lukubuzo Samsis
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 2,920
- 3,388
kifo kizuri ni kipi?Walikufa kifo kibaya sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kifo kizuri ni kipi?Walikufa kifo kibaya sana
mmh mkuu hata documentaly za vita nazo waziona si halisi 100% kumbuka kuna maigizo na documentaly always huwa ni fact tupu sizungumzii sinema za kina rambo mimi so utoto wangu na wako tukiweka vipimo nani sijui ataonekana mtotoHakuna snema halisi 100%
Acha utoto
La waparestina nakuunha mkono
So umeenda offpoint kabisa kuhusu vita ati waulizwe watu wa Kagera? wadhania hiyo vita imepigwa Kagera peke yake unaonesha u mweupe kichwani na huwezi simama kwenye debate yeyote ile humu jf... yaani kama umesoma basi uliishia njiani.Respond the matters with the facts na sio porojo. Ukweli wa vita hii waulizie watu wa Kagera, especially Wilaya ya Missenyi ndo watawapa ukweli wa vita hii. sio kwamba kila kitu kilikuwa disclosed na ushindi haukuja da way wanavyouongelea.
Ukwel mtupu kuna mzee alkuwa yuko mizinga uwa tunamuita mzee wa 130 (one thirty) akilewa uwa anasmulia visa vya kutisha sana, kidogo auwawe kwa mtutu na kamanda wa kikosi chake, anadai kuna siku vita imechachamaa hasa utekaji wa masaka na mbalala aliingia kwenye nyumba na kumtoa mama mjamzito sasa ikabidi wamhoji kwa muda sasa yule mama alikwerwa na hali ile ivyo akamtemea mate askari kilichofata yule mzee alimuulza yule mama unataman mtoto wa kiume au wakike, kabla ajajibu mzee alimpasua tumbo kwa sime na kumtoa mtoto kisha kumlipua kwa bomu la mkono, kitendo ambacho kilipelekea kamanda wake kumuweka sero walivofka mbalala......hatari sanaBaada ya wanajeshi kurudi vitani nyerere aliwashukuru kwa mchango wao wakulitetea taifa ila ilitoa angalizo moja Kali sanaa" YALE YOTE MLIYOFANYA AU KUYAONA NI MARUFUKU KUYAONGELEA KATIKA JAMII AU VYOMBO VYA HABARI" akatoa mabasi kwaajili ya kuwarudisha wanajeshi hao kwao.jamii ya miaka hiyo walikuwa watiifu sanaa kwa mamlaka zao tofauti na sasa kwani kuna mambo mengi sanaa ya kinyama yalifanyika vitani.1972
What do u mean hauwezi??? Kaangalie documentary za world war two uone watu wanavyofanya ambush za wanajeshi mpaka division 2 zinasagwa zote katikati ndio sembuse 2000..... Kasome vita ya winter war kati ya finland na Russia hao wanajeshi wa finland hawakuzidi laki 5 ila urusi ilikuwa na million mbili kuna wakati wanajeshi wa russia walikuwa zaidi ya division kadhaa wanazungukwa na kibrigade tu na watandikwa milimani.... Katafiti usikaririhamna unachokijua kwa taaluma yangu ndogo ya JKT watu 2000 ni kama vikosi viwili.heuwezi poteza wanajeshi wote hao kwa mara moja.kama sisi tulipoteza 2000 basi adui ni 10000
Hapo kwa Ahmed shekilango hapaeleweki vizuri ulikusudia kusema nini.VITA VYA KAGERA!Kama jinsi vilivyofahamika Vita vya Kagera (1978-1979). Vita vya Takkribani Mwaka Mmoja na Miezi Kadhaa,viliingiza Tanzania katika hali mbaya ya kiuchumi ambayo iliharibu ustawi wa Taifa letu kwa kiasi kikubwa sana!
Nisichoshe watu naomba na mie nitoe dondoo (Zilizoleteleza Vita) nilizojifunza kutokana na Vita hivi kama ifuatavyo:-
- Ni vita ambavyo Nyerere alijaribu kuviepuka kidiplomasia lakini vilishindikana kabisa; Alienda OAU akawaomba walaani vitendo vya Alhaji, Field Marshal,Black Hitler,CBE The Life President of Uganda. IDD AMIN anavyovifanya vya Uvamizi na tishio la Vita dhidi ya TZ,Mashirika mbalimbali ya kimataifa yalikaa kimya juu ya ombi la Nyerere Kuwataka Wapaze sauti isikike duniani - Aliomba tu Jumuiya za Kimataifa ZIMRAANI AMIN na UZUSHI WAKE DHIDI YA TZ.
- OCD wa Bukoba Hans Pope (Chotara wa kijerumani) aliuwa( alikuwa kwenye doria mpakani) na Maiti yake kutembezwa Kampala, na Nchi ya Uganda kutangazia kuwa Nyerere alikuwa anajiandaa na vita na tayari alishaleta Askari wa Kichina TZ.(uzushi).
- Amin alidai eneo la mto kagera ni ardhi ya Uganda.(uzushi)
- Comrade Cho Enlai (Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje ya china) alimpigia simu Nyerere akamwambia usipigane vita na Uganda;Amin amejipanga na anasubiri uingie mkenge akutandike.
- IDD AMIN alikuwa ameahidiwa siraha nzito mbalimbali na nchi kadhaa za nje (Uingereza,Urusi pamoja na Israel).
- Idd Amin alifanikiwa kupata siraha nyingi toka urusi na Libya.Hivyo Amin alikuwa amepania Kupigana Vita.
- Wakati huo Uganda ilikuwa ikitawaliwa kama DEEP STATE - Yaani Vyombo vya ulinzi na Usalama ndio vilitawala Uganda na mitaa yake.
- SRB (State Research bureau) shirika la Ujasusi la Uganda lilishika hatamu ya ushauri na uongozi wa Nchi chini ya Amin,likitesa na Kuua raia na watu waliodhaniwa kuwa ni adui wa Amin.
- Frank Terpil dalali mbaya sana aliyemtafutia Kila kitu alichokitaka Amin toka Ulaya na marekani,Huyu jamaa alikuwa kiungo kiovu katika siasa za Uganda kwa wakati ule.(siraha,magari ya kifahari na vitu vingine vya starehe).
- inasemekana Wanafunzi Saba toka UDSM waliuwawa kinyama Uganda walipokuwa wamekwenda Field Katika Shirika la Mawasiliano la Afrika Mashariki(East African telecominication headquarter ilikuwa Uganda kabla ya shirikisho kuvunjika 1977).
- Waziri Mkazi wa nchini Uganda wa TZ ndg. Ahmed Shekilango alikufa Ghafla baada tu ya kuongea na Nyerere kuhusu jambo ambalo mpaka leo hatujui ilikuwa ni nini na alitaka kuja kuonana na mwl. kumweleza nini?
- Wakati huo Milton Obote akipata hifadhi ya ukimbizi nchini Tz,Uganda ilitaka sana Obote arudishwe Uganda kwa Amini(extradition) Kitu ambacho TZ ilikataa kata kata chini ya Waziri wa mambo ya Nje Dr. John S. Malecela.Ndugu Malecela alimuapia Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Joshua W. Kibedi (shemeji wa Amin) akamwambia kuwa hata yeye anaweza kuwa mkimbizi wakati wowote ule hivyo hajui anachoomba kwa TZ,Kwani Ukimbizi ni Haki ya kiraia. Kweli baada ya miezi michache Kibedi alikimbia Uganda.
- Somalia nchini ya"Dikteta" Siad Bare alikuwa msuluhishi wa Mgogoro kati ya Uganda na Tz.
- Askofu Mkuu wa Anglican nchini Uganda auawa kinyama - Bishop Janan Luwum (inasemekana aliuwawa na Amin kwa mkono wake mwenyewe - Janan Alikemea Vitendo vya Kidikteta hadharani Amin hakupendezwa na hilo)
- Wakati chokochoko hizi zinaendelea hapa nchini mambo hayakuwa Shwari sana,jeshi letu pendwa lilikuwa Kusini mwa Tz kusaidia harakati za Ukombozi hasa Mozambique(1970s).
- Nyerere alitafakari sana akakonda mno!Aliiona Uganda inataka kuwa nchi ya Ajabu -Udikteta sio Kitu kizuri - Nyerere akaapa kwamba hataruhusu Uganda Martyr (historia inaeleza vizuri sana juu ya hili)Ingine itokee Uganda akafunga kwa maombi kanisani siku tatu,akainuka na Maneno - NIA,UWEZO NA SABABU.
- Tanzania ikaingia Vitani rasmi Mwaka 1978 ( Inasemekana ni kwa taarifa za Kijasusi zilizokusanywa na Mashushushu wetu huko na kwa Maelezo binafsi ya baadhi ya Maaskari wa JW waliomjua Amin vizuri(General Msuguli).
- Vita ni Vita tu - casultes of war huwa hazitamaniki kabisa sio kwa upande wowote ule.
- Inasemekana takriban US Dollars 508,000/- zilipotea kutokana na Vita hivyo! ni Zaidi ya hela ambazo hata wafadhili wa nje wasingeweza kutupa sisi kirahisi rahisi.
- Idadi ya waliopoteza maisha(Askari) Vyanzo nilivyopitia vinadai si chini ya Askari 300.
- Baadhi ya Makanda waliotutoa Kimasomaso ni Lt.Col. Ben Msuya (Huyu Jamaa hakuna askari hata mmoja aliyekufa kwenye Battalion yake) Alipokuwa Uganda alivaa Rain boot Nyeupe na Mkuki - aliongoza kuteka kituo cha redio Uganda.
- Abdalla Twalipo,Yusuph Himid,Herman Lupogo,Shimani,Roland Chacha,Major Musuguli,Tumainel Kiwelu,Mirisho Sarakikya,Walden,Marwa,Silas Mayunga,James Luhanga na wengineo wengi.
War may sometimes be a necessary evil. But no matter how necessary, it is always an evil, never a good. We will not learn how to live together in peace by killing each other's children.- Jimmy Carter.
- Natunaimini nimeleza kidogo na mimi hapo.Asante
Mkuu hapa umeandika uongo mkuu yani kweli askari wa mikoa 3 mikubwa hivyo haizidi 2000Askari 2000? Yaani askari wote walioko Arusha na Tanga jumlisha na walioko Dar na Pwani. Hizo ndio Battalion mbili. Hakuna Jeshi litasimama ukitokea msiba mzito namna hiyo. Hapo ina maana kila kitu kilinyang'anywa na majeshi ya Amini na tayari waliukalia mji wa Bukoba, Arusha na Dar. Kweli za kuambiwa changanya na zako.
AISEEE KUMBE KUNA MENGI WANAFICHA KUHUSU VITA HII???!!!INAWEZEKANA HATA USHINDI HAUKUWA WA KISHINDO KAMA TUNAVYOAMINISHWA
Mkuu iwapo kuna taarifa haijakaa sawa unaweza ukaongezea maarifa hapo! Nashukuru kwa kujali kwako.Ha
Hapo kwa Ahmed shekilango hapaeleweki vizuri ulikusudia kusema nini.
Shekilango,waziri mdogo na mbunge wa zamani wa Korogwe alianguka na ndege alipokuwa akija nchini kutoka Uganda,ile barabara pale Sinza imetajwa kwa heshima yakeHa
Hapo kwa Ahmed shekilango hapaeleweki vizuri ulikusudia kusema nini.
Asante sana je alidondokea ug au tz naona kama kuna suspicion ya kifo chakeShekilango,waziri mdogo na mbunge wa zamani wa Korogwe alianguka na ndege alipokuwa akija nchini kutoka Uganda,ile barabara pale Sinza imetajwa kwa heshima yake
Hujui kitu nyamaza nenda kanyonye maziwa ya mama yako bado kinda sana wewe!!bahati yetu vita hii tukaipigana wakati ambapo tulikuwa na umoja wa kitaifa pamoja na Kiongozi mzalendo, vijana wa tarime na maeneo mengine waliona ufahari kwenda kufa kwa ajili ya nchi yao, ila ingekuwa ni leo!! kuna mikoa asingejitokeza kijana hata mmoja.
J. K NYERERE alikuwa kiongozi mbarikiwa, alikuwa na kitu cha ziada ndani yake.
Ndio maana nasema wachangiaji wengi humu walikuwa hawajazaliwa.Jonh Bolton Walden alistaafu akiwa na cheo cha major General alikuwa mtanzania chotara wa Scotland mama yake alikuwa mnyakyusa.Mungu ailaze pema roho yake na mashujaa wengine waliotangulia mbele za hakiSoma au fuatilia vizuri historia ya luteni enzi hizo japo alistaafu akiwa na cheo cha meja bila Shaka aliitwa John Walden afu pia hilo tukio Amin alilitegemea na njia yao ya kupita aliijua lakini ukumbuke kwamba waliotangulizwa walikuwa ni wale wazalendo wa nchi yao waliojitolea tu na wakapata mafunzo ya muda mfupi Sana tuseme walikuwa migambo
Natamani kuendelea kukufahamisha ila nahisi usingizi hivi (kifupi hao waliotangulia hawakuwa na mbinu za kivita za mm au km
Na lengo la amiri jeshi mkuu lilikuwa ni kuona adui yake (Amin) amejipanga vipi yuko wapi na kashika njia gani ukumbuke muda huo bado ujenzi wa daraja liliovunjwa kagera lilikuwa linaendelea kujengwa.unadhani bila hiyo mbinu lazima nduli angewafuata pale wasifanikishe azima yao
Ngoja nilale endeleeni kubisha
Sio mjinga, hisia yake inaweza kua na ukweli .Mjinga kabisa
Hapo ndipo makao makuu ya TISS ? .wengine hatujafika DAR tunaskia tu hiyo sehemu mnaitaja humu sanaNatamani kuona picha halisi za pale ngome upanga za enzi hizo za vita palikuwaje?
Yani heka heka za pale Maliki street diamond jubilee na palm beach zilikuwaje kwa picha halisi
Kweli upanga ya zamani duh
Muda siyo mrefu watasema hata hiyo vita ilikuwa ya kutengenezwa sababu tanzania ilikuwa inajifanya kiburi sana, hapo tu nipowapendea CIA. hawajui kukaa na siri.