The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Zaidi ya wananchi 300 wa Kijiji cha Ikungugazi kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wamekabidhiwa Hati za Ardhi za Kimila. Wananchi hao wameeleza kuwa hati hizo ni urithi kwa watoto wao, na kwamba zitaongeza thamani ya ardhi, kupunguza migogoro ya ardhi, na kuwawezesha kuwa na umiliki wa ardhi kisheria.
Akikabidhi hati hizo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe, Paulo Faty, amesema wananchi waliokabidhiwa hati za ardhi wana haki ya umiliki na wanatambuliwa na sheria kama wamiliki halali.
Kwa upande wake, msimamizi wa Kanda ya Ziwa kutoka Tume ya Taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi, Abdallah Magombana, amesema wameweza kutatua migogoro ya ardhi kati ya kijiji cha Ikungugazi na vijiji vilivyokuja kuzaliwa baadaye. Amesema pia tume hiyo imeweka mipaka ya vijiji vitatu vilivyokuwa vimepakana na msitu wa Halmashauri ya Mbogwe, na kupewa ekari 2,300 baada ya Serikali kutoa mwongozo kwa wananchi waliosogea maeneo hayo.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, vijiji tisa vimepitiwa na tume hiyo na kupatiwa jumla ya hati 300 za ardhi za kimila.