Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
WANAHARAKA WAJIGAWE WANAPOMLENGA ADUI HIYO NI MEDANI YA VITA. WALIHAMASISHA WATU KUSUSIA SHOW YA WANAMUZIKI. KIKO WAPI!
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Ni kweli kwa sasa wamefanikiwa kupata ushawishi mitandaoni kwa mbinu mbalimbali. Hilo kwao ni jambo kubwa.
Changamoto ninayoiona kwao ni wanatumia mbinu moja na ileile kumkabili adui yao. Jambo ambalo linawafelisha.
Wanajikuta wakucheza ngoma ya Adui yao. Na kuwa watu wakufuata matukio na trends zinazoratibiwa na adui yao. Hiyo kwa sisi Watibeli tunalihesabu kama kosa la kiufundi.
Kwenye masuala ya Kivita na kijasusi. Katika meza ya kupanga vita na mashambulizi. Viongozi wa vikosi na mastermind wa mchezo hugawa jeshi(wapiganaji) katika vikosi kadha wa kadha na kila kikosi hukipa jina na majukumu yake. Lengo ni adui mmoja lakini mwenye matawi na mbinu nyingi.
Mbinu hii niliwahi kuieleza. Inaitwa utawiwishaji au matrix.
Hapo utakuja kikosi kinaitwa BRAVO, ALPHA, OMEGA, SAVANAH, REDBULL n.k.
Kila kikosi kinaendesha operation yake kulingana na mission, mbinu na adui yukoje.
Wanaharakati hapa nchini mbinu hii hawaitumii na hawajawahi kuitumia. Nafikiri ni kwa sababu ya kukosa good organization, kutokuaminiana kutokana na yeyote anaweza kuwa yeyote. Kuogopa kuwekewa mashushushu kutoka serikalini.
Athari ya kukosa vikosi vya kuendesha mashambulizi utaziona kwenye kudandia agenda, Leo Free Tundu Lisu, kesho wanamsahau, watakuja Maandamano, yatapita, itakuja Susia wanamuziki, yaani wanarukia rukia matawi kama Ngedere. Hii inawafanya wapoteza focus.
Adui yao anatumia mbinu nyingi na majukwaa kadha wa kadha. Hivyo wanaharakati ingewapasa nao waunde vikosi vitakavyojikita na kujihusisha na majukwaa na mbinu za adui. Mfano vikosi kama ifuatavyo;
a) Wanaharakati wa kisiasa, wajiite Bendera nyekundu kama Code name.
Hawa kazi zao ziwe kukabiliana na siasa na wawe na ujuzi wa mambo ya kisiasa, kisheria, Kiser na kidiplomasia.
Hawa ndio watahusika na mambo ya kudai katiba, maandamano, kesi huko mahakamani na matukio ya kisiasa. Sijui Free Tundu Lisu, na mambo kama hayo.
b) Wanaharakati wa kidini, Msalaba mwekundu. Iwe code name.
Adui zao hutumia dini na propaganda za kidini kuwapumbaza na kuwasahaulisha watu.
Wanaharakati lazima wawe na watu kwaajili ya kushughulikia mambo ya kidini.
Wazijue Dini vilivyo, wawe wataalamu wa Dini. Sijui uislam, ukristo, sijui nini. Huko kote.
Masuala ya kijadi kama sijui machifu, sijui waganga.
Wakina Mwaipopo hapa wangeshughulikiwa na kundi hili.
c) Wanaharakati wa burudani na michezo, DARK ARENA liwe code name.
Hawa ndio watashughulika na mambo ya muziki, filamu na michezo kama mipira huko.
d) Wanaharakati wa kijamii na wa mambo yote. OMEGa liwe Code name.
Hawa ndio watakuwa kazi yao wanashambulia popote wanapoona. Yaani wao yakitokea yakijamii wapo. Yakisiasa wapo, yakimichezo na burudani yapo. Yaani Hawa ndio wanaofuata trends na matukio.
Hii ni kumaanisha wanaharakati watakuwa wanampa wakati mgumu adui yao kwani watakuwa na ile consistency kwenye kushambulia. Kumaanisha mpaka hivi leo bado watu wangekuwa hawajamsahau Mdude, Polepole, Ben saanane na wengine kwani wapo wanaharakati watakaoshikilia bango na Bomba mwanzo mwisho bila kurukia tawi jingine mambo ya dini au wasanii.
Ndio maana kwenye vita na mpira wa miguu namba saba uwanjani ambaye ni Winga licha ta kuingia ndani namba kumi au tisa lakini bado atarudi kwenye namba yake saba kutekeleza majukumu yake.
Serikali inambinu nyingi za kusahaulisha watu hasa ukizingatia watu wengi ni wakawaida, elimu ndogo, exposure hawana, maskini wanaowaza mlo wa siku. Hivyo ni rahisi kucheza nao.
Unawaambia watu wasuse show za wasanii, round ya kwanza watasusa, vipi ya Tatu na yanne, ikiwa hakuna wakuwekea mkazo na kuwakumbusha mara kwa mara?
Unapopambana na serikali hasa kwenye michezo ya kisiasa na propaganda ni ngumu sana kuishinda kama hutakuwa na good plan, strategic, na organization.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam