Wananchi tunamsaidiaje Mpina?
Ukigusa maslahi ya CCM lazima wakukate kichwa. Luhaga Mpina kagusa maslahi ya WENYE NCHI.
 
Hakuna cha uonezi hapo. Alitaka tuendelee kununua sukari kwa shs 6000 plus? Anatumika tu kuwatetea wamiliki wa viwanda vya sukari waliogoma kuagiza sukari ya kuziba gap.
🎯👍👌👊👏🤝🙏🛡️

Mkuu bahati mbaya Mpina ni kiongozi mwandamizi wa Sukuma Gang! Kajiweka mwenyewe kwenye kilengeo!!!

Mwisho wake kisiasa umeshaamuliwa. Another Ndugai on the way out.

Mpina ndani ya CCM ni kama samaki majini, nje ya CCM hawezi chochote!!

Mkuu watoto wa mjini wanamsubiri nchi kavu wafanye kitoweo!!!

⚖️4Asimwe#
 
Kila mzalendo wa kweli anayelipenda Taifa lake, na mwenye akili timamu ANASIMAMA NA MPINA. Mimi naipenda nchi yangu na nina akili timamu.
 
Kila mzalendo wa kweli anayelipenda Taifa lake, na mwenye akili timamu ANASIMAMA NA MPINA. Mimi naipenda nchi yangu na nina akili timamu.
na unasimama na muongo 🐒
 
Taarifa ya Mpina ni ya hakika na inapaswa kuungwa mkono, lakini Mimi huwa siungi mkono watu walioshiriki dhuluma kipindi cha dhalimu magu. Hivyo aungwe mkono na wananchi, lakini mimi na watu wa dhuluma hapana.

Alisimamia Sheria.

Tuache chuki.

Pakiwa na Vita Haki ya mwanajeshi kuishi inaondoka kwa ajili ya kuilinda nchi.

Rasilimali za nchi na uchumi wa nchi ni muhimu kuliko mtu yeyote.

Mpina Mungu atamsimamia.
Yule ni Msukuma Halisi.
Hakuna Msukuma Muoga kwenye kutetea Haki na kutetea nchi.
Biteko sioni sifa anazopewa zinatokana na nini?
Biteko Ni aina ya kina Bashe

Lakini Tundu Lisu , Mwabukusi ,Gwajima, Mpina , Heche, Pambalu, Ole Sosopi, Askofu Mwamakula,Askofu, Mbowe,Mdude Chadema, Mwanamapinduzi,Padri Kitima, Shekhe Ponda n.k. Hawa watu historia yao itadumu sana .

NASIMAMA NA MPINA kupinga ufisadi.
CCM byebye 2025.
 
Mwabukusi ana saut kubwa sana aingilie hili jamaa ananguvu ya kuungamisha watu sana alibebe hili tungane
 
Manabii na wanafunzi wengi wa Yesu walikuwa wauaji kabla. Hata Shetani hapo awali alikuwa malaika mkuu.

Watu hujifunza na kubadilika mkuu na tuyazingatie mabadiliko badala ya kuishi kwa historia.

Mkuu kuhusu mfano wa shetani hapana, shetani Kawa malaika kipindi kifupi kuliko anachoishi kama shetani!!! Yazingatiwe mabadiliko ya binadamu ila sio kufikiria shetani!!!

⚖️4Asimwe#
 
Bila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane katika uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina.

Shime watanzania kila mtu aandike katika uzi huu maneno yafuatayo:
"NASIMAMA NA MPINA",

Hii itasaidia kumtia moyo Mpina na kumshinikiza spika Tulia kuachana na njama zake za kumnyamazisha.

NB: Huu siyo uzi wa kupiga stori, andika hayo maneno matatu tu. Comment ya kwanza nimeonesha mfano.

PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
Spika kasimamia kanuni, kwamba ukisema fulani ni muongo unakuwa na kazi ya kuuweka wazi uongo wake.

Hiyo ni kanuni inayoliongoza bunge, kwamba Mpina muda huu afanye kazi ya kuumiza kichwa ili aje na taarifa zenye uhakika wa vyanzo.
 
Mpina na Charles Taylor hawana tofauti. Baada ya kushinda uchaguzi Taylor aliendelea kuwaua hata vijana wapumbavu waliomchagua. Mpina naye ana hasira za kukosa madaraka kwenye utawala huu wa awamu ya 6. Huyo akipewa uwaziri atarudi upya kwenye ukatili wake. Wapumbavu peke yao ndo watasimama na fedhuli kama Mpina.
Watu wa karba hiyo huwa sikubaliani nao
 
Hakuna cha kumsaidia mtu aliyevunja kanuni. Unaagizwa ushahidi halafu unauanika kwenye vyombo vya habari ili upate sympathy. Muache apambane na hali yake.


Mkuu hali ya mbunge kukaa nje ya bunge vikao 10, sio mchezo ukizingatia uchaguzi unakaribia. Wanaomshabikia wamemtanguliza kwenye mteremko akiwa amekalia baisikeli ya mbao!!! 🤣 🤣 🤣

⚖️4Asimwe#
 
Tido ni kama mimi tu. Mpina anazuri gani la kusifiwa? Mara hii mmesahau alivyotesa wafugaji na wavuvi? Hizo kelele ni za kutafuta kauwaziri tu.
✍️📝👍👌👊🤝👏🙏🎁💐🗼🛡️
 
Spika kasimamia kanuni, kwamba ukisema fulani ni muongo unakuwa na kazi ya kuuweka wazi uongo wake.

Hiyo ni kanuni inayoliongoza bunge, kwamba Mpina muda huu afanye kazi ya kuumiza kichwa ili aje na taarifa zenye uhakika wa vyanzo.
Basi itakuwa hujafuatikia sakata hii tangu mwanzo. Hicho unachokisema ndicho Mpina alichokifanya. Amewasilisha ushahidi wake kwa maandishi kwenye ofisi ya spika, kisha akaja kuwajulisha watanzania ushahidi aliopeleka bungeni.

Kilichomkera spika ni Mpina kuwajulisha wananchi ushahidi alioupeleka ofisini kwake (spika), kabla ya ofisi yake kuupitia na kuuchambua. Anadai kwa kufanya hivi Mpina kama anaielekeza ofisi yake kufanya maamuzi kwa shinikizo la wananchi, hivyo ameitafsiri kama dharau.

Upo hapo nyonyo?
 
Hapana. Ushahidi ulishakabidhiwa, lkn ulikuwa bado haujafanyiwa kazi na Kamati ya maadili ya bunge. Spika anadai kwa kufanya hivyo Kamati inapokwa madaraka yake, maana itafanya kazi (itaujadili huo ushahidi) kwa shinikizo la wananchi.
Hapo cha msingi hiyo hoja yake isikilizwe kwa upana wake kabisa bila kujali kwamba alikosea taratibu za kuitoa kwa waandishi wa habari kabla ya kupitiwa kwenye kamati... Dah hii nchi hii yaani ukismsikiliza waziri wakati anawasilisha hoja yake hiyo ya kuamua kutoa vibali vya uagizaji sukari nje unaweza sema ni mtu smart na innocent kabisa kumbe ni lipigaji lisilo na mfano hata kidogo dah! 😭😭😭
 
Alisimamia Sheria.

Tuache chuki.

Pakiwa na Vita Haki ya mwanajeshi kuishi inaondoka kwa ajili ya kuilinda nchi.

Rasilimali za nchi na uchumi wa nchi ni muhimu kuliko mtu yeyote.

Mpina Mungu atamsimamia.
Yule ni Msukuma Halisi.
Hakuna Msukuma Muoga kwenye kutetea Haki na kutetea nchi.
Biteko sioni sifa anazopewa zinatokana na nini?
Biteko Ni aina ya kina Bashe

Lakini Tundu Lisu , Mwabukusi ,Gwajima, Mpina , Heche, Pambalu, Ole Sosopi, Askofu Mwamakula,Askofu, Mbowe,Mdude Chadema, Mwanamapinduzi,Padri Kitima, Shekhe Ponda n.k. Hawa watu historia yao itadumu sana .

NASIMAMA NA MPINA kupinga ufisadi.
CCM byebye 2025.
Sasa acheni kulialia spika anaposimamia kanuni na sheria za bunge. Unawasilisha ushahidi halafu unauanika kwenye vyombo vya habari ili upate huruma? Acha ayaoge.
 
Back
Top Bottom