BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mbali na Watoto hao, nilishuhudia hata watu wazima wakichota maji hayo ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu, nilipowauliza wanaenda kutumia katika matumizi gani, walisema wanaenda kunywa na kupikia.
"Tusipolinda, tembo mmoja akija kunywa maji hapa atakunywa lita mia mbili, je wakija kumi? Huoni sisi tutakosa maji? Tumepanga zamu kwa vijana 20 kutoka kila siku usiku kwa ajili ya kulinda eneo hili tembo asifike kabisa," alisema mmoja wa Mwanakijiji.
Nilipowauliza wanawezaje kuwalinda tembo hao, waliniambia wanatumia kamba kuwarushia mawe hadi waondoke licha kwamba wanakumbana na hatari kutoka kwa wanyama hao.
Kwakuwa nilikuwa na haraka niliongea na baadhi ya Wananchi waliokuwa pale, waliniambia wameteseka kwa muda mrefu bila kuwa na maji safi na salama hali ambayo imekuwa ikiwasababishia maradhi kuhara na mengineyo mengi.
Wote kwa pamoja, waliiomba Serikali kufanya juhudi za haraka sana kwakuwa wanateseka mno kutokana na kadhia hiyo.
Nikiwa naelekea kwenye gari ili niondoke nilijiuliza vipi kuhusu mifugo itakuwa inapataje maji, nilipouliza kwa mmoja wa mchungi aliniambia wananunua maji yanayoletwa kutoka duka bovu ambapo kuna umbali wa zaidi ya kilometa 20, na wananunua kwa shilingi 50,000 kwa lita 1,000, ikiwa na maana kuwa ndoo moja ya lita 20 ni shilingi 500.
Mchungi huyo aliniambia maji hayo unaweza kutumia kwa siku mbili tu, na itakubidi ukanunue tena hali anayodai inawaporomosha kiuchumi kutokana na kulazimika kuuza baadhi ya mifugo ili kujipatia maji hayo.
Nilipomuuliza kwanini asiende kuchota kwenye bwawa lililopo karibu naye? aliniambia hawaruhusiwi kwenda kuchota wakiwa na pikipiki ya miguu mitatu (guta) kwa kuwa kila mmoja akienda hivyo hayo maji ya bwawa yataisha na wananchi watakosa maji.
Nikipata safari tena ya kuelekea huko Kaskazini nitawatembelea wananchi hawa tena, ila kwa nafasi yangu kama Mtanzania nimetimiza wajibu wangu, sasa kazi kwenu Serikali.
=====
UPDATES ; 30 OKTOBA 2024
=====
WIZARA YA MAJI YATOLEA UFAFANUZI KERO HII.
Wizara imesema eneo la Mtimmoja ni moja wapo wa Vijiji 13 vitakavyonufaika na mradi mkubwa wa Maji wa Vijiji 13 ambao kwa sasa uko katika hatua ya ujenzi na utakamilika karibuni ambapo Mkandarasi yuko site kwa gharama ya Tshs Bilioni 20.3.
Kusoma zaidi, bonyeza HAPA