Wananchi wa Arusha mlichofanya kwa RC ni dharau kubwa kwa mamlaka za uteuzi; acheni mgomo fungueni mioyo

Wananchi wa Arusha mlichofanya kwa RC ni dharau kubwa kwa mamlaka za uteuzi; acheni mgomo fungueni mioyo

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Wananchi wa Arusha wameingia mitini kumpokea RC mpya. Hii siyo Ishara nzuri kwa kiongozi anayependa kuabudiwa. Vyombo vya habari vilijiandaa kurusha live msafara wake lakini wamekwama kwa kukosekana umati.

Jambo la pili lililowaudhi wananchi wa Arusha ni kitendo cha kuwa na kiongozi anayewaza kugombana na watu kila wakati. Kila anapozungumza anaonyesha kutengeneza maadui kuliko marafiki. Huu siyo uongozi

Jambo jingine nikuchukua magari ya utalii na kuyapeleka KIA ambacho ni tafsiri ya rushwa. Haya magari kwanini wanapoteuliwa wakuu wengine wa mkoa hayalazimishwi kujitokeza kumlaki?

Mkuu wa mkoa wa Mwanza amekwenda kuripoti hakuna misafara, mkuu wa mkoa wa Mara hakuna msafara; Mongela hakuwa na misafara. Kwanini tunaamini kupanga watu kwenye msafara ndio utandaji?

Mkuu wa mkoa ni nafasi ya utumishi siyo siasa; kuchukua magari ya watu binafsi na kufanya nayo siasa ni rushwa. Kwanini tusikemee haya? Kama tunaamini ndio utaratibu basi wakuu wote wa mikoa wawe wanalazimisha misafara kila wanapokwenda tuone kama umaskini unaisha.

Viongozi wa juu jifunzeni kukemea la sivyo itanonekana kuna baraka kutoka juu
 
Wananchi wa Arusha wameingia mitini kumpokea RC mpya. Hii siyo Ishara nzuri kwa kiongozi anayependa kuabudiwa. Vyombo vya habari vilijiandaa kurusha live msafara wake lakini wamekwama kwa kukosekana umati...
Umesema nafasi ya mkuu wa mkoa sio siasa halafu unasema magari yamechukuliwa na kupelekwa kwenye siasa hapo sijaelewa
 
Wananchi wa Arusha wameingia mitini kumpokea RC mpya. Hii siyo Ishara nzuri kwa kiongozi anayependa kuabudiwa. Vyombo vya habari vilijiandaa kurusha live msafara wake lakini wamekwama kwa kukosekana umati...
Paul analazimisha Kiki kwa pikipiki.....Arusha atanyooka
 
Hapa ataondoka kabla ya mwaka.
. Asiletee pigo za kiwakiii. Chuga ni Nchi sio mkoa kama dar aloo.
Utanyooka tu dogo!

Wewe endelea na bango zako uone
 
Wananchi wa Arusha wameingia mitini kumpokea RC mpya. Hii siyo Ishara nzuri kwa kiongozi anayependa kuabudiwa. Vyombo vya habari vilijiandaa kurusha live msafara wake lakini wamekwama kwa kukosekana umati...
gubu ni mzigo mzito sana kuubeba moyoni.....
 
Asee jomba chuga ni wadudu hawanaga ushamba wakushobokea undezii.

ee
Nyie si wadudujiandaeni kuuliwa kwa kupuliziwa dawa maalumu.

Mkandaji wenu yupo hapo chuga
 
Wadudu tutadeal nae... Chuga sio Dar jomba... Hata mazaleee amempanga akamwambia kabisa unaenda Nchi ya wadudu kuwa makini. Huku kingi ni jomba Lema tu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Unajitahidi kujitia moyo.

Kiboko yako yupo hapo chuga
 
Back
Top Bottom