Narudia tena, ni hatari kupigana vita na hivi vikundi kama Hamas, Hizbollah nk, hawa wameshajikataa na hawana cha kupoteza.
Vita na hivi vikundi vinaleta stress maana hamjui siku wala saa vita itakapoisha.
Netanyahu anajidanganya atawamaliza hawa jamaa lakini ni uongo, hapo anatesa watu wake tu, ameua head wa Hizbollah na Hamas, ameua makamanda wale top lakini jamaa bado wanapigana kama ndio vita inaanza vile.
Israeli alipaswa ajifunze somo la Afghanistan, USA alipata stress na Afghanistan, matokeo yake akaamua kuitelekeza mission na kuondoa na kuwaacha wataleban wajiamulie watakacho.
USA akae chini ajaribu kudraft jambo amani ya kweli ipatikane mashariki ya kati, vinginevyo shoga yake Israeli hawawezi kuishi Kwa amani pale, na dunia inapoelekea vile vikundi na nchi maadui wanaweza kupata technolojia kubwa ambayo inaweza kuisambaratisha Israeli pale.