Tetesi: Wanajeshi wa Tanzania na wenzao wa SADC Washikiliwa Mateka kama Mateka wa Vita na Wanamgambo wa M23 huko Goma

Tetesi: Wanajeshi wa Tanzania na wenzao wa SADC Washikiliwa Mateka kama Mateka wa Vita na Wanamgambo wa M23 huko Goma

Kwa hiyo Rwanda aendelee kuua na kuteka askari wetu kwa sababu tu tulimwekea vikwazo tunaumia? Huko CCM mnajaza funza kwenye vichwa vyenu nini?
Hao wacongo wanakuhusu nini wewe? Hao watu wa Bukavu wenyewe wanawashangilia M23, wewe kisorokwinyo unajidai unauchungu sana na watu wa Bukavu kama sio uchizi huo ni nini
 
Hii issue ni serious sana. Nilitegemea hivi sasa hatua dhidi ya Rwanda zingekuwa zimeshaanza kuchukuliwa maana ushahidi upo wazi kuwa wanajeshi wa Rwanda zaidi ya 4000 walivuka mpaka kuingia Goma na kuiteka. So it's obvious Wanajeshi wetu waliouliwa waliuliwa na Wanajeshi wa Rwanda na Hawa waliotekwa wametekwa na Jeshi la Rwanda kwa mgongo huu wa M23.
Mnajuaje kuwa hakuna viongozi wa nchi hii wanaofaidika na vita hivi. DRC ni shamba na labda vikosi kuendelea kuwa huko ni project.
 
Propaganda nilete mimi? Unaweza jifananisha na mimi kwa uzalendo juu ya nchi yangu wewe?

Hiyo habari nimeitoa X nq imepostiwa leo saa kumi na mbili jioni.
Hakuna hiyo kitu. Kwa huo weledi wako ulipaswa kujiridhisha kidogo kabla ya kuisambaza. Goma airport iko mikononi mwa M23 tangu Januari 27 na 28. Halafu askari wetu hawapigani kule hao wahuni tu wanaeneza propaganda nyeusi za kitoto.
 
Kuna taarifa imetolewa jioni hii na Waandishi wa Habari Kupitia Mtandao wa X (Zamani Twitter) waliopo Goma ambayo inaeleza wametaarifwa na Wanamgambo wa M23 kuhusu kutekwa kwa Wanajeshi wa SADC kutoka Mataifa ya Afrika Kusini, Malawi na Tanzania waliopo Goma.u

Kwenye taarifa yao, waandishi hawa wameelezwa na Wanamgambo wa M23 kuwa Wanajeshi wetu wanashikiliwa mateka kwenye kambi zao ambapo wameweka bendera nyeupe kama ishara ya ku surrender.

Taarifa hiyo pia imewataja moja kwa moja wanajeshi wa Tanzania na kuelezea kuwa walishiriki kwenye vita dhidi ya M23 na kushindwa mapambano hivyo kuchukuliwa mateka.

Maombi yangu.
Kama taarifa hizi ni za kweli naomba Serikali yetu ianze kuchukua hatua kwa kuwawekea vikwazo Rwanda na kuchukua hatua nyingine za kijeshi dhidi ya Rwanda.

Nimeumia sana kama Mtanzania mzalendo!
View attachment 3252351View attachment 3252359
View attachment 3252361
Waandishi akina Kabendera hizi ndio fani zao sasa.
 
Ni aibu kama ni kweli wanajeshi wetu tunaowategemea wamekalishwa

Kama ni kweli hii habari..basi kama nchi tumekwisha tubaki tu kulinda mipaka yetu dhidi ya uvamizi!

Japan ni kisiwa ila kiliwahi kutawala dunia
Rwanda ni kama Israeli. Hii statement watu hawataki kuikubali
 
Mnajuaje kuwa hakuna viongozi wa nchi hii wanaofaidika na vita hivi. DRC ni shamba na labda vikosi kuendelea kuwa huko ni project.
Kuna Fact sheet iliandikwa kuhusu Gold Mafia in Afrika ndio utaelewa kwanini vita haiwezi kuisha kirahisi Congo.
Huenda Kuna watu wengi ikiwemo majirani za Kongo wanafaidika sana
 
Si
Uingereza hajauliwa wala kutekwa askari wake ila kamwekea vikwazo Rwanda. Sie tunashindwa wapi?
ku hizi nina kusoma na kukuelewa vizuri, hasa haya maswala ya kudhalilishwa kama nchi chini ya CCM iliyo oza muda kitambo.
Kuhusu huo mstari nilio u'quote' hapo; nataka kukutahadharisha, na jaribu kuelewa ninalenga kitu gani hapa.
Chini ya CCM serikalini mwetu watu wanaofanya maamuzi muhimu sasa hivi ni watu wasiokuwa na uzalendo wowote juu ya nchi hii. Tuna watu toka kwenye nchi hizo unazo zizungumzia humu ambao wameshika nafasi muhimu ndani ya serikali yetu. Huwezi kutegemea wafanye maamuzi dhidi ya wenzao walioko nje.
Ni hivi: kama unadhani tuko salama na nchi kama Rwanda, Uganda na Kenya, utakuwa unajidanganya sana. Ni swala la muda tu, kama tusipokuwa makini hapa hapa tutavurugwa.

Nimalize kwa kusikitika pamoja na wewe, kwa kuona nchi yetu imedidimia kiasi hiki nyakati hizi. Binafsi naomba tuachane kabisa na hili la kupeleka wanajeshi wetu nje, kama sababu ya wao kwenda huko siyo kwenda kupigana vita moja kwa moja na kushinda vita hiyo.
Hii tabia ya kupeleka vijana wetu bila ya kuwapa maagizo sahihi na uwezo wa kushinda vita wanayo kwenda kupambana nayo tuachane kabisa nayo.

Pia nikutahadharishe: hivi vihabari vya kuokoteza kama hivi vya hao waandishi, bila kujuwa ni akina nani hawa; usije kushangaa ni kundi la Kagame hilo liko kazini kupotosha na kupiga propaganda.
 
Hii ni akili matope?
Mhariri ni mnyarwanda unategemea amkaange Kagame?
Acha makasiriko.....huo ndio ujnja w kagame kwamb anatuzidi kwa mengi.

Lete wahariri wako sasa tusikie.
Watu watasikiliza kilichopo.
 
Ni aibu kama ni kweli wanajeshi wetu tunaowategemea wamekalishwa

Kama ni kweli hii habari..basi kama nchi tumekwisha tubaki tu kulinda mipaka yetu dhidi ya uvamizi!

Japan ni kisiwa ila kiliwahi kutawala dunia
Tunapambania watu wa Goma huko Congo wakati wao M23 wanaifurahia mpaka wanashangalia mitaani. Sasa sisi tunapigani nini hapo sasa? Yawezekana Rais wa Congo anjua huko ndo kuna Masalia wa Kinyrwanda hawapeleki huduma yoyote kama Serikali. Bado nashangaa wnanchi wa Goma kufurahia na kuwashangilia M23
 
hawa watu ilikuwa tuwape kichapo..tatizo amiri jeshi mkuu wetu yupo soft mno sio mtu wa kufanya maamuzi magumu na pia hataki lawama na anayependa sana kubembeleza kuliko actions..
Mbona alishatoa maelekezo kwa jeshi kupambana na M23?
 
Mbona alishatoa maelekezo kwa jeshi kupambana na M23?
rais wetu hawezi kuyapa maelekezo majeshi ya pamoja yaani SARMIADC na MONUSCO walio chini ya mwamvuli wa umoja wa mataifa ambao sheria zao haziruhusu majeshi hayo ya pamoja kupigana vita zaidi ya kulinda amani na kujihami wao tu hata kama wao ndio wanashambuliwa na waasi basi wajihami tu na sio vita hasa ndio hivyo unasikia wanatekwa na m23 sababu sheria inawabana kujibu mapigo wanapaswa kujilinda tu..kwa lugha rahisi hao UN na jeshi lao wanatumika tu kulinda maslahi ya mabeberu..ndiomaana tsheked anawataka majeshi ya kigeni waondoke anawaona mizigo tu kama hawapigani wa kazi gani sasa.!
 
Si
ku hizi nina kusoma na kukuelewa vizuri, hasa haya maswala ya kudhalilishwa kama nchi chini ya CCM iliyo oza muda kitambo.
Kuhusu huo mstari nilio u'quote' hapo; nataka kukutahadharisha, na jaribu kuelewa ninalenga kitu gani hapa.
Chini ya CCM serikalini mwetu watu wanaofanya maamuzi muhimu sasa hivi ni watu wasiokuwa na uzalendo wowote juu ya nchi hii. Tuna watu toka kwenye nchi hizo unazo zizungumzia humu ambao wameshika nafasi muhimu ndani ya serikali yetu. Huwezi kutegemea wafanye maamuzi dhidi ya wenzao walioko nje.
Ni hivi: kama unadhani tuko salama na nchi kama Rwanda, Uganda na Kenya, utakuwa unajidanganya sana. Ni swala la muda tu, kama tusipokuwa makini hapa hapa tutavurugwa.

Nimalize kwa kusikitika pamoja na wewe, kwa kuona nchi yetu imedidimia kiasi hiki nyakati hizi. Binafsi naomba tuachane kabisa na hili la kupeleka wanajeshi wetu nje, kama sababu ya wao kwenda huko siyo kwenda kupigana vita moja kwa moja na kushinda vita hiyo.
Hii tabia ya kupeleka vijana wetu bila ya kuwapa maagizo sahihi na uwezo wa kushinda vita wanayo kwenda kupambana nayo tuachane kabisa nayo.

Pia nikutahadharishe: hivi vihabari vya kuokoteza kama hivi vya hao waandishi, bila kujuwa ni akina nani hawa; usije kushangaa ni kundi la Kagame hilo liko kazini kupotosha na kupiga propaganda.
Asante kwa kunisoma na kunifuatilia.

Asante pia kwa tahadhari yako. Namjua sana Kagame kwa propaganda. Ni mzuri sana kwenye eneo hilo hasa anapotaga kupitisha au kuhalalisha agenda zake.

Kwa miaka ya hivi karibuni nmekuwa nahofu kubwa sana juu ya mustakabali wa nchi yetu. Kuna muda niliwaza kuwa Tina Viongozi incompetent walioteuliwa kutokana na kuwa watu wa chama, kujuana na viongozi wakubwa au uchawa ila nikaja kugundua ni zaidi ya hayo.

Suala la kuwa na mapandikizi nimelisikia kwa watu wengi na itakuwa ni kansa nyingine inayotuangamiza kama Taifa.

Katika kipindi hiki ni vizuri kuwa na hoja za namna hii ili kuwasaidia hawa watu ambao imetokea kwa bahati mbaya ndiyo wameshika nafasi za maamuzi kwenye nchi yetu.

Pia ni vizuri kuwapa moyo wanajeshi wetu kuwa nchi yetu bado ina watu wazalendo wanaowapenda na kuwahitaji kufanya vizuri.
 
Mpaka wanajekwa hapo maana yake ni kwamba Sheria zimevunjwa hivyo wanaruhusiwa kujihami na Rais wetu anaruhusiwa kutoa amri zaidi.
 
Tulishaandika sana kama vipi Tanzani itoe kikosi chake huko mashariki mwa congo kilicho chini ya jeshi la kimataifa la kulinda amani huko. Waasi wanazidi kuteka maeneo huko, ya nini wanajeshi wetu waaibike huko kama hakuna maslahi kwa nchi? Kagame akiwekewa vikwazo mizigo yake haitapitia bandari za Tanzania. DRC iachwe ijipambanie yenyewe, kama kagame ataimega congo au kuichukua yote aachwe tu ila ajue naye atabondwa na kubondeka
si anapita mombasa
 
Hakuna hiyo kitu. Kwa huo weledi wako ulipaswa kujiridhisha kidogo kabla ya kuisambaza. Goma airport iko mikononi mwa M23 tangu Januari 27 na 28. Halafu askari wetu hawapigani kule hao wahuni tu wanaeneza propaganda nyeusi za kitoto.
The main issue hapa ni askari wetu kuwa chini ya mateka ya M23.
 
Jeshi la tanzania linavyo onekana congo huko
IMG_0719.jpeg
 
U
Pia ni vizuri kuwapa moyo wanajeshi wetu kuwa nchi yetu bado ina watu wazalendo wanaowapenda na kuwahitaji kufanya vizuri.
USalama wa nchi yetu siyo jambo la mzaha hata kidogo. Huu utawala wa CCM sasa hivi hauelewi unyeti wa swala hili.
Huwezi kupeleka vijana wetu kimzahamzaha bila ya kuwa na lengo maalum na kuwapa maagizo sahihi ni nini wanatakiwa wakifanye.
Matokeo yake ndiyo haya ya Kagame sasa kujipima nguvu. Safari nyingine ataingia Karagwe!
 
😂😂 nacheka kama mazuri , na siku hizi jeshi watu wanaajiriwa kwa kujuana sio kwa vipaji na uhodari , watu wanaenda kwa ajili ya kupokea mishahara aseee tutabondwa hadi tuchakae
 
Back
Top Bottom