Wananchi tuna haki kufahamu alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Hivi kama kiongozi mkubwa namna hii anawapambe kibao anatoweka na asijulikaline hakika alipo nawaza hawa akina kapuku wakitekwa si ndo basi.

Ni huzuni sana kuwa na serikali isiyozingatia umuhimu wa taarifa. Je, haya yaweza kuwa ni majaribio tu kwa matukio mengine makubwa?

Tuupe muda wakati,
 
Sidhani hata kama wanajali hizi dukuduku za wananchi. Nimesikia habari nzito kuhusu mwamba huyu lakini siwezi kuisema hapa kama ilivyokuwa vigumu kusema ya Magufuli aliyesemekana kufariki lakini serikali ikaja kutoa taarifa baada ya wiki moja hivyo kusogeza mbele tarehe ya kifo chake.

Ngoja pia waendelee kuficha ugonjwa wa Mpango lakini kifo kitawaumbua kama kilipowaumbua kwa Magufuli. Wakati ukuta.
"Brain respiratory center shut down" Anaandika de'levis,kwamba hiyo center Huwa Ina shutdown pole pole hadi mshindo mkuu unakua kwenye oxygen machine!!

Nimekumbuka hii kitu leo!!iliwahi kuandikwa zamani humu jamvini!!
 
kivipi.

Then wanaotuongoza siyo binadamu wenzetu.
Ni kuzua taharuki na kumfanya mgonjwa (kiongozi) wetu katika hali anayopitia, kwa mwenendo wa kiusalama pia unajua taasisi ni watu na sio mtu , muda ukifika taarifa zitatolewa, ni kanuni tu na sheria zilizowekwa kikatiba
 
Katiba na sheria mnazozitunga nyie bila utashi wa raia ni batili na laanifu.

hauna hoja kiufupi
 
mkuu karibu sana sana kwetu. just panda gari la mwendokasi, ukishuka tu ulizia kwa Msanii, unafikishwa chap kwa haraka😅😅😅😅 (kidding)

ngoja niangalie Google hapa nijue nipo wapi kisha fungua inbobo
😂😂
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.

Rais ni wa Jamhuri ijulikane kuwa anamilikiwa na wananchi wote bila kujali itikadi, imani wala kabila. Nasema anamilikiwa ni kwa sababu shughuli zake zote zinamhusu kila raia awe mdogo au mkubwa kwa jinsia zote.

Rais anamilikiwa na wananchi ndo maana analindwa na wananchi na kutunzwa na kodi za wananchi. Ingawa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanadhani wao pekee ndo wenye dhamana ya kumtunza na kumlinda Rais. Wananchi watasali kwa miungu yao, watatambika kwa mahoka wao na kadhalika ilimradi Rais aweze kufikia matarajio na matamanio yao. Wenye Mungu nao watamuombea ili awe salama na aweze kutekeleza majukumu yake vyema.

Inaelekea tukio la marehemu JPM halijatupa funzo lolote. Zimeanza tetesi kupitia wale wale walioeneza uvumi kuhusu hatma ya JPM na sasa wanamtaja Makamu wa Rais. Tetesi hizi zimeendelea kupata mwangwi mkubwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu afya na uhai wa Makamu wa Rais.

Serikali, imeendelea kupuuza uvumi huo kama ilivyopuuza uvumi (uliokuwa siyo uvumi) enzi Mwendazake wakati anapigania uhai wake vyumba vya afya. Tuliona viongozi wakubwa akiwemo Waziri Mkuu wakitoa matamko ya kubeza tetesi hizo kwa kuuaminisha Umma kwamba Rais wao anachapakazi yupo gado kabisa.

Jana, serikali ilisambaza bango mitandaoni kumuonesha Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa TAWIRI unaoanza tarehe 06 Desemba 2023..... sisi tunaochoshwa na tetesi za vifo vya wakubwa tukanyenya mikono juu kumshukuru Mungu kuwa tetesi kuhusu hali ya Mhe. Mpango ni uzushi na upotofu. Lakini aliyefika mkutanoni ni mwakilishi (Mhe. Kairuki) na siyo mgeni mlengwa.

Tumepatwa na msiba wa kitaifa kule Hanang kwa kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mafuriko makubwa. Tumeona mfariji wa Taifa ambaye ni Rais ameshajitokeza na kusimama na wananchi wote na hata Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali wanafanya kila linalowezekana ili kuwanasua waliokwama chini ya tope zito la mlima Hanang. Lakini hatujamsikia popote Makamu wetu wa Rais akitoa pole kama ilivyo kawaida yake kwa matukio aina hii.

Kwa niaba ya Watanzania, naleta ombi kwa serikali ituondoe kizani kuhusu alipo makamu wa Rais. Hizi tetesi zinazoendelea hazina afya kwa Taifa.

Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.

Naomba tujulishwe
inakusaidia nini?
 
Ni kuzua taharuki na kumfanya mgonjwa (kiongozi) wetu katika hali anayopitia, kwa mwenendo wa kiusalama pia unajua taasisi ni watu na sio mtu , muda ukifika taarifa zitatolewa, ni kanuni tu na sheria zilizowekwa kikatiba
Taharuki gani itazuka? VP ni binadamu kama wengine. Punguza uchawa kama huwezi kuacha kabisa mkuu. VP akifa atazikwa, atateuliwa mwingine maisha yataendelea. Amekufa Magufuli sembuse VP.

Usiwajengee watanzania taharuki isiyokuwepo kwa sababu zako binafsi za kulinda na kutetea uchawa wako. Kuwa na nidhamu na wapiga kura. Watanzania wanataka kufahamu maendeleo ya kiongozi wao.

Baba wa Taifa, mwalimu Nyerere, allipougua leukemia taifa lilikuwa linajulishwa hali yake kila siku. Itakuwa Mpango? Tatizo la Mpango linatibika kwa kuwa amewahi matibabu ijapokuwa, kwa sababu ya umri mkubwa, hawezi kurejea kawaida 100%.

Machawa muache kututia hofu. Tunataka kujua kiongozi wetu anaendeleaje. Afu haya mambo ya kuficha ugonjwa yameanzia kwenye ugonjwa (Covid 19) wa Magufuli. Mbona ujinga huu haujawahi kuwepo kwenye nchi hii hapo kabla? Ni nani aliyenazisha huu mtindo wa kipuuzzi wa kuwaficha wananchi ugonjwa wa viongozi wao? Inauma na inasikitisha sana😳😳
 
Mimi nadhani labda VP yupo likizo ya mwisho wa mwaka...Ila sijui Kama yupo likizo..lazima aonekane hadharani??!!!!!! Mnataka aende sokoni Magomeni au kariakoo??

Anatumia fedha za nani huko? Magu alishasema kuna watu wasioenda kwao kbs wanabaki wazunguka nchi za watu. [emoji3]
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.

Rais ni wa Jamhuri ijulikane kuwa anamilikiwa na wananchi wote bila kujali itikadi, imani wala kabila. Nasema anamilikiwa ni kwa sababu shughuli zake zote zinamhusu kila raia awe mdogo au mkubwa kwa jinsia zote.

Rais anamilikiwa na wananchi ndo maana analindwa na wananchi na kutunzwa na kodi za wananchi. Ingawa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanadhani wao pekee ndo wenye dhamana ya kumtunza na kumlinda Rais. Wananchi watasali kwa miungu yao, watatambika kwa mahoka wao na kadhalika ilimradi Rais aweze kufikia matarajio na matamanio yao. Wenye Mungu nao watamuombea ili awe salama na aweze kutekeleza majukumu yake vyema.

Inaelekea tukio la marehemu JPM halijatupa funzo lolote. Zimeanza tetesi kupitia wale wale walioeneza uvumi kuhusu hatma ya JPM na sasa wanamtaja Makamu wa Rais. Tetesi hizi zimeendelea kupata mwangwi mkubwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu afya na uhai wa Makamu wa Rais.

Serikali, imeendelea kupuuza uvumi huo kama ilivyopuuza uvumi (uliokuwa siyo uvumi) enzi Mwendazake wakati anapigania uhai wake vyumba vya afya. Tuliona viongozi wakubwa akiwemo Waziri Mkuu wakitoa matamko ya kubeza tetesi hizo kwa kuuaminisha Umma kwamba Rais wao anachapakazi yupo gado kabisa.

Jana, serikali ilisambaza bango mitandaoni kumuonesha Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa TAWIRI unaoanza tarehe 06 Desemba 2023..... sisi tunaochoshwa na tetesi za vifo vya wakubwa tukanyenya mikono juu kumshukuru Mungu kuwa tetesi kuhusu hali ya Mhe. Mpango ni uzushi na upotofu. Lakini aliyefika mkutanoni ni mwakilishi (Mhe. Kairuki) na siyo mgeni mlengwa.

Tumepatwa na msiba wa kitaifa kule Hanang kwa kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mafuriko makubwa. Tumeona mfariji wa Taifa ambaye ni Rais ameshajitokeza na kusimama na wananchi wote na hata Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali wanafanya kila linalowezekana ili kuwanasua waliokwama chini ya tope zito la mlima Hanang. Lakini hatujamsikia popote Makamu wetu wa Rais akitoa pole kama ilivyo kawaida yake kwa matukio aina hii.

Kwa niaba ya Watanzania, naleta ombi kwa serikali ituondoe kizani kuhusu alipo makamu wa Rais. Hizi tetesi zinazoendelea hazina afya kwa Taifa.

Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.

Naomba tujulishwe
Likitokea la kutokea kwa makamu wa rais samia lazima awajibike maana ndio mchawi. Wananchi hawatakua tena na shaka.
 
Back
Top Bottom