KERO Wananchi Kibangu mtaa wa Kajima jimbo la Ubungo hatuna maji mwezi wa tatu sasa

KERO Wananchi Kibangu mtaa wa Kajima jimbo la Ubungo hatuna maji mwezi wa tatu sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Yupo bize huko kusifia watawala anasahau jimbo lake.

Useless Member of Parliament
Ubungo Kibangu mtaa wa Kajima kuna shida sugu ya maji, na Mbunge ni Profesa kitila mkumbo lakini hamna kitu ametusaidia

Suluhisho la maji alileta mradi wa matenk yaani matenki yanajazwa maji kisha wananchi wanauziwa maji nayo ni kama yametelekezwa.

Ni mwezi wa tatu huu hatuna maji naombeni mtusaidie namba ya Waziri Aweso hali ni mbaya!!

Tuna miezi mitatu bila maji na wananchi wanateseka na huku hamna visima, imagine mateso wanayopitia wananchi.

Mwenye namba ya waziri aweso naomba please hali ni mbaya sana tushalalamika tumechoka dawasa wametupuuza!!
 
Poleni ubungo na vitongoji vyake.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Wr
Mbona unakuwa muongo mzee minipo kimara stopover maji mbona siyo shida kama unavyosema kukatika yanakatika ila siyo kama unavyosema et miezi mitatu kitu unachotakiwa kufanya ndo hata mimi nimefanya nimenunua simitank ya lita 2000 ndo nipo nayo ingawa nyumba ya kupanga najua nikimaliza ujenzi nikiamia kwangu ntaondoka nayo
Umeishia darasa la ngapi wewe?
Mwenzio kasema maeneo ya ubungo, riverside na msewe....kimara stopover imekuja vipi kwenye mada?
 
Kuna maeneo mengine sijui watu mnaishije

Ova
 
Ubungo kuna shida ya maji sio poa

Usijichanganye ukapanga Ubungo kibangu, kajima,makoka, Rivaside juu au Msewe, maeneo mengi ya Mbezi

Mfano Ubungo kibangu huwa ni kawaida ya watu kukaa miezi mitatu mpaka 6 bila maji

Maji yakitoka ni mara moja kwa mwezi tena yatoke hata lisaa hayamalizi.

Kuna mtaa unaitwa Kajima (Rivaside juu) huu mtaa ni balaa hamna siku imewahi kutokea maji yakakaa hata robo siku hali ni mbaya sana na huku hakuna visima, watu wamelalamika Dawasa na wameenda hadi dawasa lakini dawasa ni kama wamepuuza na kuwatelekeza wananchi

Tunaomba mtupazie sauti jamani, tunaomba jamiiforum mtupostie kero yetu hii kwenye page zenu za mitandao ya kijamii labda waziri atatusikiliza maana tumelalamika ngazi zote lakini hatujapata msaada wowote

Hizo sehemu hazifai
Pole sana mkuu najaribu kuwaza mkijisaidia mnachambia nini!??

Sipati majibu kabisa
 
kibangu inakuwaga na shida ya maji sana, nimeishi mitaa hiyo
 
Bado hujaenda maramba mawili sjui msakuzi huko 😄 balaa

Ova
 
Back
Top Bottom