Masamila
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 6,490
- 7,422
Askari 2000? Yaani askari wote walioko Arusha na Tanga jumlisha na walioko Dar na Pwani. Hizo ndio Battalion mbili. Hakuna Jeshi litasimama ukitokea msiba mzito namna hiyo. Hapo ina maana kila kitu kilinyang'anywa na majeshi ya Amini na tayari waliukalia mji wa Bukoba, Arusha na Dar. Kweli za kuambiwa changanya na zako.
Umekosea sana. Kipindi cha utawala wa JK Nyerere JWTZ lilikuwa na wanajeshi elfu thelathini, kadiria sasa ni miaka zaidi ya thelathini baada ya JK Nyerere kuondoka madarakani JWTZ litakuwa na wanajeshi wangapi.
Umetaja mikoa minne ambayo inajulikana kabisa kuna Brigade mbili kabisa katika mikoa hiyo, Brigade ya Kanda ya kaskazini yenye makao yake makuu Arusha na Brigade ya kanda ya mashariki yenye makao yake makuu pale Lugalo.
Na Brigade huwa haiwi na askari wachache hivyo , 2000?!!
Brigade zinazokuwaga na askari wachache hivyo huwa ni task organization na kutokana na umuhimu wa task hizo na ukubwa au idadi ya wanajeshi wanaofanya task hizo ndio zinapelekea organizational formation hizo kuitwa Brigade.