Wanajeshi wa Urusi wawaita Wanajeshi wa Afrika "Takataka" wakiwa wote vitani Ukrein

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Moja ya jambo linalotembea mtandaoni ni video inayoonesha Wanajeshi wa Kirusi waliokuwa vitani Ukreni wakiwa wameketi na Wanajeshi wa Afrika, Porini katika baridi kali. Huku Wanajeshi hao wa Kiafrika wakiwa wanaimba nyimbo za Kiswahili zenye kiitikio cha "Moto unawaka" ambacho ni kiashiria kuwa wanatoka katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wengine wakidai hao ni Watanzania, wengine wakisema hao ni Wakenya. Lakini wengine wanasema wakenya wamefungana na Wamarekani sana, ni ngumu Wanajeshi wao kujiunga na Warusi wakati Marekani iko upande wa Ukrein.

Tanzania kwa ukanda huu ndio nchi inayofungamana na Urusi kiitikadi hasa Ujamaa. Na Kiswahili kwenye hiyo nyimbo ni cha kitanzania zaidi, hata rafudhi ukisikia.

Video hii imehudhunisha Waafrika wengi baada ya Mrusi mmoja akisikika akisema kwa Kirusi badae kutafsiri kwa Kiingereza kuwa Wanajeshi hao wa Kiafrika ni Disposable, neno linalotafsirika kama Takataka au kitu cha kutumiwa na kutupwa.

Inaonekana kuwa Waafrika hao ndio watakuwa mstari wa mbele (Frontline) kwenye mapambano hayo, huku warusi wakija kwa nyuma.

Kama huko Kwao wakuu wao wanaingiziwa bilioni chap bila sababu ya yeye anauwezo wa kwenda kuitafuta yake ya kihalali anaachaje? Wajanja wengi wamekimbia shithole countries
 
Are you mbupu? Siku nyingine andika vitu vinavyoeleweka... ukishindwa kaa kimya
Acha umbea kwenye kaz za watu hao mafata pesa umbea wako hautasaidia kitu

Kikubwa wanafanya kaz na wanalipwa inatosha,we endelea kula ugali Kwa shemej
 
Majeshi wote wanao pelekwa mbele kupigana ni takataka tu, haijaalishi wa nchi ipi. Sababu vita vingi anae nufaika ni Watawala na Banker’s kwa watakacho vuna huko walipo kuteka.

Mfano mdogo angalia vita vya Tanzania na Uganda au vya Congo kule au vya Iraq na Afghanistan majeshi wengi wao wamepata vilema na kuwa homeless tu.
 
Moja ya jambo linalotembea mtandaoni ni video inayoonesha Wanajeshi wa Kirusi waliokuwa vitani Ukreni wakiwa wameketi na Wanajeshi wa Afrika, Porini katika baridi kali. Huku Wanajeshi hao wa Kiafrika wakiwa wanaimba nyimbo za Kiswahili zenye kiitikio cha "Moto unawaka" ambacho ni kiashiria kuwa wanatoka katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wengine wakidai hao ni Watanzania, wengine wakisema hao ni Wakenya. Lakini wengine wanasema wakenya wamefungana na Wamarekani sana, ni ngumu Wanajeshi wao kujiunga na Warusi wakati Marekani iko upande wa Ukrein.

Tanzania kwa ukanda huu ndio nchi inayofungamana na Urusi kiitikadi hasa Ujamaa. Na Kiswahili kwenye hiyo nyimbo ni cha kitanzania zaidi, hata rafudhi ukisikia.

Video hii imehudhunisha Waafrika wengi baada ya Mrusi mmoja akisikika akisema kwa Kirusi badae kutafsiri kwa Kiingereza kuwa Wanajeshi hao wa Kiafrika ni Disposable, neno linalotafsirika kama Takataka au kitu cha kutumiwa na kutupwa.

Inaonekana kuwa Waafrika hao ndio watakuwa mstari wa mbele (Frontline) kwenye mapambano hayo, huku warusi wakija kwa nyuma.

Napataje hii nafasi?
 
Propaganda
Propaganda ya nani sasa.... kama huamini fanya transcript upate text, kisha uitafsiri kwa Kiingereza, mimi nimefanya transcription kisha nikaitafsiri kwa Kiingereza kutoka Kirusi nikaona kweli jamaa anawaita Takataka za kutupa "Disposable"
 
Back
Top Bottom