Wanahitaji kutumia NIDA yangu kumsajilia mtu mkopo wa simu.

ni ofisi inayohusika na ukopeshaji wa simu za smartphone..wameniomba wanipe posho kidogo wamsajilie mtu simu ya mkopo vipi mnaojua huwa kuna risk au side effect yoyote kwa namba yangu kutumika?
Endelea kukaza fuvu mzee
Ww si mtiifu bwana deo
 
ni ofisi inayohusika na ukopeshaji wa simu za smartphone..wameniomba wanipe posho kidogo wamsajilie mtu simu ya mkopo vipi mnaojua huwa kuna risk au side effect yoyote kwa namba yangu kutumika?
Iweni na hakiri kama nyoka! mkuu kitakulamba very soon
 
Kwa sasa unaweza kufurahia kupata hiyo posho lakini baadaye inaweza kukuletea changamoto kubwa sana.
Mfano mdogo ni uliotokea kwangu, Mdogo wangu alitumia NIDA yangu kuchukua simu ya mkopo na kusajili laini kwa jina langu. Baadaye alitumia laini hiyo kukopa TSh 400,000 kutoka Vodacom, lakini hakurejesha mkopo huo, na akaitelekeza laini.
Akaja kuchukua Simu ya mkopo, simu aliyochukua ilikuwa Samsung A56 yenye thamani ya takribani TSh milioni 1, lakini kutokana na riba, deni lilifika karibu TSh milioni 2.
Cha kusikitisha zaidi, hata mwezi haukupita simu hiyo ikaibiwa. Kwa kuwa ilikuwa ya mkopo, hakujali sana na akaipotezea.
Tatizo kubwa lilinikumba mimi. Nilipoenda benki kuomba mkopo wa takribani TSh milioni 60 kwa ajili ya kuendeleza biashara yangu, nilikataliwa. Benki walinieleza kuwa kwenye taarifa zangu nilionekana kuwa mdaiwa sugu kutokana na madeni ya Vodacom na kampuni ya simu yaliyokuwa yamesajiliwa kwa jina langu.
Sikukuwa na namna nyingine zaidi ya kulipa madeni yote kwanza ndipo nilipoweza kuendelea na mchakato wa kuomba mkopo.
Ushauri wangu: Usikubali kutumia kitambulisho chako cha NIDA kwa mtu mwingine, hata kama ni ndugu wa karibu. Madhara yake yanaweza kukugharimu sana baadaye.
 
Asipolipa deni litakuwa lako.
Utawekwa kwenye orodha ya wadaiwa sugu kule kweye mfumo wa serikali.
Ikilazimu kushitakiwa utashitakiwa wewe mahakamani.
 
Mbona ha

Kivip maana naskia namba za simu hutumika zake
Namba yako ya nida ni utambulisho wako. Wakopeshaji hawa deal na namba ya simu ya mkopaji, wanadeal na namba ya nida iliyotumika kuombea mkopo.

Unaenda kuchafua jina lako, n ahutokopesheka tena, na polisi watapewa taarifa zako kwamba wewe ni tapeli, hata wasipokufuatilia, jua tu kwamba itaenda kuharibu profile yako
 
Kwa sasa unaweza kufurahia kupata hiyo posho lakini baadaye inaweza kukuletea changamoto kubwa sana.
Mfano mdogo ni uliotokea kwangu, Mdogo wangu alitumia NIDA yangu kuchukua simu ya mkopo na kusajili laini kwa jina langu. Baadaye alitumia laini hiyo kukopa TSh 400,000 kutoka Vodacom, lakini hakurejesha mkopo huo, na akaitelekeza laini.
Akaja kuchukua Simu ya mkopo, simu aliyochukua ilikuwa Samsung A56 yenye thamani ya takribani TSh milioni 1, lakini kutokana na riba, deni lilifika karibu TSh milioni 2.
Cha kusikitisha zaidi, hata mwezi haukupita simu hiyo ikaibiwa. Kwa kuwa ilikuwa ya mkopo, hakujali sana na akaipotezea.
Tatizo kubwa lilinikumba mimi. Nilipoenda benki kuomba mkopo wa takribani TSh milioni 60 kwa ajili ya kuendeleza biashara yangu, nilikataliwa. Benki walinieleza kuwa kwenye taarifa zangu nilionekana kuwa mdaiwa sugu kutokana na madeni ya Vodacom na kampuni ya simu yaliyokuwa yamesajiliwa kwa jina langu.
Sikukuwa na namna nyingine zaidi ya kulipa madeni yote kwanza ndipo nilipoweza kuendelea na mchakato wa kuomba mkopo.
Ushauri wangu: Usikubali kutumia kitambulisho chako cha NIDA kwa mtu mwingine, hata kama ni ndugu wa karibu. Madhara yake yanaweza kukugharimu sana baadaye.
Sijakubali japo wameniomba saaaaana hata mi nimehisi kama itakua ni kuongeza mzigo wa mikopo
 
Sikiliza, hata mkeo akitaka NIDA yako kusajili vitu mtandaoni kataa, achilia mbali mtu baki, hata mkeo tu. That's how serious it gets, acha upumbavu.
 
Back
Top Bottom