Wanaharakati wa Jamhuri ya Twitter

Wanaharakati wa Jamhuri ya Twitter

Miaka minne ilopita nilitoa maoni kuwa, endapo wale jamaa wa UKUTA wangenywea na kutokufanya maandamano yao waliyokuwa wameyapania, basi huo ungekuwa ni ushindi mkubwa kwa Rais Magufuli. Si tu ushindi uonekanao kwa macho, bali ushindi wa kisaikolojia pia.

Niliandika hapa:

Maandamano hayo hayakufanyika. Rais Magufuli aliwaambia hao walokuwa wamepanga hayo maandamano kuwa yeye ‘hajaribiwi’.

Nadhani walimwelewa alichokisema.

Miaka 2 baadaye kukapangwa tena kuwe na maandamano makubwa ambayo yangefanyika siku ya muungano. Haya hayakuitishwa na chama chochote cha kisiasa. Yaliitishwa na dada’ake na Salary Slip 🤣.

Hakuna aliyethubutu kuingia barabarani.

Mwaka huu tena vyama vya ACT-Wazalendo na CHADEMA baada ya kushindwa uchaguzi mkuu na kudai kuwa vimefanyiwa hujuma, viongozi wake wakaitisha maandamano ya amani nchi nzima, yasiyo na kikomo, ya kupinga matokeo.

Hakuna hata mtu mmoja aliyeingia barabarani na kuthubutu kuandamana.

Huwa naona sana humu wale akina dada wa Twitter, wale wanaharakati wa Jamhuri ya Twitter, Shangazi na yule mwezake Binti Maria wakisifiwa sana wanapo longalonga huko kwenye hiyo jamhuri yao. Halafu kuna huyu raia mpya aitwaye Amsterdam. Naye naona anapenda sana kulong

Kwamba eti ni majasiri sana. Hawamwogopi mtu, blah blah blah.

Sasa, kama kweli hawamwogopi mtu na hawaogopi kitu, kwa nini sasa huwa wanaishia kupiga mayowe kwenye hiyo jamhuri yao? Kwa nini waait etende kwa vitendo hayo maneno yao kwa kuingia barabarani na mabango yao na vipaza sauti kumpinga huyo wasiyempenda?

Jibu ni moja tu: na wao wanajua kuwa huyo Ngosha hajaribiwi. Akisema kitu akiwa amekasirika huwa anamaanisha. Aliposema hajaribiwi, naamini wote walioisikia hiyo kauli, waliielewa.

Kelele zipigwazo jamhuri ya Twitter haziwezi kubadili chochote kilichopo huku uraiani.

Kauli ya Ngosha na virungu vya kamanda Mambosasa, vimewapa watu uhamisho toka Tanzania kwenda Jamhuri ya watu wa Twitter.
Watu wenye akili hawawezi kupambana na kichaa, bora kumpisha ila mmsaidie kumweleza kuwa yeye naye ni binadamu nyama ya udongo
 
Unajua watu wa twitter asilimia kubwa ni kama wanazalishwa hivi, yani watu wameweka mradi wao huko twitter wa kutengeneza wafuasi
Yani wapo kimakakati sana kwenye uzalishaji wao yani wamejipanga hawapotei twitter kirahisi ndio kwanz wanaongeza team work

Na wako vizuri kweli kweli unaweza ukajazwa upepo mpaka ukatamani ukampige mkuu.
 
Magufuli akisema hapana ni hapana

Kule Zanzibar ACT walipuuzia wakatest (wakavamia msikiti, wakakata watu mapanga, wakachoma maskani za CCM, wakaandamana na kufanya vurugu) baada ya kila tukio walilokuwa wakifanya, kilichofuata si malizii
 
Kuna binadamu asiyetambua kwamba yeye ni binadamu?
 
Magufuli akisema hapana ni hapana

Kule Zanzibar ACT walipuuzia wakatest (wakavamia msikiti, wakakata watu mapanga, wakachoma maskani za CCM, wakaandamana na kufanya vurugu) baada ya kila tukio walilokuwa wakifanya, kilichofuata si malizii
Ngosha means business...
 
Unajua watu wa twitter asilimia kubwa ni kama wanazalishwa hivi, yani watu wameweka mradi wao huko twitter wa kutengeneza wafuasi
Yani wapo kimakakati sana kwenye uzalishaji wao yani wamejipanga hawapotei twitter kirahisi ndio kwanz wanaongeza team work

Na wako vizuri kweli kweli unaweza ukajazwa upepo mpaka ukatamani ukampige mkuu.
Halafu utadhani wako wengi kumbe wapi! Hata 20 hawafiki.

Ila hizo kelele zao sasa....
 
Nyani Ngabu,

..angalia hali inavyokuwa kwa wana-ccm wanapokosa msaada wa polisi.

..umeona jinsi jamaa wa chadema anavyotupa makonde?

Ni kwamba walio tayari kwa maandamano hawafiki 20.
Sio ishirini tu ni kwamba hakuna aliyekuwa tayari. Hata waitishaji wenyewe. Kilichofanyika ni waitishaji kusubiri tulio tayari tuanzishe. Bahati mbaya kumbe hata sisi hatukuwa tayari.
Si maandamano bila kikomo?
Hata sasa wanawaeza/tunaweza kuanza kuandamana.
 
Kazi ya Mambosasa ni kushika bunduki mkuu. Unataka aje barabarani na maua?

..na wanasiasa na wanaharakati kazi yao siyo kushika bunduki.

..sasa kwanini unataka asiyeshika bunduki apambane na anayeshika bunduki?
 
Sio ishirini tu ni kwamba hakuna aliyekuwa tayari. Hata waitishaji wenyewe. Kilichofanyika ni waitishaji kusubiri tulio tayari tuanzishe. Bahati mbaya kumbe hata sisi hatukuwa tayari.
Si maandamano bila kikomo?
Hata sasa wanawaeza/tunaweza kuanza kuandamana.
Mimi natamani sana Shangazi na bff wake Binti Maria siku moja waandamane wakiwa mstari wa mbele kabisa 🤣.

Hiyo siku ikitokea hata mimi ntaandamana kuwaunga mkono.
 
..angalia hapo jamaa wa ccm vs cdm.

..ccm bila polisi hawawezi kukabiliana na cdm.

Wanaandamana moyoni 😂😂😂
Huu moyo umepewa kazi kubwa sana
 
Back
Top Bottom