Wanajeshi na Askari mnatumia nini kuzuia ndevu na vipele?

Wanajeshi na Askari mnatumia nini kuzuia ndevu na vipele?

Piga mvuke uso wako tumia wembe mpya kunyoa.
Jua uelekeo wa ndevu zako.
Usitumie nguvu kabisaa wakati wa kunyoa fanya km unafuta.
Paka sabuni yoyote acha ikauke
Osha kwa maji vuguvugu.
Interval ya kunyoa izingatiwe ili kuondoa kulazimisha.
•Inategemea na asili ya ngozi yk.
Asante sana mkuu
 
Binafsi nawashangaa sana watu wanaonyoa ndevu.....Mimi hujisikia fahari nikiwa na ndevu.....nazitunza vizuri na zinawaka.....zinanipa ujasiri na kujiona mwanaume niliyekamilika.........

Nikinyoa ndevu najiona kama mvulana mdogo.......najiona kama nimedondokwa na tauro.........

Kweli haya maisha tunatofautiana.......
 
Dawa ya ndevu kila baada ya siku tatu au nne nyoa ukizoea ni very addictive maana ikizidi siku ya tano au sita ni kuwashwa na mapele juu! Hivyo vipele havina dawa utamaliza pesa bure jaribu hiyo 4mula thank me later
 
Hata hivyo, ndani ya week lazima ndevu ziote na kuchoma na kutoa vipele.
  • Kutoka kwa vipele ni dalili mojawapo ya maambukizi ya vimelea kwenye ngozi. Chakufanya onana daktari akushauri ni dawa gani ya kutumia.
  • Wakati ukitumia dawa husika | Ziachendevu kwa angalau wiki 2 bila kunyoa.
  • Nunua na uwe na mashine yako binafsi ya kunyolea, iwe unajinyoa mwenyewe au unaenda saloon, hakikisha unakuwa na mashine yako ndio itumike.
  • Iwapo umeenda saloon epuka na kataa matumizi ya vile vitaulo vyao sio salama.
  • Baada ya kunyoa waweza safisha kidevu kwa sabuni ya deto na usipake kitu chochote.
 
Direct kwenye hoja

Mimi ni miongoni mwa wasiopenda ndevu kabisaa. Nikitoa ndevu naonekana nazifu sana na najisikia kujiamini kuliko nikiacha ndevu ziote.

Utaratibu wangu ni kunyoa mara Moja Kwa week na inanigalimu sana na inanipotezea muda. Hata hivyo, ndani ya week lazima ndevu ziote na kuchoma na kutoa vipele.

Mwanzo nilikua natumia nyembe nikaona sipati matokeo nayoyataka nikawa natumia mashine but no any improvement.


But wanajeshi na askali Kwa matakwa ya taaluma Yao huwa hawafugi ndevu na always wako smart. Ebu wakuu tusaidieni hints za namna ya kunyoa ndevu na kuhepuka kutokea vipele.

Karibuni
Hebu tuwekee kwanza picha yako ukiwa na ndevu, na ile ambayo huna ndevu! Pamoja na picha za hao wanajeshi/askari ambao ni nadhifu wakiwa wamenyoa hizo ndevu, ili tulinganishe.
 
Back
Top Bottom