KERO Wananchi Ubungo Kibangu tunadai hati za viwanja, Manispaa ya Ubungo inatuzungusha

KERO Wananchi Ubungo Kibangu tunadai hati za viwanja, Manispaa ya Ubungo inatuzungusha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi tulinunua viwanja katika eneo la Ubungo Kibangu Jeshini mwaka 2020, wakati Jeshi lilipokuwa linaweka mpaka kati ya maeneo ya wananchi na eneo la Jeshi, Kikosi Na. 671.

Katika zoezi hilo la upimaji na uwekaji wa mipaka, vilipatikana viwanja kadhaa ambavyo vilifanyiwa demarcation na kuwekwa beacons, ambazo hadi sasa zipo eneo husika. Pia, mchoro wa mipango miji uliandaliwa na kuidhinishwa, huku faili la upimaji likipelekwa Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya hatua za kuidhinishwa.

Baada ya sisi kununua viwanja hivyo na kuanza kufuatilia taratibu za kuviendeleza, Mkuu wa Kikosi alileta mgogoro akidai kuwa maeneo hayo bado ni mali ya Jeshi, licha ya kuwepo kwa mipaka na beacons zilizowekwa wakati wa zoezi la upimaji.

Kutokana na mgogoro huo, sisi wamiliki wa viwanja tuliamua kufikisha malalamiko yetu Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jijini Dodoma ili kupata ufafanuzi na suluhisho.

Mwaka 2024, Makao Makuu ya JWTZ Dodoma ilitoa barua kuhusu mgogoro huo na kueleza kuwa, “Eneo lililokuwa likilalamikiwa kuwa ni mali ya Jeshi lilitolewa kwa wananchi hivyo si mali ya Jeshi tena,” na kulielekeza Manispaa ya Ubungo kuendelea na taratibu za kupima na kumilikisha wananchi maeneo hayo.

Pamoja na maelekezo hayo kutoka Makao Makuu ya JWTZ, sisi wananchi bado tunadai kuwa Manispaa ya Ubungo imeshindwa kukamilisha taratibu hizo. Tumekuwa tukifuatilia mara kwa mara kuhusu faili la upimaji, lakini tumekuwa tukizungushwa bila kupewa majibu ya wazi kuhusu hatua iliyofikiwa au sababu ya kuchelewa kulipitisha.

Hali hii imetuweka katika wakati mgumu kwa sababu tunamiliki maeneo hayo lakini hatuwezi kuyaendeleza kwa uhakika bila kupata umiliki halali na hati. Tunaomba Manispaa ya Ubungo itoe ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa kwenye faili la upimaji na kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Makao Makuu ya JWTZ ili wananchi hao waweze kukamilisha taratibu za umiliki wa viwanja vyao kisheria.
 
Back
Top Bottom