USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 10,904
- 26,184
Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari kuwa askari walinda amani wa MONISCO waliokamatwa siku ya jumapili ni kutoka Tanzania, wamekamatwa kupisha uchunguzi wa mauaji ya waandamanaji raia wa Congo.
Tangu kuzuka kwa maandamano ya kupinga walinda amani nchini DRC askari watano wameuwa, waliouwawa ni wahindi wawili, wamoroco wawili na moja aliuwawa peke yako na utaifa wake haukawekwa wazi ambao wote hawajafanya kazi zaidia ya miezi sita.
Maandamanaji wamekuwa wakivamia kambi za askari walinda amani wakishinikiza waondoke kwa kuwa wameshindwa kuleta amani kwa miaka kadhaa huku hali ikizidi kudhorota mashariki mwa Congo.
========
Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kwamba walinda amani waliokamatwa siku ya Jumapili kwa kuwapiga risasi watu wawili hadi kufa katika mpaka kati ya Congo na Uganda walikuwa wanatoka Tanzania.
Haya ni kwa mujibu wa, Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa MONUSCO, Khassim Diagne, aliyezungumza na BBC
Umoja wa Mataifa umeshtumu vikali shambulio hilo ambapo watu 15 walijeruhiwa .
Katika kipindi cha juma moja lililopita takriban watu 20 wamefariki katika maandamano ya ghasiadhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaojulikana kama MONUSCO .
Raia wengi wa DR Congo wamewashtumu walinda amani hao kwa kushindwa kuwalinda raia kutokana na mashambulizi yanayotekelezwa na waasi.
Huku shambulizi hilo la siku ya Jumapili likitarajiwa kuliharibia sifa jeshi hilo la Umoja wa mataifa , wanahabari wanasema vurugu zimejitokeza kutokana na kile wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaona kushindwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusitisha mashambulizi ya makundi yenye silaha katika eneo hilo na kusababisha maandamano makali wiki iliyopita.
Waandamanaji hao walishambulia kambi mbili za Umoja wa Mataifa huko Goma na Butembo, ambapo walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa waliuawa.
Walinda amani wawili kati ya hao walikuwa raia wa Morocco na wengine wawili walikuwa Wahindi, wote walikuwa wamefanya kazi nchini DR Congo kwa Umoja wa Mataifa kwa muda wa chini ya miezi sita - huku mmoja wa waliouawa akiwa amekaa kwa miezi miwili na siku 22 pekee.
Mwezi Juni vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa viliondoka katika jimbo tofauti la mashariki - Tanganyika - baada ya kile walichokieleza kuwa kuimarika kwa hali ya usalama.
Chanzo: BBC