Wanaharakati nguli, mnaokoteza matukio mitandaoni au wahitaji wanawafikiaje?

Wanaharakati nguli, mnaokoteza matukio mitandaoni au wahitaji wanawafikiaje?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Nisiwachoshe sana. Twende kwenye hoja

Nimekuwa nafuatilia kwa uchanya sana shughuli za wanaharakati hususan wanasheria wa kujitolea wanaosimamia haki kwa gharama kubwa ya kujitolea.

Nimeangalia kurasa zao zote za mitandaoni hawajaweka mawasiliano yao na wameenda mbali zaidi wamefunga inbox zao wasipokee jumbe zozote. Nimeona jambo hili halipo sawa. Kama unasimama kwenye HAKI, basi ni budi kufahamu kuna wadau watapenda kutoa hoja ama malalamiko yao kwa faragha. Kama hqupatikani online basi weka anuani ili upatikanaji uwe wa uhakika.

Angalia matukio mengi wanaokoteza online huku ikijulikana siyo yote yanawekwa online.

Kuna unyama unatendwa na dola kimya kimya, hivyo ni busara kuweka option ya kupokea malalamiko na mahitaji kwa faragha.
 
Back
Top Bottom