KERO Wananchi Mti Mmoja - Monduli (Arusha) wanakunywa maji ya bwawa yaliyotuama, hakuna Huduma ya Maji ya Bomba

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Juzikati Oktoba 23, 2024 nilipofika eneo la Mti Mmoja - Monduli (Arusha) nikiwa njiani kuelekea Dodoma nikitokea Arusha, niliona jambo la kushangaza sana, nilishuhudia Wanafunzi wa shule wakinywa maji yaliyotuama ya mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu (2024).

Mbali na Watoto hao, nilishuhudia hata watu wazima wakichota maji hayo ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu, nilipowauliza wanaenda kutumia katika matumizi gani, walisema wanaenda kunywa na kupikia.
Screenshot 2024-10-28 114134.png

Screenshot 2024-10-28 114150.png
Nilipoendelea kusema nao, waliniambia eneo hilo la bwawa linalindwa usiku na mchana, kwa maana usiku vijana wa maeneo ya Mti Mmoja, Nanja, Lendikinya na Orukaria huwa wanakuja kulinda tembo wasinywe maji katika eneo hili, pia mchana wanalinda mifugo isije kunywa maji eneo hilo.

"Tusipolinda, tembo mmoja akija kunywa maji hapa atakunywa lita mia mbili, je wakija kumi? Huoni sisi tutakosa maji? Tumepanga zamu kwa vijana 20 kutoka kila siku usiku kwa ajili ya kulinda eneo hili tembo asifike kabisa," alisema mmoja wa Mwanakijiji.

Nilipowauliza wanawezaje kuwalinda tembo hao, waliniambia wanatumia kamba kuwarushia mawe hadi waondoke licha kwamba wanakumbana na hatari kutoka kwa wanyama hao.

Kwakuwa nilikuwa na haraka niliongea na baadhi ya Wananchi waliokuwa pale, waliniambia wameteseka kwa muda mrefu bila kuwa na maji safi na salama hali ambayo imekuwa ikiwasababishia maradhi kuhara na mengineyo mengi.

Wote kwa pamoja, waliiomba Serikali kufanya juhudi za haraka sana kwakuwa wanateseka mno kutokana na kadhia hiyo.

Nikiwa naelekea kwenye gari ili niondoke nilijiuliza vipi kuhusu mifugo itakuwa inapataje maji, nilipouliza kwa mmoja wa mchungi aliniambia wananunua maji yanayoletwa kutoka duka bovu ambapo kuna umbali wa zaidi ya kilometa 20, na wananunua kwa shilingi 50,000 kwa lita 1,000, ikiwa na maana kuwa ndoo moja ya lita 20 ni shilingi 500.

Mchungi huyo aliniambia maji hayo unaweza kutumia kwa siku mbili tu, na itakubidi ukanunue tena hali anayodai inawaporomosha kiuchumi kutokana na kulazimika kuuza baadhi ya mifugo ili kujipatia maji hayo.

Nilipomuuliza kwanini asiende kuchota kwenye bwawa lililopo karibu naye? aliniambia hawaruhusiwi kwenda kuchota wakiwa na pikipiki ya miguu mitatu (guta) kwa kuwa kila mmoja akienda hivyo hayo maji ya bwawa yataisha na wananchi watakosa maji.

Nikipata safari tena ya kuelekea huko Kaskazini nitawatembelea wananchi hawa tena, ila kwa nafasi yangu kama Mtanzania nimetimiza wajibu wangu, sasa kazi kwenu Serikali.
Screenshot 2024-10-28 114217.png

=====

UPDATES ; 30 OKTOBA 2024

=====

WIZARA YA MAJI YATOLEA UFAFANUZI KERO HII.

Wizara imesema eneo la Mtimmoja ni moja wapo wa Vijiji 13 vitakavyonufaika na mradi mkubwa wa Maji wa Vijiji 13 ambao kwa sasa uko katika hatua ya ujenzi na utakamilika karibuni ambapo Mkandarasi yuko site kwa gharama ya Tshs Bilioni 20.3.

Kusoma zaidi, bonyeza HAPA
 
Nchi imeoza kabisa.halafu unasikia kichaa mmoja ananunua goli la Mpira Kwa milioni kumi.
 
Hela zote rais anawapa akina pacome na azizik watume kwa wazazi wao

Hatuna rais hii nchi ovyo kabisa yaan
 
Monduli kwa ujumla iko nyuma mno. Watu walikuwa wanamuabudu hayati EL ila jimboni kwake hakuna alilofanya. Hata huyu mwanae aliyemrithisha ubunge ni hovyo.
 
Juzikati Oktoba 23, 2024 nilipofika eneo la Mti Mmoja - Monduli (Arusha) nikiwa njiani kuelekea Dodoma nikitokea Arusha, niliona jambo la kushangaza sana, nilishuhudia Wanafunzi wa shule wakinywa maji yaliyotuama ya mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu (2024).

Mbali na Watoto hao, nilishuhudia hata watu wazima wakichota maji hayo ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu, nilipowauliza wanaenda kutumia katika matumizi gani, walisema wanaenda kunywa na kupikia.
Nilipoendelea kusema nao, waliniambia eneo hilo la bwawa linalindwa usiku na mchana, kwa maana usiku vijana wa maeneo ya Mti Mmoja, Nanja, Lendikinya na Orukaria huwa wanakuja kulinda tembo wasinywe maji katika eneo hili, pia mchana wanalinda mifugo isije kunywa maji eneo hilo.

"Tusipolinda, tembo mmoja akija kunywa maji hapa atakunywa lita mia mbili, je wakija kumi? Huoni sisi tutakosa maji? Tumepanga zamu kwa vijana 20 kutoka kila siku usiku kwa ajili ya kulinda eneo hili tembo asifike kabisa," alisema mmoja wa Mwanakijiji.

Nilipowauliza wanawezaje kuwalinda tembo hao, waliniambia wanatumia kamba kuwarushia mawe hadi waondoke licha kwamba wanakumbana na hatari kutoka kwa wanyama hao.

Kwakuwa nilikuwa na haraka niliongea na baadhi ya Wananchi waliokuwa pale, waliniambia wameteseka kwa muda mrefu bila kuwa na maji safi na salama hali ambayo imekuwa ikiwasababishia maradhi kuhara na mengineyo mengi.

Wote kwa pamoja, waliiomba Serikali kufanya juhudi za haraka sana kwakuwa wanateseka mno kutokana na kadhia hiyo.

Nikiwa naelekea kwenye gari ili niondoke nilijiuliza vipi kuhusu mifugo itakuwa inapataje maji, nilipouliza kwa mmoja wa mchungi aliniambia wananunua maji yanayoletwa kutoka duka bovu ambapo kuna umbali wa zaidi ya kilometa 20, na wananunua kwa shilingi 50,000 kwa lita 1,000, ikiwa na maana kuwa ndoo moja ya lita 20 ni shilingi 500.

Mchungi huyo aliniambia maji hayo unaweza kutumia kwa siku mbili tu, na itakubidi ukanunue tena hali anayodai inawaporomosha kiuchumi kutokana na kulazimika kuuza baadhi ya mifugo ili kujipatia maji hayo.

Nilipomuuliza kwanini asiende kuchota kwenye bwawa lililopo karibu naye? aliniambia hawaruhusiwi kwenda kuchota wakiwa na pikipiki ya miguu mitatu (guta) kwa kuwa kila mmoja akienda hivyo hayo maji ya bwawa yataisha na wananchi watakosa maji.

Nikipata safari tena ya kuelekea huko Kaskazini nitawatembelea wananchi hawa tena, ila kwa nafasi yangu kama Mtanzania nimetimiza wajibu wangu, sasa kazi kwenu Serikali.
Mkuu haya maisha ya kutegemea na kutumia maji ya bwawa yamekuwa kawaida sana kwa wakazi wa Monduli na hata Simanjiro. Watu washazoea hiyo hali.

Nilishawahi kuishi maeneo hayo ya Nanja, Mti Moja na Nadosoito mwaka 2015, kuna mabwawa makubwa ambayo maji yake hutumiwa na watu na mifugo pia. Walichokuwa wanafanya baada ya kuchota hayo maji ni kuweka majivu ili kuondoa uchafu (sedimentation) ili yanyweke.

Pia kuna baadhi ya watu walipata aina fulani za ndoo za kuchuja hayo maji ili kupunguza uchafu. Zilikuwa zinatolewa na wazungu fulani kama sikosei.

Kipindi kama cha uchaguzi wanasiasa wakienda huko huahidi kuchimba mabwawa hayo kwani Kuna wakati yanajaa matope. Hawaahidi kuleta maji masafi na salama bali uchimbaji wa mabwawa mapya au kuboresha yale ambayo yapo kama yamejaa tope.

Maji hayo huwa na kinyesi cha wanyama na hata binadamu kwa sababu ni mkusanyiko wa maji kutoka ktk korongo ambazo watu huenda kwa haja. Kiukweli ni Mungu tu ndiye anayewasaidia watu huko.
 
C

Utakuta hapo Kuna Mwenyekiti wa Kijiji,Diwani,Mbunge,mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa,n.k Ccm oyeee...kaaaazi kwelikweli
 
Mbona Dar wapo wengi tu wanaokunywa maji ya madimbwi, njoo uswazi uyaone.
 
Mkuu haya maisha ya kutegemea na kutumia maji ya bwawa yamekuwa kawaida sana kwa wakazi wa Monduli na hata Simanjiro. Watu washazoea hiyo hali.

Nilishawahi kuishi maeneo hayo ya Nanja, Mti Moja na Nadosoito mwaka 2015, kuna mabwawa makubwa ambayo maji yake hutumiwa na watu na mifugo pia. Walichokuwa wanafanya baada ya kuchota hayo maji ni kuweka majivu ili kuondoa uchafu (sedimentation) ili yanyweke.

Pia kuna baadhi ya watu walipata aina fulani za ndoo za kuchuja hayo maji ili kupunguza uchafu. Zilikuwa zinatolewa na wazungu fulani kama sikosei.

Kipindi kama cha uchaguzi wanasiasa wakienda huko huahidi kuchimba mabwawa hayo kwani Kuna wakati yanajaa matope. Hawaahidi kuleta maji masafi na salama bali uchimbaji wa mabwawa mapya au kuboresha yale ambayo yapo kama yamejaa tope.

Maji hayo huwa na kinyesi cha wanyama na hata binadamu kwa sababu ni mkusanyiko wa maji kutoka ktk korongo ambazo watu huenda kwa haja. Kiukweli ni Mungu tu ndiye anayewasaidia watu huko.
Mdau
Eneo la Mtimmoja ni moja wapo wa Vijiji 13 vitakavyonufaika na mradi mkubwa wa Maji wa Vijiji 13 ambao kwa sasa uko katika hatua ya ujenzi na utakamilika karibuni ambapo Mkandarasi yuko site kwa gharama ya Tshs 20.3Bil.
Mradi huu ndio utamaliza kabisa changamoto ya Maji Monduli.

Hata hivyo mapema serikali ilikarabati Bwawa la Nanja ambalo pia linanufaisha kijiji cha Mtimmoja ambalo kwasasa kutokana na hali ya ukame unaoendelea limekauka, na hata hivyo mwaka 2022 hali hiihii ilitokea na serikali iligawa matenk 2 ya lita 5000 kwa kila kijiji kwa ajili ya kuhifadhia maji.
Kwasasa hatua za kuwapatia maji wananchi kwa hatua mbalimbali inaendelea kwa kushirikiana na mdau wadau.

Aidha, katika Kijiji jirani cha Meserani (duka bovu) na Lendikinya ambavyo viko jirani na vijiji hivi hupata maji kwa bei nafuu ya Tshs 50 kwa ndoo ya lita 20 na serikali itaendelea kusimamia bei hiyo kuhakikisha jumuiya za watumia maji hazipandishi ili wananchi wasitumie gharama kubwa kupata huduma hii muhimu.
1.jpeg
2.jpeg
3.jpeg
4.jpeg
 
Back
Top Bottom