Wanajeshi na Askari mnatumia nini kuzuia ndevu na vipele?

Asante sana mkuu
 
Binafsi nawashangaa sana watu wanaonyoa ndevu.....Mimi hujisikia fahari nikiwa na ndevu.....nazitunza vizuri na zinawaka.....zinanipa ujasiri na kujiona mwanaume niliyekamilika.........

Nikinyoa ndevu najiona kama mvulana mdogo.......najiona kama nimedondokwa na tauro.........

Kweli haya maisha tunatofautiana.......
 
Dawa ya ndevu kila baada ya siku tatu au nne nyoa ukizoea ni very addictive maana ikizidi siku ya tano au sita ni kuwashwa na mapele juu! Hivyo vipele havina dawa utamaliza pesa bure jaribu hiyo 4mula thank me later
 
Hata hivyo, ndani ya week lazima ndevu ziote na kuchoma na kutoa vipele.
  • Kutoka kwa vipele ni dalili mojawapo ya maambukizi ya vimelea kwenye ngozi. Chakufanya onana daktari akushauri ni dawa gani ya kutumia.
  • Wakati ukitumia dawa husika | Ziachendevu kwa angalau wiki 2 bila kunyoa.
  • Nunua na uwe na mashine yako binafsi ya kunyolea, iwe unajinyoa mwenyewe au unaenda saloon, hakikisha unakuwa na mashine yako ndio itumike.
  • Iwapo umeenda saloon epuka na kataa matumizi ya vile vitaulo vyao sio salama.
  • Baada ya kunyoa waweza safisha kidevu kwa sabuni ya deto na usipake kitu chochote.
 
Hebu tuwekee kwanza picha yako ukiwa na ndevu, na ile ambayo huna ndevu! Pamoja na picha za hao wanajeshi/askari ambao ni nadhifu wakiwa wamenyoa hizo ndevu, ili tulinganishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…