Wanajeshi 3000 hadi 4000 wa Rwanda wanashirikiana na waasi wa M23 katika mapigano mashariki mwa Kongo

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,042
Reaction score
3,674
UN: Vikosi vya Rwanda vyasaidiana na M23 kupigana Kongo

Ripoti moja ya wataalam wa Umoja wa Mataifa iliyoonekana na shirika la habari la Ufaransa AFP inasema, kati ya wanajeshi 3000 hadi 4000 wa Rwanda wanashirikiana na waasi wa M23 katika mapigano mashariki mwa Kongo.

Ripoti hiyo inasema Kigali, ndiyo inayodhibiti operesheni za waasi hao wa M23.

Watafiti wa ripoti hiyo walikadiria wakati wa kuandikwa kwake mnamo mwezi Aprili kwamba, idadi ya vikosi vya Rwanda inalingana au imeivuka idadi ya waasi wa M23 ambayo ilikuwa inadaiwa kuwa karibu 3,000.

Ripoti hiyo inajumuisha picha zilizohakikiwa, mikanda ya video, picha zilizopigwa na droni, ushuhuda na ripoti za majasusi mambo yanayothibitisha uingiaji wa jeshi la Rwanda RDF huko mashariki mwa Kongo.

Watoto kusajiliwa jeshini

Mikanda hiyo ya video na picha zinaonesha milolongo ya wanajeshiwaliojihami wakitumia silaha na magari ya kijeshi yaliyo na mifumo ya kuzuia mashambulizi ya makombora ya ndege. Picha hizo pia zinaonesha malori yanayotumiwa kuwasafirisha wanajeshi.

Vile vile ripoti hiyo inaeleza kwamba watoto kuanzia umri wa miaka 12 wamesajiliwa kutoka walau kila kambi ya wakimbizi ndani ya Rwanda na wanapelekwa katika kambi za mazoezi katika maeneo ya waasi chini ya usimamizi wa wanajeshi wa Rwanda na wanamgambo wa M23.

Inaongeza kwamba watoto walio na umri wa miaka 15 na zaidi wanapewa mafunzo ya kijeshi na kupelekwa vitani ili kuwa katika mstari wa mbele kushiriki mapigano hayo.

Wataalam hao wa Umoja wa Mataifa wanadai kwamba kusajiliwa kwa watoto jeshini nchini Rwanda, ni jambo linalofanywa na maafisa wa ujasusi wakitoa ahadi za uongo za mishahara na malipo kwa watoto hao. Inaripotiwa kwamba wale wanaopinga, wanachukuliwa na kusajiliwa jeshini kwa nguvu.

Rwanda iliwasaidia waasi kunyakua maeneo mengi zaidi

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekuwa ikiituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ila Kigali imekuwa mara zote ikikanusha vikali tuhuma hizo.

Lakini ripoti hiyo iliyoitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, inasema hatua ya jeshi la Rwanda kuzidhibiti harakati za waasi wa M23 ni jambo linaloifanya nchi hiyo kulaumiwa kwa vitendo vya waasi hao.

Kulingana na wataalam hao wa Umoja wa Mataifa, uingiliaji wa jeshi la Rwanda na operesheni zake za kijeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini katika maeneo ya Nyiragongo, Rutshuru na Masisi, ulikuwa muhimu kwa waasi hao kutanua maeneo zaidi inayoyadhibiti kati ya Januari na Machi mwaka huu.

Mkoa wa Kivu Kaskazini umekuwa chini ya udhibiti wa waasi wa M23 tangu mwishoni mwa mwaka 2021, huku kundi hilo likinyakua maeneo makubwa na kuanzisha utawala wa kivyake katika maeneo ambayo sasa yako chini ya udhibiti wake.

Chanzo: AFP
 
Attachments

  • Screenshot_20240708_152122_Chrome.jpg
    Screenshot_20240708_152122_Chrome.jpg
    272.5 KB · Views: 14
UN wanafiki sana. Wakati Kagame na Kabalebe wanamtoa Mobutu walikuwa wapi?. Yani Rwanda ni Wazuri wakati wa kumtoa Dikteta ila wakati wa Kulinda kundi la Wanyamulenge lililotengwa nchini Kongo ni shida.
 
Solution moja tu

Kongo ikubali kuwa watusi walioko Kongo ni raia wake

Sijui kwa nini kongo inakuwa nzito

Watusi wako kongo miaka na miaka kabla hata kongo haijapata uhuru iwakubali.kama raia halali wa kongo isiwanyanyase

Tanzania mbona tuliwakubali makabila kibao ya yaliyoko nchi zingine na hatuna tuliwakubali wanyasa ambao ni wengi Malawi,tuliwakubali wamasai na wajaluo ambao ni wengi Kenya,tukawakubali wamakonde na wamakua ambao ni wengi msumbiji ,Tuna wabembe ambao wengi ni wako Congo nk na nchi iko tulivu haina shida

Kongo wawakubali watusi wa Kongo kama raia halali wa kongo kutaka ohh waondoke warudi Rwanda si sahihi

Mkoloni alichora ramani vibaya makabila yanakatika kabila moja kipande kinajikuta kiko nchi ingine na kingine nchi ingine

Kila nchi ikubali tu kupokea kipande kilichokatikiwa kwao mipaka ikichorwa na wakoloni kwenye mkutano wa Berlin
 
Anapigania maslahi yake. Aache chokochoko kwenye nchi za watu. Huwezi kupeleka jeshi zima kupigana kwenye nchi nyingine, alafu uje na utetezi wa namna hiyo.
 
DRC anachojua ni kulalamika kama demu badala ya kupambana
 
Solution moja tu

Kongo ikubali kuwa watusi walioko Kongo ni raia wake

Sijui kwa nini kongo inakuwa nzito

Watusi wako kongo miaka na miaka kabla hata kongo haijapata uhuru iwakubali.kama raia halali wa kongo isiwanyanyase

Tanzania mbona tuliwakubali makabila kibao ya yaliyoko nchi zingine na hatuna tuliwakubali wanyasa ambao ni wengi Malawi,tuliwakubali wamasai na wajaluo ambao ni wengi Kenya,tukawakubali wamakonde na wamakua ambao ni wengi msumbiji ,Tuna wabembe ambao wengi ni wako Congo nk na nchi iko tulivu haina shida

Kongo wawakubali watusi wa Kongo kama raia halali wa kongo kutaka ohh waondoke warudi Rwanda si sahihi

Mkoloni alichora ramani vibaya makabila yanakatika kabila moja kipande kinajikuta kiko nchi ingine na kingine nchi ingine

Kila nchi ikubali tu kupokea kipande kilichokatikiwa kwao mipaka ikichorwa na wakoloni kwenye mkutano wa Berlin
Tatizo la Wanyarwanda ni tabia zao chafu za kutaka kutawala wengine. Ili Congo itulie lazima imalize huu uasi kwa njia ambayo hautajirudia.
 
UN wanafiki sana. Wakati Kagame na Kabalebe wanamtoa Mobutu walikuwa wapi?. Yani Rwanda ni Wazuri wakati wa kumtoa Dikteta ila wakati wa Kulinda kundi la Wanyamulenge lililotengwa nchini Kongo ni shida.
Kama wanawapenda wanyamulenge kwanini wasiwahamishie Rwanda??
 
UN: Vikosi vya Rwanda vyasaidiana na M23 kupigana Kongo

Ripoti moja ya wataalam wa Umoja wa Mataifa iliyoonekana na shirika la habari la Ufaransa AFP inasema, kati ya wanajeshi 3000 hadi 4000 wa Rwanda wanashirikiana na waasi wa M23 katika mapigano mashariki mwa Kongo.

Ripoti hiyo inasema Kigali, ndiyo inayodhibiti operesheni za waasi hao wa M23.

Watafiti wa ripoti hiyo walikadiria wakati wa kuandikwa kwake mnamo mwezi Aprili kwamba, idadi ya vikosi vya Rwanda inalingana au imeivuka idadi ya waasi wa M23 ambayo ilikuwa inadaiwa kuwa karibu 3,000.

Ripoti hiyo inajumuisha picha zilizohakikiwa, mikanda ya video, picha zilizopigwa na droni, ushuhuda na ripoti za majasusi mambo yanayothibitisha uingiaji wa jeshi la Rwanda RDF huko mashariki mwa Kongo.

Watoto kusajiliwa jeshini

Mikanda hiyo ya video na picha zinaonesha milolongo ya wanajeshiwaliojihami wakitumia silaha na magari ya kijeshi yaliyo na mifumo ya kuzuia mashambulizi ya makombora ya ndege. Picha hizo pia zinaonesha malori yanayotumiwa kuwasafirisha wanajeshi.

Vile vile ripoti hiyo inaeleza kwamba watoto kuanzia umri wa miaka 12 wamesajiliwa kutoka walau kila kambi ya wakimbizi ndani ya Rwanda na wanapelekwa katika kambi za mazoezi katika maeneo ya waasi chini ya usimamizi wa wanajeshi wa Rwanda na wanamgambo wa M23.

Inaongeza kwamba watoto walio na umri wa miaka 15 na zaidi wanapewa mafunzo ya kijeshi na kupelekwa vitani ili kuwa katika mstari wa mbele kushiriki mapigano hayo.

Wataalam hao wa Umoja wa Mataifa wanadai kwamba kusajiliwa kwa watoto jeshini nchini Rwanda, ni jambo linalofanywa na maafisa wa ujasusi wakitoa ahadi za uongo za mishahara na malipo kwa watoto hao. Inaripotiwa kwamba wale wanaopinga, wanachukuliwa na kusajiliwa jeshini kwa nguvu.

Rwanda iliwasaidia waasi kunyakua maeneo mengi zaidi

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekuwa ikiituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ila Kigali imekuwa mara zote ikikanusha vikali tuhuma hizo.

Lakini ripoti hiyo iliyoitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, inasema hatua ya jeshi la Rwanda kuzidhibiti harakati za waasi wa M23 ni jambo linaloifanya nchi hiyo kulaumiwa kwa vitendo vya waasi hao.

Kulingana na wataalam hao wa Umoja wa Mataifa, uingiliaji wa jeshi la Rwanda na operesheni zake za kijeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini katika maeneo ya Nyiragongo, Rutshuru na Masisi, ulikuwa muhimu kwa waasi hao kutanua maeneo zaidi inayoyadhibiti kati ya Januari na Machi mwaka huu.

Mkoa wa Kivu Kaskazini umekuwa chini ya udhibiti wa waasi wa M23 tangu mwishoni mwa mwaka 2021, huku kundi hilo likinyakua maeneo makubwa na kuanzisha utawala wa kivyake katika maeneo ambayo sasa yako chini ya udhibiti wake.

Chanzo: AFP
Mungu jaajilia amani
 
Miafrika akili haina kazi kuwana tu, hio Congo haiwezi kutulia sio sababu ya Kagame, ni sababu ya USA na Western hao hawawezi kukubali mwafrika aishi kwa amani na starehe kwenye mali zao.

Lazima watafute mjinga wamtumie kwa faida zao, exactly kama wanavyo fanya nchi za kiarabu.

We leo unakuta jitu linashangilia genocide zinazo fanywa na Israel, eti taifa teule, yani taifa lenu ni la watumwa au 😆

Wafrika ni makondoo sana, kupata watu wenye akili wakafocus na maisha ya nchi zao, na kuhudumia wananchi zao ni vigumu sana.
 
Akitokea ccm akajibu kuhusu mkoa wa kagera karagwe kuhusu kambi za M23 zipo pale na ofisi zao zinapokea kila kifaa na njia mnayo danganywa kuhusu katoro. Mengine ni nyamaze
 
Tatizo kwenye Nini?. Kulinda watu wenye asili ya kitusi nchini Kongo?. Halafu Kagame angejua angeyaachaga makongoman yapambane na Mobutu yenyewe. Akayasaidia kupitia James Kabarebe kumtoa Mobutu leo hayana shukrani.
Hakusaidia,yalikua makubaliano maalum kwamba atamegewa eneo mashariki ya congo ambako ni ardhi nzuri ya kilimo,kabila alipoingia ikulu kwa ushawishi wa tz akavunja mkataba
 
Back
Top Bottom