Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Harakati Harakatini
Msingi mkubwa wa haki za binadamu ni mapokeo ya Universal Declaration of Human Rights ya mwaka 1948 ambapo humo kuna vipengele 30 vya hizi haki za binadamu. Ni document ya page 8; yeyote anaweza kuisoma na kujionea kilichomo.
Ukipitia hiyo document ya haki za binadamu ambayo inaenda kutimiza miaka 80; kwa haraka haraka nimeona kwamba Tanzania ya sasa bado haiheshimu haki nyingi sana za binadamu na saa nyingine hata serikali yenyewe imejihusisha wazi wazi kwenye vitendo vya kuzivunja hizo haki za binadamu (rejea uchaguzi uchafuzi wa 2019, 2020 na 2024).
Ukitazama hivo vifungu vya haki za binadamu, nyingi ama zote zina umuhimu mkubwa sana, hata hawa watu wanaozivunja hizi haki za binadamu, endapo mzani ukabadilika na ikawa wao ndo wanavunjiwa, hakika wataona ni kiama ama dunia inawaonea. Unawezaje kustahimili kilichomkuta mzee Ali Kibao au wanachokipitia akiana Deus Soka, hata watekaji wenyewe hawawezi kupitia hizo shuruba.
Hivo basi, kuna maana kubwa ya kuwepo kwa harakati za kupigania haki za binadamu, ni kitu chema. Lakini kwa hapa Tanzania, harakati za kupigania haki za binadamu ni kama sasa zimehodhiwa na makundi ya watu ambao kwa maneno yao na matamshi yao, wanaonekana ni watu waliopungukiwa 'logical thinking'.
Logical thinking kwa tafsiri rahisi kabisa ni ule uwezo wa kuhitimisha jambo ukiwa umeshaainisha masuala kadhaa ya kulithibitisha jambo hilo (concluding something based on well grounded premises). Mfano mdogo, kuna tofauti kubwa ya hawa watu wawili
Mtu A
Hili ni tunda la embe
Embe hili lina wadudu
Embe hili halifai kuliwa
Mtu B
Hili ni tunda la embe
Embe hili halifai kuliwa
Tofauti kati ya mtu A na mtu B ni kwamba, mtu A ameenda kwenye hitimisho la 'Embe hili halifai kuliwa' ikiwa tayari ameweka na sababu ya kwanini embe hili halifai kuliwa (Huyu ni logical thinker kwasababu hitimisho lake haliachi maswali yasiyo na majibu). Mtu B yeye amerukia kwenye hitimishi bila kuweka sababu ya ni kwanini 'embe hili halifai kuliwa' (Huyu sio 'logical thinker' kwasababu maneno yake yanakaribisha maswali badala ya kuja na majibu)
Mfano mchache, nimemsoma mwandishi Erick Kabendera kwenye pages chache zile zenye serious allegations kuhusu Magufuli, nikajaribu kuzipima kwenye mizania ya logical thinking process, nikagundua kwamba nyingi zina lack complete premises. Halafu pia kuna masuala mengine kwenye kitabu yanaonekana kama breach of privacy, ambayo ni haki muhimu ya binadamu. (hapo linaibuka swali, as much as tunazipenda kweli haki za binadamu, ila tunakwepaje mtego wa kuzivunja haki hizo hizo za binadamu kwa gia ya kuzipigania haki za binadamu?)
Mfano mngine, kwa mwanadada huyu Tsehai alopata kashikashi ya kutekwa, yap anajaribu kuwa mstari wa mbele kuzipigania hizi haki lakini naye kuna vitu anaongea ambavyo wakati mwingine ni just rhetoric, havina complete premises, ni kama amekuwa mtu wa kuanguka na kukimbilia kwenye conclusion muda wote.
Madhara ya kukosekana 'logical thinking' kwa wanaharakati ni kwamba endapo watatokea 'logical thinkers' kwa upande wa oppressors, kuna hatari ya harakati za wanaharakati kupoteza ushawishi kwasababu mwisho wa siku, ili hizi haki zisimame imara wanaharakati watatakiwa kuzigonganisha hoja zao na zile za upande wa pili (oppressors), ila ikiwa wanaharakati wametawaliwa na poor reasoning, kuna hatari ya wao kushindwa hii vita na wengi wao hata wakaishia magerezani. Mfano mdogo tu, as much as hata mimi siupendi utawala wa Samia kwenye kusimamia haki za binadamu, mwanaharakati anayetoa statement ya 'Rais fulani ni muuaji na mla rushwa' unadhani mtu huyu akienda kwenye chujio la sheria anatokaje salama bila kufungwa? obvious hawezi kuja na proof kuhusu hiyo statement, sasa who is the loser?
Maana yake ni kwamba, wanaharakati wajitahidi kuwekeza kwenye utafiti na kupangilia hoja zao, hii itawafanya kutoonekana watu wa hovyo na kukurupuka, na itawapa pia uhalali na ushindi pindi mnapoingia kwenye dialogue dhidi ya oppressors; mimi naamini endapo kama 'logical thinking' iki prevail kwa wanaharakati wetu, in the long run matunda ya harakati tutayaona Tanzania, ila kama tukiendelea na aina hii ya harakati zilizo na basis ya poor logical thinking, naona itatuchukua muda sana kwa harakati kuzaa matunda.