WanaJF tunaomuunga mkono Lissu sasa ni muda muafaka wa kumsaidia Lissu ashinde!

Hii imekaa vibaya
 
Ushindikwa JPM hauepukiki kila niliyemwambia ampigie kura JPM ameniambia inyeshe mvua liwake jua kura ni kwa JPM.

Watu wanataka MAENDELEO na watamchagua JPM OCTOBER 28TH ili wapate MAENDELEO.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Hamjali maendeleo ya watanzania bali maendeleo ya tanzania
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
Kusema kweli mwaka huu wapinzani ni dhaifu kuliko wakati wowote ule
Lkini hali ni tofauti kwa wapiga kura safari hii wapiga kura wako imara kuliko wakati wowote ule
 
Sasa haya yote ya nini maana tushasema ccm imechokwa na tunaona nyomi kwenye mikutano ya Lissu tena bila kuwepo wasanii.
 
Kweli kabisa umenena mkuu! Tena mie nawaomba tuisaidiane pia kuitafta ile plan ya vita ya CCM, Nakumbuka baada ya kura za maoni za ccm kuna wanaccm waliohujumiwa na kuondolewa walituahidi kutuuzia ramani ya vita ya chama chao, huu ndo wakati mzuri wa biashara hiyo. Pamoja na kumpigia kura LIssu pia Tuleteeni bidhaa hiyo ndugu zetu wanaccm wapenda mabadiliko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…