Wanaharakati wa Jamhuri ya Twitter

Watu wenye akili hawawezi kupambana na kichaa, bora kumpisha ila mmsaidie kumweleza kuwa yeye naye ni binadamu nyama ya udongo
 
Unajua watu wa twitter asilimia kubwa ni kama wanazalishwa hivi, yani watu wameweka mradi wao huko twitter wa kutengeneza wafuasi
Yani wapo kimakakati sana kwenye uzalishaji wao yani wamejipanga hawapotei twitter kirahisi ndio kwanz wanaongeza team work

Na wako vizuri kweli kweli unaweza ukajazwa upepo mpaka ukatamani ukampige mkuu.
 
Magufuli akisema hapana ni hapana

Kule Zanzibar ACT walipuuzia wakatest (wakavamia msikiti, wakakata watu mapanga, wakachoma maskani za CCM, wakaandamana na kufanya vurugu) baada ya kila tukio walilokuwa wakifanya, kilichofuata si malizii
 
Watu wenye akili hawawezi kupambana na kichaa, bora kumpisha ila mmsaidie kumweleza kuwa yeye naye ni binadamu nyama ya udongo
Kuna binadamu asiyetambua kwamba yeye ni binadamu?
 
Magufuli akisema hapana ni hapana

Kule Zanzibar ACT walipuuzia wakatest (wakavamia msikiti, wakakata watu mapanga, wakachoma maskani za CCM, wakaandamana na kufanya vurugu) baada ya kila tukio walilokuwa wakifanya, kilichofuata si malizii
Ngosha means business...
 
Halafu utadhani wako wengi kumbe wapi! Hata 20 hawafiki.

Ila hizo kelele zao sasa....
 
Nyani Ngabu,

..angalia hali inavyokuwa kwa wana-ccm wanapokosa msaada wa polisi.

..umeona jinsi jamaa wa chadema anavyotupa makonde?

 
Ni kwamba walio tayari kwa maandamano hawafiki 20.
Sio ishirini tu ni kwamba hakuna aliyekuwa tayari. Hata waitishaji wenyewe. Kilichofanyika ni waitishaji kusubiri tulio tayari tuanzishe. Bahati mbaya kumbe hata sisi hatukuwa tayari.
Si maandamano bila kikomo?
Hata sasa wanawaeza/tunaweza kuanza kuandamana.
 
Kazi ya Mambosasa ni kushika bunduki mkuu. Unataka aje barabarani na maua?

..na wanasiasa na wanaharakati kazi yao siyo kushika bunduki.

..sasa kwanini unataka asiyeshika bunduki apambane na anayeshika bunduki?
 
Mimi natamani sana Shangazi na bff wake Binti Maria siku moja waandamane wakiwa mstari wa mbele kabisa 🀣.

Hiyo siku ikitokea hata mimi ntaandamana kuwaunga mkono.
 
..angalia hapo jamaa wa ccm vs cdm.

..ccm bila polisi hawawezi kukabiliana na cdm.

 
Wanaandamana moyoni πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Huu moyo umepewa kazi kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…