Kuna taarifa imetolewa jioni hii na Waandishi wa Habari Kupitia Mtandao wa X (Zamani Twitter) waliopo Goma ambayo inaeleza wametaarifwa na Wanamgambo wa M23 kuhusu kutekwa kwa Wanajeshi wa SADC kutoka Mataifa ya Afrika Kusini, Malawi na Tanzania waliopo Goma.u
Kwenye taarifa yao, waandishi hawa wameelezwa na Wanamgambo wa M23 kuwa Wanajeshi wetu wanashikiliwa mateka kwenye kambi zao ambapo wameweka bendera nyeupe kama ishara ya ku surrender.
Taarifa hiyo pia imewataja moja kwa moja wanajeshi wa Tanzania na kuelezea kuwa walishiriki kwenye vita dhidi ya M23 na kushindwa mapambano hivyo kuchukuliwa mateka.
Maombi yangu.
Kama taarifa hizi ni za kweli naomba Serikali yetu ianze kuchukua hatua kwa kuwawekea vikwazo Rwanda na kuchukua hatua nyingine za kijeshi dhidi ya Rwanda.
Nimeumia sana kama Mtanzania mzalendo!
View attachment 3252351View attachment 3252359
View attachment 3252361