Tuache uzushi na propaganda , mhariri mkuu wa gazeti asimulia alichokiona Goma na Bukavu
22 February 2025
MGOGORO WA DR Congo :
Yaliyokutwa katika ghala la silaha za askari wa Tshisekedi na mipango yake ya kuvamia Rwanda
View: https://m.youtube.com/watch?v=STZBGC_UncE
Mhariri mtendaji James Munyaneza wa The New Times Rwanda atoa ushuhuda wa kina alipopata fursa kuwepo Goma na leo akiwa studio pamoja na mwandishi James Kahuranga kwa njia ya simu akiwa Rusizi kutupa habari za kina...
Inaonesha FARDC walikuwa wamejipanga kuivamia Rwanda kutokana na mpangilio wa zana zilivyopangwa (formation) kuelekea nchi ya Rwanda. Mhariri mtendaji James Munyaneza anasimulia kwa undani hali hiyo alivyokuwa amejipanga Tshisekedi ..
Mhariri mtendaji James Munyaneza alichokiona Goma ni uthibitisho unaoweza kuchukuliwa kuwa kulikuwa na mkakati mpana wa jeshi la Congo FARDC, Burundi kuivamia Rwanda kama tukio la bahati la M23 wasingejitokeza na kutibua mipango hiyo kwa ...
Mhariri mtendaji James Munyaneza aliweza kufika eneo la Airport ya Goma ambapo kilikuwa kitovu cha mapambano makali baina ya FARDC na M23 yaliyotokea wiki mbili zilizopita ....
Mhariri mtendaji James Munyaneza aliweza kufika kambi iliyokuwa na hadhi ya Joint Command Centre iliyokuwa inaratibu mipango ambapo kulikuwa na milingoti minne ya bendera kuwakilisha jeshi la Congo FARDC, jeshi la Burundi, jeshi la SADC SAMIDRC, jeshi la BURUNDI na FDLR - mgambo wa intarahamwe
Na kuwa ...Joint Command Centre hiyo ni kambi ongozi ya Operesheni za kijeshi kuna nyaraka na ramani zilizotokana ukusanyaji wa intelejesia ya kijeshi zinazobainisha maeneo mkakati nyeti ambayo FARDC na FDLR wangeyashambulia Rwanda... zilizoachwa baada ya kambi hizo kukimbiwa kufuatia kipigo kutoka kwa M23
Kilima Nyoka vilikuwepo vikosi special forces wa FARDC wakiwa wamejichimbia wanataza mpaka wa Rwanda na Kanyamahoro kulikuwepo kambi ya FDLR iliyo kilometa 3 tu kutoka mpaka na Rwanda..
Kambi zenye majina ya Satan 2 (shetani) Armageddon (Ziwa la Moto) majina hayo yakiashiria unyama unyama na silaha kali za maangamizi zilizo tayarishwa kuishambulia Rwanda ...
Kambi za mamluki waliosema ni 'wataalamu' kwa kumaanisha wangekuwa wanatoa ujuzi wa kutumia silaha hizo za maangamizi za 'shetani' na 'Ziwa la Moto' kuitia adabu Rwanda ..
View attachment 3252482
Kwa hiyo majeshi haya FARDC, kikosi cha ulinzi wa Rais, FLDR, mamluki wote hawa wangejiunga pamoja kuivamia Rwanda kwa kustukiza ... kama M23 wasingeanzisha mashambulizi February 2023..
Makontena yaliyosheheni silaha za mizinga ya masafa marefu ya kila aina , RPG , sniper rifles, kamikaze drones, camera ikionesha ingekuwa vita ya kisasa ...
Masimulizi hayo ya Mhariri mtendaji James Munyaneza yanakwenda na video mwendo ndani ya mahojiano haya ya ushuhuda wa kina..
Wataalamu kijeshi, utambuzi (intelejensia) ya kijeshi na intelejensia ya kiraia wanasema mkusanyiko huo wote wa mikakati, silaha, utaalamu, matayarisho mazito ya upande wa serikali ya Tshisekedi jirani na mpaka wa Rwanda. i
Inaonesha hayakuwa kujitayarisha kuishughulikia majeshi ya waasi wa M23 bali lengo lilikuwa kukamilisha tamko la Tshisekedi kuwa wataipiga Rwanda na kubadilisha uongozi wa kiserikali uliopo nchini Rwanda..
Vifaa vya Tshisekedi vilivyokutwa na M23
View attachment 3252480