Anae kwambia mapinduzi yame feli anakudanganya, wamewai kufanya propaganda tu serikali ya benin
"Mimi ni Kanali Pascal Tigri, rais wa Kamati ya Kijeshi ya Kuunda Upya (Military Committee for Refoundation).
Nawahutubia leo kuwaomba wananchi wote wa Benin waamke na kuunga mkono operesheni hii ya kizalendo inayolenga kuikomboa nchi yetu kutoka kwa utawala wa kidikteta wa Patrice Talon.
Saa ya ukweli imewadia. Wananchi lazima waingie barabarani, wajiunge na safu zetu, na kwa pamoja tutaijenga upya Benin yenye haki, heshima, na uhuru kamili.
Tunauonya serikali ya Ufaransa na washirika wake uingiliaji wowote au uungaji mkono kwa utawala ulioondolewa utachukuliwa kama kitendo cha uchokozi dhidi ya mapenzi makuu ya wananchi wa Benin. Ufaransa lazima ikae mbali na mambo yetu ya ndani—enzi yenu ya ukoloni mamboleo barani Afrika imekwisha.
Waishi Wananchi wa Benin! Iishi Benin huru na iliyoundwa upya!
Baada ya taarifa iyo ikafatia na ya kutaka shuguli zisimamae kwa wananchi bado wanaendelea na mapambano,
Taarifa rasmi kutoka kwa jeshi lililochini ya Lt colonel Pascal Tigri ambalo linaongoza zoezi la mapinduzi nchini Benin
TAARIFA RASMI N°001/CMR
Kamati ya Kijeshi ya Ujenzi Upya
Cotonou, 7 Desemba 2025
Kamati ya Kijeshi ya Ujenzi Upya inatangaza hatua maalum zifuatazo, zitakazoanza kutumika kuanzia tarehe 8 Desemba 2025 saa sita usiku (00h00) kwa muda wa siku saba (7):
1. Kusimamishwa kwa masomo yote katika maeneo yote ya nchi.
2. Kuwekwa kwa amri ya kutotoka nje kitaifa kila usiku, kuanzia saa 4 usiku hadi saa 11 alfajiri (22h00–05h00).
3. Marufuku kwa wanachama wote wa serikali ya zamani kuondoka nchini.
Maamuzi haya, ambayo ni ya muda na ya lazima, yamelenga kuhakikisha usalama wa umma na kuandaa mazingira ya mpito wa amani. Kamati inatoa wito wa utulivu na uwajibikaji. Huduma muhimu zitaendelea kutolewa.
Kwa niaba ya Kamati,
Uongozi wa Juu
Nchi bado haijatulia
Baada ya taarifa iyo ikaja ya kutangaza bado mamlaka yapo chini yake ila rais kaifaziwa kwenye ubalozi wa ufaransa wa nchi iyo, hawez kwenye kutolewa kwa itifaki za diplomasi tu, ila akitoka wanae
Kiongozi wa mapinduzi wa Benin Lieutenant colonel Pascal Tigri akiongea na wananchi
Tigri amesema bado serikali ipo chini yake na kutoa onyo kwa Ufaransa isiingilie mambo ya ndani ya Benin
Tigri pia amewataka wananchi wazidi kuliunga mkono jeshi lake
Kwasasa raisi wa nchi hio Patrice Talon yupo kwenye ubalozi wa Ufaransa alipohifadhiwa
Jeshi la Benin limegawanyika ambapo kuna walipwatiifu kwa serikali ya Talon na kuna walioupande wa Tigri
Hata wananchi pia wanaonekana wengi wapo upande wa Tigri