Wengi humu yaelekea hawakuwepo wakati huo.
Amin alijiandaa kwa vita ile mapema. Tanzania haikuwa na maandalizi. Jeshi la Amin lilikuwa na vifaa vya kisasa zaidi kuliko jeshi letu.
Kwa taarifa za ndani ni kuwa askari wa mwanzo kwenda mstari wa mbele walikuwa ni mgambo na JKT. Na baadaye walifuata askari wa kutoka kikosi cha Zanzibar. Vikosi hivi vya mwanzo au viliteketea kabisa au walibakia manusura wachache.
Amin alikuwa akisaidiwa na makaburu na Gadafi wa Libya. Tanzania tulipata msaada mkubwa toka kwa Fidel Castro wa Cuba.
Tanzania ilishinda vita vile kutokana na moyo wa kujitoa, weledi, umoja na uzalendo lakini siyo kwa ubora wa vifaa.
Ile ilikuwa ni vita, siyo sherehe. Tulivamiwa. Aliyevamia alijiandaa. Mshindani wako ambaye mmekaribiana kwa kila hali, siyo rahisi umshinde wakati wote na kila mahali. Waulize waliopigana vita vile ndiyo watakueleza ugumu ulivyokuwa. Unafuu ulikuja mwishoni, wakati Jeshi la Uganda likiwa limegawanyika na kukosa uongozi wa pamoja.