KERO Wananchi Kibangu mtaa wa Kajima jimbo la Ubungo hatuna maji mwezi wa tatu sasa

KERO Wananchi Kibangu mtaa wa Kajima jimbo la Ubungo hatuna maji mwezi wa tatu sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
NIMEONA NIWEKE LINK YA DAWASA HAPA WANANCHI WANALALAMIKA WANAJIBIWA HOVYO TUNAOMBENI MSAADA HAPA JF[emoji1313]

Shida ya maji maeneo ya Kibangu 1996- 2000 ilinifanya nichukie kibangu na jirani yake .. hata nilipoanza maisha sikufikiria kununua eneo kiwanja huko hata uchimbaji wa maji maeneo hayo sio mrahisi


Karibuni kigamboni..
 
Tuna miezi mitatu hatuna maji

Eneo ni kajima (Rivaside juu) mtaa wa Kibangu Ubungo

Maji hayatoki lakini watu wanauza maji na kuleta na magari na kuyauza kwa ndoo 500

Tumelalamika tumechoka inaonekana kuna mfumo wa watu kula hela na kujineemesha

Kipindi cha Magufuli maji yalikua yakitoka

Sio hivyo tu, wameleta matank ya kuuza maji na inadaiwa na miradi ya mheshimiwa fulani hivi

Naombeni mnisaidie namba ya Aweso tumechoka!!
 
Na ni Dar es Salaam na Kuna bahari kubwa tu ya India, ni aibu Kwa chama tawala kuwa baada ya miaka 60 ya uhuru bado watu wanateseka na shida ya maji, uarabuni huko wanakoenda kuomba misaada na kuwapa bandari zetu wanaishi jangwani lakini hawana shida ya maji Kwa kuwa wanayafanyia desalination maji ya bahari na yanakuwa potable Kwa ajili ya kunyweka Kwann tusiombe huo utaalamu tukayafanyia desalination maji ya bahari ya Hindi yakawa potable Kwa ajili ya kunyweka na hivyo kupunguzia watu adhabu ya kukaa miezi mingi bila maji ambayo kimsingi ni muhimu Kwa maisha ya binadamu Kwa kweli ni aibu Kwa nchi iliyobarikiwa maziwa makubwa, mito, na bahari kuwa na shida ya maji, AIBU hii haipatikani popote duniani isipokuwa Tanzania tu
Watu wako busy kuliombea taifa huku wakiacha viongozi wanafanya wanavyotaka. Kuomba hakujawahi kulikomboa taifa lolote.
 
Bonyokwa ipi? Halafu haipo Ubungo. Maji tunapata
Bonyokwa ya Tabata maji yapo. Huku hatutaki mchezo, yakikosekana tu wiki dawasa wanakipata . Kuna group la dawasa lakujadili masuala ya maji, so tatizo lolote linashughulikiwa. Tena yanatoka na pressure kubwa hadi yanapasua mabomba.
 
Hili hili linatosha kuwawajibisha viongozi. Sema nini wao wameshiba, tumewaajiri wameshindwa kazi basi tuwatoe tuwaajiri wengine, yaani bana hii sema watu ni waoga mno, yaani mtu umemuajiri wewe unashangaa Tena unaanza kumuogopa tena
 
Kabisa
Hili hili linatosha kuwawajibisha viongozi. Sema nini wao wameshiba, tumewaajiri wameshindwa kazi basi tuwatoe tuwaajiri wengine, yaani bana hii sema watu ni waoga mno, yaani mtu umemuajiri wewe unashangaa Tena unaanza kumuogopa tena
 
Back
Top Bottom