KERO Wananchi Kibangu mtaa wa Kajima jimbo la Ubungo hatuna maji mwezi wa tatu sasa

KERO Wananchi Kibangu mtaa wa Kajima jimbo la Ubungo hatuna maji mwezi wa tatu sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Fact
Uwezo wa mitambo kupumb maji kutoka kwenye matank na kuwapelekea wakazi WA kwenye mwinuko na hili tatizo halitakwisha kwasababu Lucas Mwashambwa anakubali kuwa Tanzania itauza umeme nje Ati kwasababu ni mwingi Sana kwahiyo mambo ya kutumia umeme kusukumia maji kuwapelekea wakazi wenye uhitaji hayana kipaumbele .Kama Leo Tu unatuambia kuna mitambo imewashwa pale Nyerere power plant na hadi sasa kuna maeneo hayana maji sababu zikiwa ni zile zile sasa huu mradi wa Nyerere Una tija gani Kwa taifa? Nje hapo Lucas atuambie Dar es salaam ina upungufu wa rasilimali maji na kwamba Dar es salaam ni jangwa moja linalo tegemea Oasis
 
Tatizo ni kubwa sana
Back in 2006 nikiwa form four na wanangu tulipanga chumba maeneo ya ubungo kibangu aisee kulikuwa na shida ya maji usipime! Nashangaa imepita miaka karibia 20 tatizo bado lipo palepale, inasikitisha sana
 
[emoji91]
Na ni Dar es Salaam na Kuna bahari kubwa tu ya India, ni aibu Kwa chama tawala kuwa baada ya miaka 60 ya uhuru bado watu wanateseka na shida ya maji, uarabuni huko wanakoenda kuomba misaada na kuwapa bandari zetu wanaishi jangwani lakini hawana shida ya maji Kwa kuwa wanayafanyia desalination maji ya bahari na yanakuwa potable Kwa ajili ya kunyweka Kwann tusiombe huo utaalamu tukayafanyia desalination maji ya bahari ya Hindi yakawa potable Kwa ajili ya kunyweka na hivyo kupunguzia watu adhabu ya kukaa miezi mingi bila maji ambayo kimsingi ni muhimu Kwa maisha ya binadamu Kwa kweli ni aibu Kwa nchi iliyobarikiwa maziwa makubwa, mito, na bahari kuwa na shida ya maji, AIBU hii haipatikani popote duniani isipokuwa Tanzania tu
 
Wewe utakua afisa wa dawasa tu
Mbona unakuwa muongo mzee minipo kimara stopover maji mbona siyo shida kama unavyosema kukatika yanakatika ila siyo kama unavyosema et miezi mitatu kitu unachotakiwa kufanya ndo hata mimi nimefanya nimenunua simitank ya lita 2000 ndo nipo nayo ingawa nyumba ya kupanga najua nikimaliza ujenzi nikiamia kwangu ntaondoka nayo
 
Tunakuja huko
Shida ya maji maeneo ya Kibangu 1996- 2000 ilinifanya nichukie kibangu na jirani yake .. hata nilipoanza maisha sikufikiria kununua eneo kiwanja huko hata uchimbaji wa maji maeneo hayo sio mrahisi


Karibuni kigamboni..
 
Fact
Wachaga wazee wa fursa wangeshachukua hilo dili fasta, ukiona hivyo huenda maji yake yana chumvi sana au ni gharama sana kuyapata hayo maji, kuna sehemu nilienda Malamba mawili kuchimba kisima mpaka upate maji ni almost 8 milion, na hapo huenda ukapata ya chumvi.
Sasa shida yote ya nini.

Nilichoona kule mtu ananunua tenki kubwa anaagiza gari inaleta maji anawauzia watu.
 
Mkuu chimba kisima uuze maji, kwenye tatizo ndio penye fursa.
Maji mengi ya kisima dar siyo salama sababu ya uhovyo wa mipango miji.yaani viwanja vidogo na mashimo ya vyoo lukuki
 
Tuna miezi mitatu hatuna maji

Eneo ni kajima (Rivaside juu) mtaa wa Kibangu Ubungo

Maji hayatoki lakini watu wanauza maji na kuleta na magari na kuyauza kwa ndoo 500

Tumelalamika tumechoka inaonekana kuna mfumo wa watu kula hela na kujineemesha

Kipindi cha Magufuli maji yalikua yakitoka

Sio hivyo tu, wameleta matank ya kuuza maji na inadaiwa na miradi ya mheshimiwa fulani hivi

Naombeni mnisaidie namba ya Aweso tumechoka!!
 
Duh hata banana ukonga toka Nov mpaka sasa hakuna maji manager dawasa kinyerezi haeleweki kila siku anatoa ahadi hewa
 
Watu maji yanawatesa sana
Ila wakati wa uchaguz mitaa walikuwa wanaleta boza la maji
Dawasco wanawagawia watu maji...uchaguz umeisha maumivu pale pale

Ova
Ni mateso kwa kweli.
 
Ubungo kuna shida ya maji sio poa

Usijichanganye ukapanga Ubungo kibangu, kajima,makoka, Rivaside juu au Msewe, maeneo mengi ya Mbezi

Mfano Ubungo kibangu huwa ni kawaida ya watu kukaa miezi mitatu mpaka 6 bila maji

Maji yakitoka ni mara moja kwa mwezi tena yatoke hata lisaa hayamalizi.

Kuna mtaa unaitwa Kajima (Rivaside juu) huu mtaa ni balaa hamna siku imewahi kutokea maji yakakaa hata robo siku hali ni mbaya sana na huku hakuna visima, watu wamelalamika Dawasa na wameenda hadi dawasa lakini dawasa ni kama wamepuuza na kuwatelekeza wananchi

Tunaomba mtupazie sauti jamani, tunaomba jamiiforum mtupostie kero yetu hii kwenye page zenu za mitandao ya kijamii labda waziri atatusikiliza maana tumelalamika ngazi zote lakini hatujapata msaada wowote

Hizo sehemu hazifai
Kakindu Pongwe, Tanga mwezi wa pili unaenda wa Tatu huu
 
Back
Top Bottom