Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma wameviasa vyama vya siasa nchini kudumisha amani wakati wa kukamilisha michakato ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024
Kadhalika, wameishukuru Serikali kwa kutoa muda zaidi kwa wagombea ambao hawakuridhika kukata rufaa. Ikumbukwe jana Novemba 15 ilikuwa mwisho wa kupokea na kusikiliza rufaa za wagombea wa nafasi mbalimbali.