Wanajeshi wa Tanzania takribani 2000 walifyekwa na majeshi ya Idd Amin; huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya Kagera

Wanajeshi wa Tanzania takribani 2000 walifyekwa na majeshi ya Idd Amin; huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya Kagera

Vitano lazima uwe na chabo hivyo hao walitangulizwa kama chabo na kupunguza risasi za adui na kuwajengea kujiamini adui ili a relax na hpo ndipo wanapoibuka wanaume na kufanya yao . wale mgambo na polisi ndo chabo.
 
Unaua vipi askari 2000 kwa mda mfupi?
Soma au fuatilia vizuri historia ya luteni enzi hizo japo alistaafu akiwa na cheo cha meja bila Shaka aliitwa John Walden afu pia hilo tukio Amin alilitegemea na njia yao ya kupita aliijua lakini ukumbuke kwamba waliotangulizwa walikuwa ni wale wazalendo wa nchi yao waliojitolea tu na wakapata mafunzo ya muda mfupi Sana tuseme walikuwa migambo

Natamani kuendelea kukufahamisha ila nahisi usingizi hivi (kifupi hao waliotangulia hawakuwa na mbinu za kivita za mm au km

Na lengo la amiri jeshi mkuu lilikuwa ni kuona adui yake (Amin) amejipanga vipi yuko wapi na kashika njia gani ukumbuke muda huo bado ujenzi wa daraja liliovunjwa kagera lilikuwa linaendelea kujengwa.unadhani bila hiyo mbinu lazima nduli angewafuata pale wasifanikishe azima yao

Ngoja nilale endeleeni kubisha
 
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amini.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na jinja ambapo Idd Amini alitimkia Libya na baadae saudi Arabia.

Hii historia sjiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.
Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amini aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.
Mahusiano ya wazazi wangu walikutania huko,,,yaan huwa nafarijika mno mno

Naamini love at first sight

Ee mwenyez mungu walinde wazazi wangu,wajalie yote waombayo katika nafsi ya kukuamini wewe.
 
AISEEE KUMBE KUNA MENGI WANAFICHA KUHUSU VITA HII???!!!INAWEZEKANA HATA USHINDI HAUKUWA WA KISHINDO KAMA TUNAVYOAMINISHWA
wewe ni bogus! Kama kuna kilichofichwa kuhusiana na vita ya Kagera, BBC walipata wapi hizo taarifa? uwe unatafuta literatures na kujisomea badala ya kusubiri simulizi za BBC, ebo!
 
Nadhani data au takwimu halisi za wanajeshi waliopteza maisha wakati wa vita ya Kagera ipo pale Ngome....na haitusaidii sana kwa sasa zaidi ya kuadhimisha siku ya mashujaa na kuangalia familia zao.
 
Huu ni upuuzi tu na kuzalilisha jeshi letu vyombo husika vikanushe habari hizi
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amini.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na jinja ambapo Idd Amini alitimkia Libya na baadae saudi Arabia.

Hii historia sjiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.
Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amini aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.
 
Kwani makaburi ya Bunazi-Kagera yakihesabiwa inapatikana idadi gani?
 
Huyo babu ni mzushi eti bila Tanzania kusaidiwa wasingemuweza Idd Amin. Huyu jamaa lazima atakuwa lofa tu.
Tulijipanga kwa vita? Kama ndiyo basi hiyo vita haikuwa nyepesi kwetu. Ndiyo maana Marekan anajiandaa kwa lolote hivyo usimkejeli huyo mzee huenda kuna chembe za ukweli
Kosa tulilofanya ni kuwatanguliza FFU na migambo mbele, ilikuwa bado haija aminika kuwa jeshi la amin limevuka mpaka,
 
Wengi humu yaelekea hawakuwepo wakati huo.

Amin alijiandaa kwa vita ile mapema. Tanzania haikuwa na maandalizi. Jeshi la Amin lilikuwa na vifaa vya kisasa zaidi kuliko jeshi letu.

Kwa taarifa za ndani ni kuwa askari wa mwanzo kwenda mstari wa mbele walikuwa ni mgambo na JKT. Na baadaye walifuata askari wa kutoka kikosi cha Zanzibar. Vikosi hivi vya mwanzo au viliteketea kabisa au walibakia manusura wachache.

Amin alikuwa akisaidiwa na makaburu na Gadafi wa Libya. Tanzania tulipata msaada mkubwa toka kwa Fidel Castro wa Cuba.

Tanzania ilishinda vita vile kutokana na moyo wa kujitoa, weledi, umoja na uzalendo lakini siyo kwa ubora wa vifaa.

Ile ilikuwa ni vita, siyo sherehe. Tulivamiwa. Aliyevamia alijiandaa. Mshindani wako ambaye mmekaribiana kwa kila hali, siyo rahisi umshinde wakati wote na kila mahali. Waulize waliopigana vita vile ndiyo watakueleza ugumu ulivyokuwa. Unafuu ulikuja mwishoni, wakati Jeshi la Uganda likiwa limegawanyika na kukosa uongozi wa pamoja.
 
Umeeleza vema, naona wengi wanaropoka kutetea bila hoja, au kupinga bila hoja.... ndo maana watanzania ni wepesi kufall ktk propaganda
 
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya Kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amin.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na Jinja ambapo Idd Amin alitimkia Libya na baadae Saudi Arabia.

Hii historia sijiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.

Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amin aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.
kwa kua bbc imesema wewe unakubali tu kama zuzu.
 
sidhani kama ni kweli babu Mjomba kaka zangu wawili wote walikuwa vitani Mimi nilitoroka nyumbani na wote walirudi na sikuwahi kusikia
Ni kweli vita ya Uganda ilipoteza Asikari wengi sana wa Tanzania na kilichookoa Habari isijulikane sana ni ushindi walioupata ingawa ushindi wenyewe ulitokana na kuwakuta waasi porini yaani Akina Mseveni na Tito Okelo ambao walisaidia kuwaonyesha njia za kupitia na kuwadhibiti Jeshi la idd Amin, na kama si waasi hao kwa kweli idd Amin angewasaga sana maana alikuwa na Jeshi kali na vifaa vizuri toka libya.
 
Back
Top Bottom