Ninyi Vijana acheni kudanganywa! Hata ukisoma vitabu vilivyoandikwa Kuhusu vita ya Uganda, takwimu kama Hizo hazimo. Aidha Ukienda pale Kaboya kwenye makaburi walipozikwa wanajeshi waliokufa vitani Uganda, takwimu Hizo hazipo. Wanajeshi waliokumbwa na uvamizi ule, maili 10 kutoka mpaka wa Mutukula walikuwa detachment Moja na troop Moja. Hawatimii hata watu 100. Aidha kutokana na ukubwa wa kikosi Cha Amin kilichovamia, askari wetu hao waliwahi kupata Taarifa za uvamizi na wakawahi kuondoka Kisha kuvuka Mto Kagera na kuja maeneo ya Kasambya Mashariki ya Daraja la mto Kagera kabla ya kuvunjwa daraja Hilo.
Yawezekana Watz waliouawa kwenye vita Ile kuwa wengi ukijumlisha na Raia Ambao waliuliwa na askari wa Amini kuanzia Mpakani Mutukula Hadi kwenye daraja. Maana raia wengi wa maeneo hayo walijua waliokuwa wakifuatwa ni askari na sio raia. Kwahiyo wengi waliuawa. Maiti za raia wengi zimeonyeshwa katika vitabu kadha vinavyosimulia vita hiyo na siyo Askari.
Halafu wanasema kuwa Magambo na askari wa majeshi mengine waliokuwa mobilized ndio waliuawa, siyo Kweli. Kwani askari hao walichanganywa vyema na askari wa JW na ilikuwa vigumu kuwatofautisha. Nakumbuka ni Brigedi Moja TU ambayo ilikuwa na mchanganyiko mkubwa wa mgambo Ndiyo ilipata matatizo pale Lukaya, napo ni BAADA ya kukabiliana na askari walioingia vitani kutoka Libya na walikuwa na silaha nzito. Kwa ushujaa mkubwa silaha zote Hizo na askari wa Libya walitekwa, kutokana na umakini wa mbinu za Jeshi Letu! Pia tunaambiwa askari waliouawa kwenye actual war hawakufika100. Ila wengi waliouawa Uganda ni baada ya vita. Wengi waliuawa kwenye starehe, ajali, sumu, nk.
Ujue wanajeshi 2000 kuuawa vitani ni karibia Brigade nzima. Ingetokea hivyo vita Ile ingechukua muda mrefu sana! Lakini nakumbuka ilikuwa rahisi kwasababu ndegevita zote za Uganda ziliteketezwa kabla majeshi yetu hayajavuka daraja la Kagera. Zote zolitunguliwa Kila zilipotumwa kuja kushambulia daraja au kufanya uchunguzi. Hii ilitokana na silaha makini za kuangusha ndege wakati ule. Aidha vifaru vingi vya adui vilifutwa kabla ya kufika Lukaya na Mpigi, miji ya mwisho kabla kuingia Kampala. Nakumbuka kifaru chetu kimoja ndicho kiliteketezwa wakati tunavuka daraja la Karuma Falls karibu na njiapanda za kwenda Arua, Lang'o na Gulu.
Kwahiyo kitendo Cha kuangamiza ndege vita na vifaru vyao mapema, ilikuwa lift tosha ya kuikamilisha Ops Chakaza Kwa urahisi kabisa.
Kwahiyo Vijana hebu jaribuni kufanya tafiti mnaposikia mambo mazito kama haya, kabla hamjaandika humu. Hata ku Google mnashindwa?