Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake nchini Afrika Kusini kutoka Taasisi ya Women for Change wameanzisha kampeni ya kutaka kusitishwa kwa shoo ya staa wa RnB duniani, Chris Brown maarufu Breezy pnchini humo linalotarajiwa kufanika kwa siku mbili, Desemba 14 na 15, 2024.
Wanaharakati hao wamedai kuwa Breezy ana historia mbaya ya unyanyasaji wa kijinsia kwa tukio lake la kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna na kwamba tarehe ya shoo hizo itaangukia katika Maadhimisho ya Wiki ya Kupinga Ukatili na kwamba hatakiwi kufanya shoo nchini humo kwani itakuwa ni sawa na kuhalalisha ukatili wanaofanyiwa wanawake.
Licha ya tiketi za shoo yake kumalizika ndani ya saa mbili tu tangu zilipoanza kuuzwa Oktoba 3 na kuwalazimu waandaaji kuongeza siku nyingine kutokana na uhitaji, bado kuna kigugumizi katika kupitisha tamasha hilo, ambapo wanaharakati hao wamekusanya saini 20,000 mpaka sasa, huku mawakili wakiitaka Idara ya Mambo ya Ndani kumfutia viza yake.
Soma:
=> Tamasha la Chris Brown Johannesburg: Tiketi zote zimeuzwa, zikiwa na bei kuanzia Tsh. 94,000 hadi 800,000
=> Afrika Kusini ndio nchi yenye Kiwango kikubwa cha Mauaji ya Wanawake barani Afrika na mara 5 ya Wastani wa Dunia