Narumu kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 1,888
- 4,489
Maafisa wawili wa Iran waliuawa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran; wote wawili walikuwa askari wa jeshi la Iran, sio Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Tofauti na IRGC, jeshi la Iran - linalojulikana kama Artesh - kwa ujumla haliogopi wala kuchukiwa na Wairan wengi, kwani jukumu lake ni kulinda mipaka ya Iran.
Walinzi wa Mapinduzi, hata hivyo, wana jukumu kubwa katika masuala ya kisiasa na kiuchumi ya Iran, ambayo ni zaidi ya kazi za kijeshi.
Wanashiriki kikamilifu katika operesheni za nje ya nchi kuanzia Yemen hadi Levant, inayopakana na Israel, na walikabiliana vikali na maandamano ya kitaifa katika miaka ya hivi karibuni.
Chanzo cha picha,Hamshahri Newspaper
Maelezo ya picha,Mohammad Mehdi Shahrokhifar alikuwa mmoja wa maafisa wawili wa jeshi la Iran waliouawa katika mashambulizi ya Israel.
IRGC ina nguvu kubwa ndani ya Iran, na wanachama wanachukua majukumu yenye ushawishi katika serikali.
Wamejikita zaidi katika miradi mikubwa ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na miradi ya mafuta na gesi hadi ujenzi wa barabara, jambo ambalo limechochea malalamiko ya umma dhidi yao baada ya kubainika kuwa wanaendekeza rushwa na ukiritimba wa rasilimali.
Chanzo cha picha,Hamshahri Newspaper
Maelezo ya picha,Meja Hamzeh Jahandideh wa Jeshi la Iran pia aliuawa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran
Bbc