Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Wananchi wa Kaliua - Kazaroho Wala Kiapo cha Kumlinda Rais Samia Mbele ya DC ChuaChua
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Dkt. Rashid ChuaChua amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepeleka Shilingi Milioni 446 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji wa Kazaroho
Aidha, DC Chuachua amesema Rais Samia amepeleka fedha za kutosha Kazaroho kwenye Shule za Sekondari, Shule mbili za Msingi kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa, Mabweni, na Vyoo katika Wilaya ya Kaliua.
"Ndugu zangu Msione vyaelea, vimeundwa na aliyeunda ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishirikiana na Aloyce Andrew Kwezi (Mbunge wa Kaliua) pamoja na diwani mzee Haron" - DC Kaliua, ChuaChua
DC ChuaChua amekwenda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda S. Burian kuzindua mradi wa Maji uliopo Kazaroho
"Kama kuna jambo ambalo mmelifanya ni kumfanya Aloyce Andrew Kwezi kuwa Mbunge wenu (Kaliua). Mmempata Mbunge ambaye kila anaposimama Bungeni anaeleza mambo mazito kwa ajili ya maslahi ya watu wa Kaliua. Mbunge huyu ni tunu mliyopewa na Mwenyezi Mungu, hampaswi kuipoteza" - DC Kaliua, ChuaChua
"Kama kuna mtu analifiziafizia hili Jimbo mwambieni atasubiri sana. Mmepata Mbunge (Aloyce Andrew Kwezi) anayefanya kazi kubwa kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Kaliua. Lazima mumshikilie, mumlinde na kumtunza. Acha afanye kazi kwa ajili ya kutimiza malengo yetu (Kaliua) wana Kaliua" - DC Mhe. ChuaChua