Wanajeshi wa Tanzania takribani 2000 walifyekwa na majeshi ya Idd Amin; huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya Kagera

Wanajeshi wa Tanzania takribani 2000 walifyekwa na majeshi ya Idd Amin; huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya Kagera

Askari 2000? Yaani askari wote walioko Arusha na Tanga jumlisha na walioko Dar na Pwani. Hizo ndio Battalion mbili. Hakuna Jeshi litasimama ukitokea msiba mzito namna hiyo. Hapo ina maana kila kitu kilinyang'anywa na majeshi ya Amini na tayari waliukalia mji wa Bukoba, Arusha na Dar. Kweli za kuambiwa changanya na zako.


Umekosea sana. Kipindi cha utawala wa JK Nyerere JWTZ lilikuwa na wanajeshi elfu thelathini, kadiria sasa ni miaka zaidi ya thelathini baada ya JK Nyerere kuondoka madarakani JWTZ litakuwa na wanajeshi wangapi.

Umetaja mikoa minne ambayo inajulikana kabisa kuna Brigade mbili kabisa katika mikoa hiyo, Brigade ya Kanda ya kaskazini yenye makao yake makuu Arusha na Brigade ya kanda ya mashariki yenye makao yake makuu pale Lugalo.

Na Brigade huwa haiwi na askari wachache hivyo , 2000?!!

Brigade zinazokuwaga na askari wachache hivyo huwa ni task organization na kutokana na umuhimu wa task hizo na ukubwa au idadi ya wanajeshi wanaofanya task hizo ndio zinapelekea organizational formation hizo kuitwa Brigade.
 
Niliwah kusimuliwa na mzee wa enzi izo kuwa , Msumbiji "walituazima" wanajeshi zaidi ya 1000 tena wenye weledi wa hari ya juu kwa kipindi icho.
Pia eti wapiga mizinga ya umbali mrefu walitoka Msumbiji na mizinga yao.
 
Madhara makubwa ya mwanzo ilikuwa ni Police na kikosi kidogo cha JWTZ mpakani. Hawa hawakuwa na vifaa kuweza kuhimili uvamizi ule lakini walipambana hadi tone lao la mwisho la damu. Msaada uliopelekwa pia ukawa dhaifu kichapo kikaendelea. Madhara zaidi pia ilisababishwa na kupelekwa kwa vikosi vya JKT na mgambo ambavyo vilikutana na vipigo pia hadi pale nchi ilipoamua kujipanga na mpango kamili kutoka Ngome ndio ulioamua vita iweje na mwisho Idd Amin kukutana na kichapo cha mbwa koko.
 
bahati yetu vita hii tukaipigana wakati ambapo tulikuwa na umoja wa kitaifa pamoja na Kiongozi mzalendo, vijana wa tarime na maeneo mengine waliona ufahari kwenda kufa kwa ajili ya nchi yao, ila ingekuwa ni leo!! kuna mikoa asingejitokeza kijana hata mmoja.

J. K NYERERE alikuwa kiongozi mbarikiwa, alikuwa na kitu cha ziada ndani yake.

Ushaleta ujinga wako. Maneno tu matendo null. Utakuwa Chadema wewe sasa unataka kuprove jambo
 
Ushaleta ujinga wako. Maneno tu matendo null. Utakuwa Chadema wewe sasa unataka kuprove jambo

shule ulienda kusomea matango pori!!

kwahiyo mtu akileta hoja usiyoipenda unamuita chadema?

hivi unajua kuwa kuna watanzania wengi hawafungamani na vyama vyovyote?
 
Habari kwenu jukwaani.

Kuna simuluzi BBC Radio wanatujuza historia iliyofichwa. Mwanzoni mwa vita vya Kagera ni kuwa baada ya Amini kufanya uvamizi wake, Tanzania ilitanguliza kikosi cha wanajeshi 2000 mstari wa mbele na chote kilifyekwa na majeshi ya Amin.

Baada ya hapo jeshi letu lilijipanga upya na kusonga mbele hadi Kampala na Jinja ambapo Idd Amin alitimkia Libya na baadae Saudi Arabia.

Hii historia sijiwahi kuisikia, nilijua tulipigana bila upinzani mkali na hatukupoteza askari wengi kiasi hiki kwa mpigo mmoja.

Msimuliaji pia anadai jeshi la Uganda lilikuwa limegawanyika sana kwani baadhi hawakumtaka Amin aendelee kuongoza Uganda na hivyo kulisaidia jeshi letu lililojipanga upya kushinda vita hivyo.

Viva JWTZ.
habari yako haina Source hivyo hiyo ni habari ya kwenye vibanda vya kahawa!!
 
habari yako haina Source hivyo hiyo ni habari ya kwenye vibanda vya kahawa!!
Ametaja BBC radio hapo mwanzo

Ingawa nimewahi kusoma bandiko lako kuhusu Kagera War nadhani ndio lilibeba MAUDHUI ya kweli na halisi hebu Fanya kulirudisha Vijana wajifunze history ya nchi kdg
 
AISEEE KUMBE KUNA MENGI WANAFICHA KUHUSU VITA HII???!!!INAWEZEKANA HATA USHINDI HAUKUWA WA KISHINDO KAMA TUNAVYOAMINISHWA
Vita ni propaganda, tena sisi tuliichokoza Uganda kwa kuwapa hifadhi waasi wa FRONASA chini ya Yoweri Museven.
 
Acha waseme hao 2000 maadam kijijini kwetu walienda vijana 8 na wakarudi wote, nakumbuka tulikuwa tunafanya sherehe na kuwapongeza kama mashujaa kwa nyimbo hao wa vijiji hewa watu hewa 2000 wafe tu. Ili mradi TULIMPIGA na juzi nikiwa Kampala niliposena mTz walifurahi sana nikawa lulu kwa wadada wa kiganda,walimpenda JpM sana
 
Acha waseme hao 2000 maadam kijijini kwetu walienda vijana 8 na wakarudi wote, nakumbuka tulikuwa tunafanya sherehe na kuwapongeza kama mashujaa kwa nyimbo hao wa vijiji hewa watu hewa 2000 wafe tu. Ili mradi TULIMPIGA na juzi nikiwa Kampala niliposena mTz walifurahi sana nikawa lulu kwa wadada wa kiganda,walimpenda JpM sana
Mkuu ilikuwa mwanzo wa vita hiyo.
 
2000 tu ??? Walikufa zaidi ya 2000 , wengi walikufa kwa kupapatikia wanawake wasijue ulikuwa ni mtego kwao
 
Walikufa wanajeshi Wengi sijui idadi..
Ndo maana kulikuwa na vita mbili
Ya mwaka 1978 ndo tulishindwa wakafa Wengi...tukaenda kujipanga mwaka 1979 ndo tukarudi tena..
Inasemekana tukipeleka Sana mgambo mstari wa mbele...

Uganda walikuwa na silaha Kali sana only wanajeshi wao Wengi walikuwa hawana morali....Sisi tulikuja kukopa hela nyingi tukanunua silaha Kali baadae mwaka 1979 ndo tukaenda kushinda
 
Back
Top Bottom