Moja ya jambo linalotembea mtandaoni ni video inayoonesha Wanajeshi wa Kirusi waliokuwa vitani Ukreni wakiwa wameketi na Wanajeshi wa Afrika, Porini katika baridi kali. Huku Wanajeshi hao wa Kiafrika wakiwa wanaimba nyimbo za Kiswahili zenye kiitikio cha "Moto unawaka" ambacho ni kiashiria kuwa wanatoka katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Wengine wakidai hao ni Watanzania, wengine wakisema hao ni Wakenya. Lakini wengine wanasema wakenya wamefungana na Wamarekani sana, ni ngumu Wanajeshi wao kujiunga na Warusi wakati Marekani iko upande wa Ukrein.
Tanzania kwa ukanda huu ndio nchi inayofungamana na Urusi kiitikadi hasa Ujamaa. Na Kiswahili kwenye hiyo nyimbo ni cha kitanzania zaidi, hata rafudhi ukisikia.
Video hii imehudhunisha Waafrika wengi baada ya Mrusi mmoja akisikika akisema kwa Kirusi badae kutafsiri kwa Kiingereza kuwa Wanajeshi hao wa Kiafrika ni Disposable, neno linalotafsirika kama Takataka au kitu cha kutumiwa na kutupwa.
Inaonekana kuwa Waafrika hao ndio watakuwa mstari wa mbele (Frontline) kwenye mapambano hayo, huku warusi wakija kwa nyuma.