Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Acha kebehi na dharau mbona kuna familia zina nyumba za hali ya chini kuliko hizo na baadhi ya walimu wanatoka katika familia hizo. Hiyo ni zawadi wamejitolea wananchi kwahiyo vyovyote itakavyokuwa ndio kiwango chao walichojikamua. Madongo ni kwa serikali iliyoshindwa kuwajali walimu kwa vitu vidogo kama hivyo huku ikijaza madarasa kila uchao (imeandikwa waliojenga nyumba ni wananchi -siyo serikali ya kata, kijiji, wilaya, mkoa, wala halmashauri)Hizi ni nyumba au mabanda ya kufungia kuku? Wananchi wamuite kiongozi wa mbio za mwenge aje azindue
Tukirudi kwenye habari na picha iliyopo mbona kama haviendani? Maana naona kama imeandikwa kishabiki shabiki hivi 'coz picha inaonesha ni nyumba za matofali mabichi yasiyochomwa! Nyumba za tope nizijuazo mimi ni tofauti kabisa na hizi