WanaJF wafuatao wanastahili tuzo ya uvumilivu kwa kutoyumbishwa na mashambulizi kila wanapopost nyuzi zao

WanaJF wafuatao wanastahili tuzo ya uvumilivu kwa kutoyumbishwa na mashambulizi kila wanapopost nyuzi zao

Matongee,
Hapo chini nimeweka video inayoeleza historia ya kuandikia historia ya TANU.

Tafadhali itazame.

Nimekunyamazia kuhusu suala la ''Udini,'' naamini unakusidia Uislam.

Ukweli ni kuwa mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika hauna mfano.

Hupendi historia hii ielezwe.

Ikielezwa ni udini ila kuifuta katika historia ya Tanganyika huo si udini.

Nakushauri fungua uzi kuhusu hili suala la udini In Shaa Allah nitakuja kuchangia kwa ushahidi wa nyaraka na picha na utawaona sana akina Sykes kuanzia 1924 hadi uhuru unapatikana 1961.

Nyaraka na picha hizi hujapata kuziona popote kama ambavyo haya nielezayo katika video hujayasikia popote.

Unachotakiwa kujiuliza nisemayo ni kweli au si kweli?:

View: https://youtu.be/bgiP_SI0-vI

Dini hizi zimepotosha wengi,Mzee Mohamed muamini mungu inatosha,au karibu kuwa pagan.
 
Tofauti kabisa na kina Malisa GJ, Maria Sarungi au Martin Maranja ambao hawana kabisa uvumilivu kwa yeyote atakayekuwa kinyume na mawazo yao hawa wanaJF wanapaswa kutunukiwa tuzo za uvumilivu kwa kutojali mashambulizi ya watu pale wanapopost nyuzi.

1. ERYTHROCYTE
Huyu mfuasi kindakindaki wa chama cha Mbowe ni mfano wa kuigwa kwenye ulimwengu wa demokrasia. Huyu ni mtu aliyekula kiapo cha utiifu kwa mwenyekiti wa chama chake kiasi kwamba post zake nyingi huwa ni kumsifu chairman. WanaCCM wamekuwa wakimwandama kwa hoja na baadhi kutumia lugha za kuudhi ila huyu mfuasi wa Mbowe hajawahi rudi nyuma.

2. BIBI FAIZA FOXY
Bibi yetu ambaye inasemekana ndo alikuwa Slayqueen wa enzi za TANU, yaani nchi inapata uhuru yeye tayari kashakula nauli za wakoloni kadhaa.. sio poa. Ni bibi mahiri sana kwenye hoja zake ila wananchi wengi hukwazwa sana na chembechembe za udini alizo nazo. Mwisho wa siku bibi Faiza ni mtu asiyetishwa na maneno ya kumkatisha tamaa kwenye anachoamini.

3. MZEE PASCAL MAYALLA.
Mzee wetu ni muumini mzuri wa sheria ya KARMA. Huamini kabisa hakuna baya utakalofanya halafu karma isitimize wajibu wake wa kukuadhibu. Ila huwa najiuliza KARMA huwa inasahau anwani ya CCM au huwa inakumbuka ila CCM humpatia Karma ka-takrima kisha Karma kupotezea? Tangu nimezaliwa ninasikia CCM ikilaumiwa sana. Mzee Pascal ni mtu mwenye uzoefu mkubwa wa kufeli kwenye kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Criticism dhidi yake sio ya kitoto ila huyu dingii haterereki.

4. MZEE MOHAMED SAID
Mzee wetu ni miongoni mwa watu wachache wanaojua mambo mengi sana ya nchi yetu. Ila yeye kaamua kujizima data na kulazimisha kuwa bila familia ya Sykes hii Tanzania isingekua hivi. Kuwa kina Sykes ndo kama waliibeba TZ mabegani na kuhakikisha inapata uhuru. Huwezi mwelezea mtu mdini usimtaje huyu mzee wetu. Pamoja na yote bado mzee wetu ana ngozi ngumu sana. Hayumbishwi kwenye ishu zake za udini.

5. LUCAS MWASHAMBWA
Huyu jombi ndo staa mkubwa kwa sasa wa JF. Jamaa huwa anabubujikwa sana na machozi kila Mama Samia akiongea chochote. Mwenyewe hujiita kijana mzalendo ila wengi wanamshambulia kwa kumwita chawa.

Na
6. Cocastic cocastic ushahidi huu hapa 👇

Yeye alikwenda mapumziko Nashera wao wamemgeusia kibao lakini hajachukia
 
Tofauti kabisa na kina Malisa GJ, Maria Sarungi au Martin Maranja ambao hawana kabisa uvumilivu kwa yeyote atakayekuwa kinyume na mawazo yao hawa wanaJF wanapaswa kutunukiwa tuzo za uvumilivu kwa kutojali mashambulizi ya watu pale wanapopost nyuzi.

1. ERYTHROCYTE
Huyu mfuasi kindakindaki wa chama cha Mbowe ni mfano wa kuigwa kwenye ulimwengu wa demokrasia. Huyu ni mtu aliyekula kiapo cha utiifu kwa mwenyekiti wa chama chake kiasi kwamba post zake nyingi huwa ni kumsifu chairman. WanaCCM wamekuwa wakimwandama kwa hoja na baadhi kutumia lugha za kuudhi ila huyu mfuasi wa Mbowe hajawahi rudi nyuma.
Sina shaka naye
2. BIBI FAIZA FOXY
Bibi yetu ambaye inasemekana ndo alikuwa Slayqueen wa enzi za TANU, yaani nchi inapata uhuru yeye tayari kashakula nauli za wakoloni kadhaa.. sio poa. Ni bibi mahiri sana kwenye hoja zake ila wananchi wengi hukwazwa sana na chembechembe za udini alizo nazo. Mwisho wa siku bibi Faiza ni mtu asiyetishwa na maneno ya kumkatisha tamaa kwenye anachoamini.
Unampaisha kwa kumsagia kunguni
3. MZEE PASCAL MAYALLA.
Mzee wetu ni muumini mzuri wa sheria ya KARMA. Huamini kabisa hakuna baya utakalofanya halafu karma isitimize wajibu wake wa kukuadhibu. Ila huwa najiuliza KARMA huwa inasahau anwani ya CCM au huwa inakumbuka ila CCM humpatia Karma ka-takrima kisha Karma kupotezea? Tangu nimezaliwa ninasikia CCM ikilaumiwa sana. Mzee Pascal ni mtu mwenye uzoefu mkubwa wa kufeli kwenye kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Criticism dhidi yake sio ya kitoto ila huyu dingii haterereki.
mwalimu zaidi
4. MZEE MOHAMED SAID
Mzee wetu ni miongoni mwa watu wachache wanaojua mambo mengi sana ya nchi yetu. Ila yeye kaamua kujizima data na kulazimisha kuwa bila familia ya Sykes hii Tanzania isingekua hivi. Kuwa kina Sykes ndo kama waliibeba TZ mabegani na kuhakikisha inapata uhuru. Huwezi mwelezea mtu mdini usimtaje huyu mzee wetu. Pamoja na yote bado mzee wetu ana ngozi ngumu sana. Hayumbishwi kwenye ishu zake za udini.
Huyu mzee kawazidi wote kwa uvumilivu
5. LUCAS MWASHAMBWA
Huyu jombi ndo staa mkubwa kwa sasa wa JF. Jamaa huwa anabubujikwa sana na machozi kila Mama Samia akiongea chochote. Mwenyewe hujiita kijana mzalendo ila wengi wanamshambulia kwa kumwita chawa.
Huu ni mradi. Artificial intelligence huwa inabubujika majibu hata ukiikera namna gani
 
MZEE PASCAL MAYALLA.
Mzee wetu ni muumini mzuri wa sheria ya KARMA. Huamini kabisa hakuna baya utakalofanya halafu karma isitimize wajibu wake wa kukuadhibu. Ila huwa najiuliza KARMA huwa inasahau anwani ya CCM au huwa inakumbuka ila CCM humpatia Karma ka-takrima kisha Karma kupotezea? Tangu nimezaliwa ninasikia CCM ikilaumiwa sana. Mzee Pascal ni mtu mwenye uzoefu mkubwa wa kufeli kwenye kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Criticism dhidi yake sio ya kitoto ila huyu dingii haterereki.
Pascal Mayalla
 
Mwashambwa siku hizi atakuwa Hana smart phone,azidishe uchawa kwa mbunge wa mbeya atamnunulia
 
Dini hizi zimepotosha wengi,Mzee Mohamed muamini mungu inatosha,au karibu kuwa pagan.
CCM...
Maudhui iliyopo mezani ni ustahamilivu katika mijadala hapa JF.

Tujikite katika mada mambo ya imani ikiwa unapenda kujadili fungua uzi mpya katika Jukwaa husika.
 
CCM...
Maudhui iliyopo mezani ni ustahamilivu katika mijadala hapa JF.

Tujikite katika mada mambo ya imani ikiwa unapenda kujadili fungua uzi mpya katika Jukwaa husika.
Sawa,kuhusu imani hapana sababu dini kwangu ni uongo mtupu.
 
Sawa,kuhusu imani hapana sababu dini kwangu ni uongo mtupu.
CCM...
Imani ni suala la mtu binafsi na katiba ya Tanzania inalinda haki hii.

Hakuna wa kukubughudhi kwa kutoamini dini.

Mwenye kuamini dini sheria inamkataza kumbagua au kumbughudhi asiye na dini na halikadhalika asiye na dini asimbague au kumbughudhi mwenye dini.

Hili liko wazi.

Ndiyo maana CCM ina wanachama hadi Singasinga lau ni wachache sana nchini.
 
Sina shaka naye

Unampaisha kwa kumsagia kunguni

mwalimu zaidi

Huyu mzee kawazidi wote kwa uvumilivu

Huu ni mradi. Artificial intelligence huwa inabubujika majibu hata ukiikera namna gani
Msanii,
Mimi ni mwalimu nasomesha historia ya uhuru wa Tanganyika sitakiwi kuonyesha hulka mbaya.

Mwalimu hatakiwi kurushiana maneno na wanafunzi.

Mwalimu kazi yake ni kuelimisha jamii.

Naijua historia ya TANU na naisomesha kwa utulivu:

"Msomaji wangu jina lake Madagascar baada ya kusoma moja ya makala zangu niliyoeleza kuwa mradi wa kwanza wa kuandika historia ya TANU ulikuwa mwaka wa 1962 watafiti na waandishi wakiwa Abdul Sykes na Dr. Wilbert Klerruu, nilieleza kuwa Abdul Sykes alijitoa na Dr. Klerruu akabakia kukamilisha kazi, aliniandikia kutaka kujua sababu ya Abdul Sykes kujitoa.

Madagascar,
Kleruu alikuwa hana moja alijualo katika historia ya AA.

Abdul Sykes kwanza alikuwa na mswada wa kitabu alioandika baba yake.

Mswada huu ulikuwa kumbukumbu za baba yake akieleza historia ya vipi babu yake Sykes Mbuwane alikuja Germany Ostafrika kama askari mamluki chini ya Hermann Von Wissman.

Ndani ya mswada huu anaeleza maisha yake chini ya utawala wa Wajerumani hadi WW I akiwa askari ndani ya jeshi la Kamanda Von Lettow Vorbeck.

Anaendelea kueleza utawala wa Waingereza baada ya WW I 1918.

Anaeleza alivyounda African Association 1929 baada ya kukutana na Dr. Kweggiyr Aggrey 1924.

Anaendelea kueleza kilichomsukuma kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 kikiwa chama pembeni ya AA.

Hapa katika miaka ya 1930s anaeleza juhudi za Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika kujenga shule ili Waislam kama Wamishionari wawe na shule zao akiweka msisitizo wa Qur'an kusomeshwa kama somo katika shule.

Kleist anaeleza ushawishi wa Waislam katika taasisi hizi mbili AA na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na nguvu iliyozuka katika kukabiliana na ukoloni.

Abdul haya licha ya kuwa yameandikwa na baba yake lakini kazaliwa na kukua ndani ya historia hii na baada ya WWII na akiwa askari wa KAR ndani ya Burma Infantry akawa anaandika vipi vita hivi vilivyowasaidia Waafrika kujitambua na kuamua kudai uhuru wa Tanganyika.

Yeye binafsi alikuwa na mchango wake katika kuwakabiliaba na Waingereza kwanza kupitia Dockworkers Union kisha haada ya kuchukua uongozi wa TAA 1950 akiwa na Dr. Vedasto Kyaruzi.

Kipindi hiki ndicho kipindi muhimu sana katika historia ya TAA kwani vijana wengi kutoka Makerere College walijiunga na TAA mjini Dar-es-Salaam pale New Street.

Hiki ndicho kipindi cha bongo za kizazi kipya cha wakati ule akina Hamza Mwapachu na viongozi wengine kutoka Kanda ya Ziwa kama Ali Migeyo, Saadan Abdu Kandoro na Paul Bomani wakaanza kukusanya nguvu zao pamoja kumkabili Gavana Edward Francis Twining.

Abdul na Hamza Mwapachu wanaweka msingi wa kuunda TANU na kutafuta kiongozi mmoja kuongoza harakati za uhuru.

Abdul yeye alimtaka Chief David Kidaha Makwaia ndiye aje TAA waunde TANU.

Mwapachu yeye mtu wake alikuwa Julius Nyerere lakini mwaka wa 1950 Nyerere alikuwa hajulikani wakati Chief Kidaha alikuwa mjumbe wa LEGCO toka mwaka wa 1945.

Abdul Sykes 1950 tayari alikuwa kijana maarufu na kiongozi wa TAA na alikuwa mjumbe katika TAA Political Subcommitee pamoja na Mwapachu, Kyaruzi, Sheikh Hassan bin Ameir na Steven Mhando kwa kawataja wachache.

Huu ndiyo mwaka Abdul Sykes alikwenda Nairobi kufanya mazungumzo na Jomo Kenyatta.

Hii kamati ndani yake alikuwapo Mwanasheria Earle Seaton akitoa ushauri nyuma ya pazia.

Hii ndiyo kamati akiwemo Dossa Aziz na John Rupia iliyokuja kuunda chama cha TANU 1954.

Lakini muhimu alieleza mkutano nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio, Ukerewe alipokwenda kaongozana na Ali Mwinyi Tambwe agenda kuu ikiwa kupata kauli ya Mwapachu kuhusu kumtia Nyerere kwenye uongozi wa juu kabisa wa TAA.

Hamza alimshauri Abdul kuwa Nyerere asaidiwe ashinde uchaguzi wa 1953 awe President na 1954 TANU iundwe.

Haya ndiyo Abdul aliyoandika katika kueleza chimbuko la TANU na Abdul akaeleza vipi alikuja kujuana na Nyerere 1952.

Inasemekana kuwa Julius Nyerere hakupendezewa na historia hii.

Abdul akajitoa katika ule mradi akamwacha Dr. Kleruu.

Naweka kitabu cha Abubakar Ulotu, ‘‘Historia ya TANU,’’ kitabu kilichotokana na utafiti na uandishi wa Dr. Wilbert Klerruu.

Hiki kitabu cha Abubakar Ulotu ni kutoka mswada wa historia ya TANU kilichokuwa kinaandikwa pale TANU Office na Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu mwaka wa 1962 Nyerere akihusika.

Kama nilivyoeleza hapo juu Abdul Sykes alijitoa katika uandishi wa historia ya TANU.

Dr. Kleruu akaendelea na uandishi hadi ukakamilika lakini TANU hawakuweza kukichapa kitabu kile.

Abubakar Ulotu akachukua mswada ule kwa siri na bila idhini ya TANU akachapa kitabu baada ya kufanya mabadiliko kidogo akaweka jina lake kama mwandishi.

Hivi sasa kipo kitabu cha maisha ya Julius Nyerere.

Muhimu kujua nini kimeandikwa kuhusu uasisi wa TANU na mchango wa Nyerere.

Waandishi wa kitabu hiki walifanya mahojiano na mwandishi."
 
Back
Top Bottom