Wanaharakati wakubwa wa haki walikuwa mitume, neno wanaharakati lisitumike vibaya

Wanaharakati wakubwa wa haki walikuwa mitume, neno wanaharakati lisitumike vibaya

Sumbaye

Member
Joined
Apr 26, 2025
Posts
59
Reaction score
77
Nimeona maoni watu wengi juu ya neno mwanaharakati na matumizi yake. Neno mwanaharakati linatumika kujenga taaswira mbaya juu ya jitihada wapigania haki za watu.

Mwanaharakati ni mtu anaetetea aina flani ya mtizamo na kupinga kila kilicho kinyume chake. Kwa Maana hiyo mtu yeyote mwenye conviction ya mtizamo fulani, anauishi na kuutetea huyo ni mwanaharakati.

Mwanaharakati maarufu kuliko wote duniani ni mtume Muhammad. Yeye alitetea na kueneza mafundisho ya dini ya kiislam na alipinga kila ambacho kilikuwa kinyume na mafundisho ya dini ya kiislamu.

Mwanaharakati wa pili kwa umaarufu ni Yesu kristo. Huyu alitetea na kueneza mafundisho ya ukristo na kupinga kila ambacho kilikuwa kinyume na ukristo.

Kwa hiyo viongozi wa dini wote ni wanaharakati wa kueneza na kutetea dini zao. Hawa ni wanaharakati ambao wanafanya harakati ila wanajifanya kwamba wao sio wanaharakati. Kwa hiyo viongozi wa dini wanaolaani wanaharakati watambue kwamba na wao ni wanaharakati ila wanatofautiana na makundi mengi wao ni wanaharakati wa dini, wengine ni wanaharakati wa haki za binadamu, wengine ni wanaharakati wa haki za kiraia, wanaharakati wa mazingira nk.

Kwa kuwa wanatetea watawala tunaweza Kuwaita wanaharakati wa kutetea watawala waovu , na wengine ni wanaharakati wa kutetea haki za watu.
 
Kutugawa kidini ishabuma hiyooo!

IMG-20251123-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom