Wanajeshi wa Tanzania takribani 2000 walifyekwa na majeshi ya Idd Amin; huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya Kagera

Taarifa za ndani kbs, ni 2700 ndo waliuawa pale mpakani , na taarifa zinasema bado Mwl Nyerere alikuwa anasita kusaini nchi iingie vitani, ndipo akina msuguri wakamwambia ukigoma siye tunaingiza majeshi bc kwa shingo upande ikabidi asaini tu
 
Hapana, vita ni ile ile tu, sema majeshi yetu yali struggle sana kuvuka kuingia Uganda
 
Walikufa wanajeshi Wengi sijui idadi..
Ndo maana kulikuwa na vita mbili
Ya mwaka 1978 ndo tulishindwa wakafa Wengi...tukaenda kujipanga mwaka 1979 ndo tukarudi tena..
Inasemekana tukipeleka Sana mgambo mstari wa mbele...

Uganda walikuwa na silaha Kali sana only wanajeshi wao Wengi walikuwa hawana morali....Sisi tulikuja kukopa hela nyingi tukanunua silaha Kali baadae mwaka 1979 ndo tukaenda kushinda
Wengi hawajui hili
 
hizi ndio tunaita propaganda.
Wengi hawajui hili
Ninyi Vijana acheni kudanganywa! Hata ukisoma vitabu vilivyoandikwa Kuhusu vita ya Uganda, takwimu kama Hizo hazimo. Aidha Ukienda pale Kaboya kwenye makaburi walipozikwa wanajeshi waliokufa vitani Uganda, takwimu Hizo hazipo. Wanajeshi waliokumbwa na uvamizi ule, maili 10 kutoka mpaka wa Mutukula walikuwa detachment Moja na troop Moja. Hawatimii hata watu 100. Aidha kutokana na ukubwa wa kikosi Cha Amin kilichovamia, askari wetu hao waliwahi kupata Taarifa za uvamizi na wakawahi kuondoka Kisha kuvuka Mto Kagera na kuja maeneo ya Kasambya Mashariki ya Daraja la mto Kagera kabla ya kuvunjwa daraja Hilo.
Yawezekana Watz waliouawa kwenye vita Ile kuwa wengi ukijumlisha na Raia Ambao waliuliwa na askari wa Amini kuanzia Mpakani Mutukula Hadi kwenye daraja. Maana raia wengi wa maeneo hayo walijua waliokuwa wakifuatwa ni askari na sio raia. Kwahiyo wengi waliuawa. Maiti za raia wengi zimeonyeshwa katika vitabu kadha vinavyosimulia vita hiyo na siyo Askari.
Halafu wanasema kuwa Magambo na askari wa majeshi mengine waliokuwa mobilized ndio waliuawa, siyo Kweli. Kwani askari hao walichanganywa vyema na askari wa JW na ilikuwa vigumu kuwatofautisha. Nakumbuka ni Brigedi Moja TU ambayo ilikuwa na mchanganyiko mkubwa wa mgambo Ndiyo ilipata matatizo pale Lukaya, napo ni BAADA ya kukabiliana na askari walioingia vitani kutoka Libya na walikuwa na silaha nzito. Kwa ushujaa mkubwa silaha zote Hizo na askari wa Libya walitekwa, kutokana na umakini wa mbinu za Jeshi Letu! Pia tunaambiwa askari waliouawa kwenye actual war hawakufika100. Ila wengi waliouawa Uganda ni baada ya vita. Wengi waliuawa kwenye starehe, ajali, sumu, nk.

Ujue wanajeshi 2000 kuuawa vitani ni karibia Brigade nzima. Ingetokea hivyo vita Ile ingechukua muda mrefu sana! Lakini nakumbuka ilikuwa rahisi kwasababu ndegevita zote za Uganda ziliteketezwa kabla majeshi yetu hayajavuka daraja la Kagera. Zote zolitunguliwa Kila zilipotumwa kuja kushambulia daraja au kufanya uchunguzi. Hii ilitokana na silaha makini za kuangusha ndege wakati ule. Aidha vifaru vingi vya adui vilifutwa kabla ya kufika Lukaya na Mpigi, miji ya mwisho kabla kuingia Kampala. Nakumbuka kifaru chetu kimoja ndicho kiliteketezwa wakati tunavuka daraja la Karuma Falls karibu na njiapanda za kwenda Arua, Lang'o na Gulu.
Kwahiyo kitendo Cha kuangamiza ndege vita na vifaru vyao mapema, ilikuwa lift tosha ya kuikamilisha Ops Chakaza Kwa urahisi kabisa.
Kwahiyo Vijana hebu jaribuni kufanya tafiti mnaposikia mambo mazito kama haya, kabla hamjaandika humu. Hata ku Google mnashindwa?
 
Duuuhh, umenifungua kidogo
 
Acha uongo kaka kweli wewe kama mtu mzima unakaa apa na kutwambia mambo ya kiongo yaani vita nzima ambayo ilichukua almost miaka miwili ndo wafe askari 100 tu wa kitanzania kweli mzee ivi ulipomaliza kuandika hili bandiko ulifanya preview kweli kwa tec gani ya kuzuia madhara kwa askari wake ambayo tz alikuwa nayo kipindi kila je kwa amoured car zip tz alikuwa nazo kipindi icho useme angalau zilisaidia kupunguza madhara kwa askari wetu je kwa organization ama road map ipi iliyotumika ya kupunguza madhara kwa askari wetu acha ujinga bhana wewe ni mtu mzima ikiwa ni kweli ulikuwa vitani basi ulivyokuwa ukiona kikosi chako kimefanikiwa kulipua ama kuteka kifaru basi ujue ni ivyo ivyo na jeshi la Uganda kuna sehemu kikosi chake kilikuwa kinalipua ama kuteka deraya ama vifaru vya ktz kama ulikuwa unaona mnafanya ambushi na kuua askari wa ug basi ni ivyo ata kwa askari wa tz sehemu ya vita nao walikuwa wanapigwa ambush na kuuawa ivyo ivyo maana pande zote mbili zilikuwa zinatumia risasi za moto na si za mpira acha mambo ya kitoto bhana kwaiyo kwa kuwa wewe ulibahatika Mungu akakulinda hukutekwa wala kufa unadhani iyo bahati ilikuwa kwa wote aisee uzalendo wa akili kama hizi ni ujinga mtupu huu si uzalendo bali ni upumbavu mkubwa wa akili yaani unadanganya kwa ajili ya nini ama kwa faida gani ikiwa tayari vita ilishaga isha na tz alishaga shida jifunze kuusema ukweli ata kama ni mchungu lakini utakusaidia kwenye maisha yako

Urusi apa tu ambayo ni giant mmoja wapo duniani na ana tec ya kufuru lakini kila siku askari wake zaid ya 100 mpaka 200 wanalamba mchanga the same tu Ukraine ije kuwa tz ambayo kipindi kile ilikuwa bado iko kwenye zama za mawe broo narudia tena acha upumbavu huo wala sio uzalendo bali ni upumbavu uliotukuka

Swali je unadanganya kwa faida ya nani

Kwa maslahi yapi

Kwa mustakabali gani

Huu uzalendo kama huu mi sikutaki asee
 
Naamini ungeweza kuchangia vyema bila kutukana na kukejeli,. Sijui vizuri lkn unaonekana bado mtoto
 
Niqe mtoto ama mtu mzima lakini uongo wa kijinga acheni how comes vita iliyochukua almost 2 years mje kutwambia kuwa ni askari 100 tu wa ktz ndo walipoteza maisha ivi kweli mna alili timamu asee
 
Ninyi Vijana acheni kudanganywa! Hata ukisoma vitabu vilivyoandikwa Kuhusu vita ya Uganda, takwimu kama Hizo hazimo. Aidha Ukienda pale Kaboya kwenye makaburi walipozikwa wanajeshi waliokufa vitani Uganda, takwimu Hizo hazipo. Wanajeshi waliokumbwa na uvamizi ule, maili 10 kutoka mpaka wa Mutukula walikuwa detachment Moja na troop Moja. Hawatimii hata watu 100. Aidha kutokana na ukubwa wa kikosi Cha Amin kilichovamia, askari wetu hao waliwahi kupata Taarifa za uvamizi na wakawahi kuondoka Kisha kuvuka Mto Kagera na kuja maeneo ya Kasambya Mashariki ya Daraja la mto Kagera kabla ya kuvunjwa daraja Hilo.
Yawezekana Watz waliouawa kwenye vita Ile kuwa wengi ukijumlisha na Raia Ambao waliuliwa na askari wa Amini kuanzia Mpakani Mutukula Hadi kwenye daraja. Maana raia wengi wa maeneo hayo walijua waliokuwa wakifuatwa ni askari na sio raia. Kwahiyo wengi waliuawa. Maiti za raia wengi zimeonyeshwa katika vitabu kadha vinavyosimulia vita hiyo na siyo Askari.
Halafu wanasema kuwa Magambo na askari wa majeshi mengine waliokuwa mobilized ndio waliuawa, siyo Kweli. Kwani askari hao walichanganywa vyema na askari wa JW na ilikuwa vigumu kuwatofautisha. Nakumbuka ni Brigedi Moja TU ambayo ilikuwa na mchanganyiko mkubwa wa mgambo Ndiyo ilipata matatizo pale Lukaya, napo ni BAADA ya kukabiliana na askari walioingia vitani kutoka Libya na walikuwa na silaha nzito. Kwa ushujaa mkubwa silaha zote Hizo na askari wa Libya walitekwa, kutokana na umakini wa mbinu za Jeshi Letu! Pia tunaambiwa askari waliouawa kwenye actual war hawakufika100. Ila wengi waliouawa Uganda ni baada ya vita. Wengi waliuawa kwenye starehe, ajali, sumu, nk.

Ujue wanajeshi 2000 kuuawa vitani ni karibia Brigade nzima. Ingetokea hivyo vita Ile ingechukua muda mrefu sana! Lakini nakumbuka ilikuwa rahisi kwasababu ndegevita zote za Uganda ziliteketezwa kabla majeshi yetu hayajavuka daraja la Kagera. Zote zolitunguliwa Kila zilipotumwa kuja kushambulia daraja au kufanya uchunguzi. Hii ilitokana na silaha makini za kuangusha ndege wakati ule. Aidha vifaru vingi vya adui vilifutwa kabla ya kufika Lukaya na Mpigi, miji ya mwisho kabla kuingia Kampala. Nakumbuka kifaru chetu kimoja ndicho kiliteketezwa wakati tunavuka daraja la Karuma Falls karibu na njiapanda za kwenda Arua, Lang'o na Gulu.
Kwahiyo kitendo Cha kuangamiza ndege vita na vifaru vyao mapema, ilikuwa lift tosha ya kuikamilisha Ops Chakaza Kwa urahisi kabisa.
Kwahiyo Vijana hebu jaribuni kufanya tafiti mnaposikia mambo mazito kama haya, kabla hamjaandika humu. Hata ku Google mnashindwa?

Salute Afande
 
NYERERE ALISOMA NA RAFIKI YAKE KIPENZI MILTON OBOTE.

CHANZO Cha hii vita ni sentensi ya juu.
WENYE kuelewa waelewe, asomaye na Afahamu
 
Acha uongo kaka kweli wewe kama mtu mzima unakaa apa na kutwambia mambo ya kiongo yaani vita nzima ambayo ilichukua almost miaka miwili ndo wafe askari 100 tu wa kitanzania kweli mzee ivi ulipomaliza kuandika hili bandiko ulifanya preview kweli kwa tec gani ya kuzuia madhara kwa askari wake ambayo tz alikuwa nayo kipindi kila je kwa amoured car zip tz alikuwa nazo kipindi icho useme angalau zilisaidia kupunguza madhara kwa askari wetu je kwa organization ama road map ipi iliyotumika ya kupunguza madhara kwa askari wetu acha ujinga bhana wewe ni mtu mzima ikiwa ni kweli ulikuwa vitani basi ulivyokuwa ukiona kikosi chako kimefanikiwa kulipua ama kuteka kifaru basi ujue ni ivyo ivyo na jeshi la Uganda kuna sehemu kikosi chake kilikuwa kinalipua ama kuteka deraya ama vifaru vya ktz kama ulikuwa unaona mnafanya ambushi na kuua askari wa ug basi ni ivyo ata kwa askari wa tz sehemu ya vita nao walikuwa wanapigwa ambush na kuuawa ivyo ivyo maana pande zote mbili zilikuwa zinatumia risasi za moto na si za mpira acha mambo ya kitoto bhana kwaiyo kwa kuwa wewe ulibahatika Mungu akakulinda hukutekwa wala kufa unadhani iyo bahati ilikuwa kwa wote aisee uzalendo wa akili kama hizi ni ujinga mtupu huu si uzalendo bali ni upumbavu mkubwa wa akili yaani unadanganya kwa ajili ya nini ama kwa faida gani ikiwa tayari vita ilishaga isha na tz alishaga shida jifunze kuusema ukweli ata kama ni mchungu lakini utakusaidia kwenye maisha yako

Urusi apa tu ambayo ni giant mmoja wapo duniani na ana tec ya kufuru lakini kila siku askari wake zaid ya 100 mpaka 200 wanalamba mchanga the same tu Ukraine ije kuwa tz ambayo kipindi kile ilikuwa bado iko kwenye zama za mawe broo narudia tena acha upumbavu huo wala sio uzalendo bali ni upumbavu uliotukuka

Swali je unadanganya kwa faida ya nani

Kwa maslahi yapi

Kwa mustakabali gani

Huu uzalendo kama huu mi sikutaki asee
Pamoja na kashfa na matusi lakini Mimi nitakujibu kistaarabu tu! Kilichosaidia Watz wasife wengi vitamini Uganda ni Ile taaluma ya kutopigana vita vya kufuata Barabara tu! Majeshi ya Uganda yalifuata Barabara wakati wa kusonga mbele na kupigana. Watz waliingia Hata maporini! Mfano mzuri ni Hii Brigade ya Black Mamba iliyoambaa Ziwa Victoria ikipita kwenye swamps. Iliwazunguka na Kuwa block askari wa Libya pale Lukaya wakati Brigade ya Marehemu Kombe iliyofuata axis ya Barabara ya Masaka- Kampala ilipokutana na mashambulizi makali ya Walibya.
Black Mamba aliyekuwa kulia ya vikosi vya Marehemu Kombe aliamuru sehemu ya vikosi vyake kuswitch left kutoka mwambao wa Ziwa Victoria akikatisha mapori akawazunguka na kuteka askari wote wa Libya na silaha zao nzito. Baada ya Hapo Ikawa mchakamchaka kupita Mpigi Hadi kuishika Kampala.
Jambo lingine lililotusaidia ni nidhamu ya Hali ya Juu ya wanajeshi wetu ambao walifuata na kutekeleza orders kikamilifu zilizotolewa na viongozi wetu. Tofauti na Waganda ambao, kwamfano ilipotekwa ngome Yao madhubuti ya Mtukula kwenye mahandaki zilikutwa pombe za gongo na askari Wengine walitekwa wakiwa wamelewa hawajitambui! Aidha kutokana na raia wa Uganda kuuchoka Utawala wa Amini, basi Kila Mahali tulipewa msaada kuonyeshwa askari wa Uganda walipo na kurahisisha utendaji kivita upande wa jeshi letu.
Basi ndugu yangu uliyejaa kejeri na matusi naomba unipe takwimu zako na Mahali specific ambapo askari wetu waliuawa kiasi hicho. Aidha rejea vitabu mbalimbali vihusuzo vita hiyo ambayo imeweka wazi askari wetu waliokufa vitani kule Uganda na unaweza ku Google pia! Aidha tembelea kwenye maeneo walipozikwa mashujaa wetu kule Kaboya Kagera na maeneo mengine, utaongeza maarifa kuhusu vita hivyo, badala ya kubunia mambo na kuyaandika humu Bila takwimu bila utafiti wa kutosha!
Halafu unasema vita ilichukua miaka miwili, Siyo Kweli! Vita ilipiganwa Kwa miezi minne, kuanzia Tarehe 30.10.1978 Amin alipotuvamia, hadi tarehe 11.4.1979 pale mji wa Kampala ulipotekwa! Hii Siyo taratibu yangu, ni utaratibu kwamba wakati wa vita, mji mkuu wa Nchi unapotekwa basi ndo mwisho wa vita!
Hata hivyo Baada ya kuiteka Kampala kazi ya kuisafisja Uganda iliendelea Hadi tarehe 2.6.1979 Pale kamanda wa mwisho Jenerali Mti Mkavu alipofika mpakani mwa Sudan na Uganda upande wa Arua (Western Nile District) na kumwarifu Kamanda Musuguri aliyekuwa Maeneo ya Kitgumu (Gulu) kaskazini mwa Uganda. Ndipo ujumbe ukatumwa Kwa Mwenyekiti wa CCM wa kukamilisha kazi tuliyotumwa!

Kwahiyo actual war ilikuwa miezi minne + kuisafisha Uganda mwezi na nusu. Kwahiyo takribani miezi nane ya vita na Siyo miaka miwili uliyoandika!
 
NYERERE ALISOMA NA RAFIKI YAKE KIPENZI MILTON OBOTE.

CHANZO Cha hii vita ni sentensi ya juu.
WENYE kuelewa waelewe, asomaye na Afahamu

Nyerere na Obote walisoma pamoja Chuo kipi? Nyerere alianza kusoma Makerere Mwaka 1943 akisoma Diploma ya Ualimu. Wakati Huo Obote Alikuwa darasa la nne kwao Lira, kaskazini mashariki mwa Uganda. Maana alianza shule darasa la kwanza Mwaka 1940, akaenda Gulu Junior Seminary. Kisha akaenda Soroti College kukamilisha masomo ya sekondari. Ndipo akajiunga na Makerere. Wakati Huo Nyerere Alisha maliza zamani Makerere na MA yake Uingereza, yuko anafundisha Pugu Tabora na Pugu.

Yawezekana kweli chanzo Cha vita ya Uganda, kimojawapo ni Obote na baadhi ya viongozi wa Uganda kukimbilia Tz Baada ya mapinduzi ya Uganda ya Mwaka 1971. Ambapo Amini aliyepindua utawala wa Obote, alihisi wakiwa TZ wanafanya Mipango ya kumpindua! Lakini serikali ya TZ haikuwa na Mpango wa kuivamia Uganda Kwa kutumia majeshi yake. Amin alikosea mwenyewe alipoingia na kuivamia nchi yetu na kuua raia wa Kyaka Waliokuwa hawana silaha za kupigana nae. Kisha kutangaza kuwa eneo lile magharibi ya mto Kagera (Misenyi) ni sehemu ya Uganda na lingetawaliwa kijeshi! Kwa kitendo kile ni Nchi Gani ingenyamaza na kumwacha aue Watu wetu na kumega sehemu ya nchi yetu?
 
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya Kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amin.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na Jinja ambapo Idd Amin alitimkia Libya na baadae Saudi Arabia.

Hii historia sijiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.

Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amin aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.
Nenda kaboya kambi ya jeshi iko wilaya ya Muleba mkoani kagera kuna makaburi mengi ya mashujaa wetu walio fiaya vitani uganda
 
Unaua vipi askari 2000 kwa mda mfupi?
Vita ya urusi na ukereine leo ina mwaka 1 kama sikosei pande zote 2 wamesha kufa zaidi ya wanajeshi 60,000,ukigawanya kila mwezi wanakufa wangapi?
 
Ilikuwa inajulikana, na hata kurudishwa kwa mtangazaji Ben Kiko kutoka uwanja wa mapambano ni kutokana na kuripoti yaliyotokea kiuhalisia, Vita haikuwa rahisi kama za akina Rambo na Komando John

Umenikumbusha mbali sana Comando john, naweza pata hiyo movie youtube mkuu? Ile ndani ya misitu wanapigana
 
Back
Top Bottom