni waliojificha kwenye uanaharakati.Hata Nyerere aliacha kazi kwa uwazi huku akisisitiza anakwenda kufanya siasa kwenye chama cha siasa.Hakuna wanaharakati kuna wachumia tumbo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujui siasa wewe wanaharakati hawakwepeki,vilabu vya simba na Yanga havikuwa vyama vya siasa ili vilikuwa vinahifadhi wanaharakati wakipigania uhuru kwa kujificha kwenye hivyo vilabu,vivyo hivyo na Vyama vya Wafanyakazi ,Mzee Kawawa n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walioleta Uhuru walikuwa wanasiasa hawakuwa wahuni waliojificha kwenye uanaharakati.Hata Nyerere aliacha kazi kwa uwazi huku akisisitiza anakwenda kufanya siasa kwenye chama cha siasa.Hakuna wanaharakati kuna wachumia tumbo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujui siasa wewe wanaharakati hawakwepeki,vilabu vya simba na Yanga havikuwa vyama vya siasa ili vilikuwa vinahifadhi wanaharakati wakipigania uhuru kwa kujificha kwenye hivyo vilabu,vivyo hivyo na Vyama vya Wafanyakazi Mzee Kawawa alikitumia kudai uhuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo walikuwepo wengi lakini mfano mzuri ni Oscar kambona.

Nadhani wanaharakati ni watu muhimu sana katika taifa hili wanahitaji kupewa nafasi na tuwaunge mkono.

View attachment 1304709

Sent using Jamii Forums mobile app
Tabutupu,
Hili bandiko limekosewa.

Oscar Kambona hakuwapo katika kuunda TANU tarehe 7 Julai 1954 wala hakuhusika katika mpango wowote ndani ya TAA wa kuunda chama cha siasa.

Waliohusika na kumtia Nyerere katika TANU wanafahamika na historia hii sasa si ngeni tena.

Nimeieleza hapa Majlis mara nyingi sana.

1577479707873.png

Kulia Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968) Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962)
Hamza Mwapachu na Abdul Sykes ndiyo waliomuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA 1953 katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 Aprili 1953 Nyerere na Abdul Sykes walipogombea nafasi ya urais wa TAA.

Nyerere akashinda akawa rais na Abdul makamu wa rais.

1577480262392.png

Dennis Phombeah

Kuna historia ya kusisimua sana katika uchaguzi huu jinsi Nyerere alivyoweza kumshinda Abdul Sykes lau kama hakuwa anajulikana ila kwa wanachama wachache kama Dennis Phombeah, Mnyasa kutoka Nyasaland na yeye ndiye alikuwa msimamizi (Returnig Officer) wa uchaguzi ule.

Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa Nyerere akiwa rais kama Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walivyopanga nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe mwaka wa 1953.

Kambona alikuja Dar es Salaam TANU imeshaundwa.

Kwa kuwa umemtaja Kambona nitakueleza kitu kuhusu Phombeah.

Phombeah alikuwa rafiki mkubwa sana wa Kambona na yeye kama rafiki yake alikimbilia Uingereza na akafia huko.

Kwa kuhitimisha ningependa kukufahamisha kuwa TAA haikuwa chama cha watumishi wa umma,

Kilichokuwa chama cha wafanyakazi kilikuwa Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) na viongozi wake katika miaka ya 1950 walikuwa Rais Thomas Marealle na Katibu Ally Sykes.
 
Unamjua kambona ?
Tabutupu,
Hili bandiko limekosewa.

Oscar Kambona hakuwapo katika kuunda TANU tarehe 7 Julai 1954 wala hakuhusika katika mpango wowote ndani ya TAA wa kuunda chama cha siasa.

Waliohusika na kumtia Nyerere katika TANU wanafahamika na historia hii sasa si ngeni tena.

Nimeieleza hapa Majlis mara nyingi sana.

View attachment 1305221
Kulia Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968) Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962)
Hamza Mwapachu na Abdul Sykes ndiyo waliomuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA 1953 katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 Aprili 1953 Nyerere na Abdul Sykes walipogombea nafasi ya urais wa TAA.

Nyerere akashinda akawa rais na Abdul makamu wa rais.

View attachment 1305226
Dennis Phombeah

Kuna historia ya kusisimua sana katika uchaguzi huu jinsi Nyerere alivyoweza kumshinda Abdul Sykes lau kama hakuwa anajulikana ila kwa wanachama wachache kama Dennis Phombeah, Mnyasa kutoka Nyasaland na yeye ndiye alikuwa msimamizi (Returnig Officer) wa uchaguzi ule.

Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa Nyerere akiwa rais kama Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walivyopanga nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe mwaka wa 1953.

Kambona alikuja Dar es Salaam TANU imeshaundwa.

Kwa kuwa umemtaja Kambona nitakueleza kitu kuhusu Phombeah.

Phombeah alikuwa rafiki mkubwa sana wa Kambona na yeye kama rafiki yake alikimbilia Uingereza na akafia huko.

Kwa kuhitimisha ningependa kukufahamisha kuwa TAA haikuwa chama cha watumishi wa umma,

Kilichokuwa chama cha wafanyakazi kilikuwa Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) na viongozi wake katika miaka ya 1950 walikuwa Rais Thomas Marealle na Katibu Ally Sykes.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamjua kambona ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tabutupu,
Namfahamu kupitia utafiti wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes.

Hata pale Dodoma alipokuwapo Kambona akisomesha shule ya Alliance, hakupata kujihusisha na juhudi za akina Omari Suleiman na Haruna Taratibu wazalendo ambao walikuwa katika mipango ya kufungua tawi la TANU Central Province.

Job Lusinde alikuwapo hapo vilevile wakati ule lakini ukweli ni kuwa hawa wote walijiweka mbali na juhudi hizi kwa kuogopa kuharibu ajira zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma andiko la Dada hapo juu, nikajua tu Mzee Said atawasili hapa muda si mrefu.

Kwa hili la Kambona, popote ulipolitoa kiukweli Dada umeingia chaka.
 
NAHIC KABISA HATA CHAMA CHA CWT KIMESHABADILISHWA NA KUWA CHAMA CHA WANAWAKE TANZANIA ....

Sent using i phone x
 
Sawa, Mzee Mohamed Said.
May Day,
Mimi si kama najipigia zumari yaani "blowing my own trumpet."

Hii historia naijua vizuri sana kwa kuwa nimeishi ndani yake.

Tabu sana kwa mtu kushindana na mimi katika historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika akanishinda.

Wakati mwingine hufupisha majibu kwa kuchelea kuwachosha wasomaji wangu.

Sipingani na unavyosema Mzee Said, ila kwa yale nisiyokubaliana na wewe kwenye historia ya TAA na baadae TANU yatabaki pale pale...na wala sitarajii kubadilisha msimamo wangu.
 
Back
Top Bottom