Wananchi masikini ndani ya Nchi tajiri. Hata kama CCM itakufa sitokuja isahau

Wananchi masikini ndani ya Nchi tajiri. Hata kama CCM itakufa sitokuja isahau

Chochote kingine akiwepo lissu
Choice Variable nikuambie kitu?
Nimefuatilia kwa undani nimekuta Bandari za Tanganyika hazijauzwa wala kukodishwa kwa waarabu wa Dubai bali zote wamepewa bure!
 

Attachments

  • 72AFCDC4-6DFB-4321-A7BE-8CC6E007BC3E.jpeg
    72AFCDC4-6DFB-4321-A7BE-8CC6E007BC3E.jpeg
    115 KB · Views: 1
Unailaumu ccm lakini naona wenye shida ni sisi wananchi kwa sababu tungekuwa na akili timam ccm ingekuwa jumba la makumbusho siku nyingi
 
Unailaumu ccm lakini naona wenye shida ni sisi wananchi kwa sababu tungekuwa na akili timam ccm ingekuwa jumba la makumbusho siku nyingi
Tatizo tumejengwa katika Uwoga, Upendo wa kinafki na chuki zetu nddizo zinatumaliza na haya yote yanaanzia kwenye elimu tunayopewa
 
Choice Variable nikuambie kitu?
Nimefuatilia kwa undani nimekuta Bandari za Tanganyika hazijauzwa wala kukodishwa kwa waarabu wa Dubai bali zote wamepewa bure!
🤣🤣🤣🤣
 
Njoo pande hizi za kiroho,

Nnji hii Ina mfumo wa Vyama vingi ktk Ulimwengu wa mwili,

Bt katika Ulimwengu wa Roho, Nchi hii Ina mfumo BADO wa chama kimoja.

Kufa Kwa CCM Si jambo dogo kama tunavyodhani,

Kifo Cha CCM lazima kisababishe mengine mengi Kutokea.

Kufa na ife,

Bt kifo chema, Cha Utaratibu na mrithi apatikane mchana kweupe jua la utosini.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
 
Habari JF,

Binafsi sitachoka kuinyooshea kidole CCM kwa matatizo na maendeleo duni ya Taifa hili mbali na Tanzania kujaliwa maliasili nyingi sana.

CCM imetuaminisha kwamba hatuwezi fanya maendeleo bila Misaada ,mikopo na kujipendekeza nje ya Nchi.

CCM imefanya wananchi masikini kiasi kwamba muda mwingi wanapambana kutafuta kula yao na afya zao hawana hata muda wa kufuatilia nini kinaendelea katika nchi yao.

CCM imefanya Tanzania badala ya kuwa Muuzaji mkuu wa Nguo, sukari, gesi, Chuma, vito vya dhahabu, makaa ya mawe, samaki ...nk na dampo la bidhaa toka nje.

CCM imefanya wananchi waamini wao hawawezi kufanya kitu ni lazima kusaidiwa na mataifa ya nje.

CCM imefanya wananchi /viongozi wasiwe wazalendo bali wawe ni watu wa kuangalia maslahi yao na kufurahishana tu bila kujali maslahi ya nchi.

Mimi RNA sitoipigia kura CCM 2025 tuungane kuitoa madarakani na hata kama ikifa sitokuja isahau, na hata ntakufa kabla haijatoka madarakani ifahamike sijawahi isapoti iendelee kuwepo madarakani.
CCM imesababisha kuwe na CHAWA wengi sana, watu wanajitoa UFAHAMU kwaajili ya kupambania matumbo yao. AJABU SANA
 
Back
Top Bottom