Wanajeshi wawili wa Tanzania washikiliwa DRC kupisha uchunguzi wa mauaji ya raia

Mbona huyo Mkuu wenu wa Intelligence yenu, Trainer Mmoja wa Chuo chao Mbweni ( sasa Mstaafu ) na 45% ya Watendaji wake ( wao ) wananijua in and out GENTAMYCINE na muda wowote tu Wakinihitaji wananipata?
 
Askari wa Tanzania wamezoea kuonea raia.
 
Agosti 2022
SHARED
Walinda amani waliowapiga raia 2 risasi na kuwauwa DRC ni Watanzania

AFPCopyright: AFP
Walinda amani wa MonuscoImage caption: Walinda amani wa Monusco
Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kwamba walinda amani waliokamatwa siku ya Jumapili kwa kuwapiga risasi watu wawili hadi kufa katika mpaka kati ya Congo na Uganda walikuwa wanatoka Tanzania.

Haya ni kwa mujibu wa, Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa MONUSCO, Khassim Diagne, aliyezungumza na BBC

Umoja wa Mataifa umeshtumu vikali shambulio hilo ambapo watu 15 walijeruhiwa .

Katika kipindi cha juma moja lililopita takriban watu 20 wamefariki katika maandamano ya ghasiadhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaojulikana kama MONUSCO .

Raia wengi wa DR Congo wamewashtumu walinda amani hao kwa kushindwa kuwalinda raia kutokana na mashambulizi yanayotekelezwa na waasi.

Huku shambulizi hilo la siku ya Jumapili likitarajiwa kuliharibia sifa jeshi hilo la Umoja wa mataifa , wanahabari wanasema vurugu zimejitokeza kutokana na kile wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaona kushindwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusitisha mashambulizi ya makundi yenye silaha katika eneo hilo na kusababisha maandamano makali wiki iliyopita.

Waandamanaji hao walishambulia kambi mbili za Umoja wa Mataifa huko Goma na Butembo, ambapo walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa waliuawa.

Walinda amani wawili kati ya hao walikuwa raia wa Morocco na wengine wawili walikuwa Wahindi, wote walikuwa wamefanya kazi nchini DR Congo kwa Umoja wa Mataifa kwa muda wa chini ya miezi sita - huku mmoja wa waliouawa akiwa amekaa kwa miezi miwili na siku 22 pekee.

Mwezi Juni vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa viliondoka katika jimbo tofauti la mashariki - Tanganyika - baada ya kile walichokieleza kuwa kuimarika kwa hali ya usalama.

Article share tools

HAO RAIA KUMBE nao WALISHAUA ASKARI wanne wa UN , tena waliwavamia kambini, Sasa watu Kama hao usipojihami kwa silaha siwanakuua!?
 
Walinda amani waliowapiga raia 2 risasi na kuwauwa DRC ni Watanzania​

AFPCopyright: AFP
Walinda amani wa MonuscoImage caption: Walinda amani wa Monusco
Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kwamba walinda amani waliokamatwa siku ya Jumapili kwa kuwapiga risasi watu wawili hadi kufa katika mpaka kati ya Congo na Uganda walikuwa wanatoka Tanzania.
Haya ni kwa mujibu wa, Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa MONUSCO, Khassim Diagne, aliyezungumza na BBC
Umoja wa Mataifa umeshtumu vikali shambulio hilo ambapo watu 15 walijeruhiwa .
Katika kipindi cha juma moja lililopita takriban watu 20 wamefariki katika maandamano ya ghasiadhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaojulikana kama MONUSCO .
Raia wengi wa DR Congo wamewashtumu walinda amani hao kwa kushindwa kuwalinda raia kutokana na mashambulizi yanayotekelezwa na waasi.
Huku shambulizi hilo la siku ya Jumapili likitarajiwa kuliharibia sifa jeshi hilo la Umoja wa mataifa , wanahabari wanasema vurugu zimejitokeza kutokana na kile wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaona kushindwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusitisha mashambulizi ya makundi yenye silaha katika eneo hilo na kusababisha maandamano makali wiki iliyopita.
Waandamanaji hao walishambulia kambi mbili za Umoja wa Mataifa huko Goma na Butembo, ambapo walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa waliuawa.
Walinda amani wawili kati ya hao walikuwa raia wa Morocco na wengine wawili walikuwa Wahindi, wote walikuwa wamefanya kazi nchini DR Congo kwa Umoja wa Mataifa kwa muda wa chini ya miezi sita - huku mmoja wa waliouawa akiwa amekaa kwa miezi miwili na siku 22 pekee.
Mwezi Juni vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa viliondoka katika jimbo tofauti la mashariki - Tanganyika - baada ya kile walichokieleza kuwa kuimarika kwa hali ya usalama
 
Labda
Lkn si kwa wanajeshi maana hapa TZ hawana historia hiyo
 
tulisema toka mwanzo, askari vijana wetu kutoka JWTZ waji toe kwenye hicho kikosi cha MONUSCO, wacongoman hawana shukrani kabisa, wanajeshi wetu wawaachie wacongoman wapambane wenyewe na PK na vikosi vyake ndani ya DRC. na hata wakizidiwa tusiwasaidie ..................................
 
Kuna fungu kubwa wanapewa so hata nafasi zenyewe mpaka walogane kuzipata upo hapo
 
Chanzo ni sisi waafrika wenyewe kwasababu ya ujinga wetu.Ukinga wetu ni lundo ndo maana unatoa mwanya kwa mataifa mengine majanja kututumia kwa manufaa yao.
 
Tatizo serikali zinazotoa wanajeshi kwenda huko zinapokea mipunga na hao wanajeshi wanalipwa ndo maana wanapenda kwenda.
Ila kwa akili zangu ningewaacha wacongo wadundane mpaka AKILI zitakapokuja kuwarudia kuwa amani ya nchi yao italetwa na wao wenyewe
 
..Ni kweli askari wa Tz wameua raia huko DRC.

..Uchunguzi umeanzishwa ili kujua chanzo cha tukio hilo.

..Kilichotokea na kinachoendelea kutokea ni changamoto za ukosefu wa amani ktk eneo la Mashariki ya DRC.

..Kuna askari wa UN toka India, na Morocco, wameuawa ktk ghasia na maandamano yaliyoibuka hivi karibuni.

..Tanzania ktk nyakati tofauti tumepoteza askari wetu waliokwenda DRC kusaidia kurejesha amani nchini humo.

..Sidhani kama kuondoa askari wetu DRC ni jambo la busara.

..Ni jambo la hatari kuyaacha makundi ya waasi, na magenge yenye silaha, yashike hatamu DRC.

..Jitihada kubwa zaidi zinatakiwa kufanyika ili kurejesha amani na utulivu mashariki ya DRC.
 
I have a brother yuko Congo kwenye MONUSCO baada ya hilo tukio at first ilisemekana ni waganda nkawasiliana nae jana kumuuliza akasema askar walioua raia ni WaTz na nikabahatika kuona video ya tukio. Tusipende kuwalaumu ndugu zetu embu tuwaombeeni jaman
 
..Congo inaweza kusambaratika ikawa kama Somalia.

..Na tukifika huko majirani wa DRC, ikiwemo Tanzania, tutakuwa wa kwanza kuathirika kiusalama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…